Hivi kwanini waarabu wa Dubai wameuziwa bandari tu badala ya kuuziwa Tanzania yote?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,131
35,174
Nimesikitika sana kusikia waarabu wa Dubai kuuziwa bandari pekee badala ya kuuziwa nchi nzima ya Tanzania. Huku ni kujinyima na kujirudisha nyuma sana.

Madalali wa taifa la Tanzania (Serikali la CCM na bunge la CCM) wamesema kwa kupewa Bandari tu, waarabu wa Dubai wataongeza mapato maradufu, wataboresha miundo mbinu maradufu na kuongeza ajira maradufu kwa muda mfupi sana pale bandarini, yaani muarabu wa Dubai ana uwezo kuleta maendeleo maradufu kwenye kila kitu!

Madalali wa taifa la Tanzania (CCM) wamesema waarabu wale wanaipenda sana Tanzania na wanataka kutusaidia ili tuendelee na kufikia hatua za kimaendeleo kama wao.

Kwa kuanzia tu, lile bunge letu apewe muarabu wa Dubai (muarabu ndio ateue spika, wabunge na watumishi wote wa bunge), Ikulu yetu apewe Muarabu wa Dubai na Mahakama zetu ziwe mali ya muarabu.

Kwanini tusimpe kila kitu halafu tupate kila kitu maradufu kwa muda mchache sana. Na Tanzania ikiwa ni mali ya muarabu wa Dubai, basi Tanzania itakuwa ni sehemu ya Dubai sawa na raia wa Dubai.

Nimeamua kuwaza kiuwendazimu, nimechoka kuwa raia wa Tanzania nisiyekuwa na ajira, pesa wala maana.
 
Tupe kipengele kinachosema wameuziwa bandari
 
Back
Top Bottom