Serikali kutolipa mishahara watumishi kwa kisingizio cha kutojaza majukumu yao kwenye mfumo wa ESS ni unyang'anyi usiotumia Silaha

Ukiachana na hayo yote uliyoaandika,kimsingi watumishi wengi tu wazembe sana,tuvitu vidogovidogo tu hadi tusukumwe sukumwe kama gari bovu hadi wananchi wanatudharau.

Huo mfumo ni mrahisi mnoo lakini nashindwa kuelewa hao laki100 kama ni kweli haiingii akilini wote wawe hawajapewa role na wakuu wao,hawawezi kuwa wengi hivyo.

Acha kila mmoja awajibike ktk eneo lake
Kuna uzembe wa mtu mmoja mmoja , boss na taasis kwa ujumla.
Mfano ukishajili hujui km kunapewa Role, anayetakiwa kukupa Role ni Mkuu wa Idara au Kitengo , Sasa watumishi wengi waliambiwa TU wajisajili basi.
 
We jamaa Acha kutetea uzembe.

Unataka miezi mingapi kujaza hizi forms, kitu cha madakika tu mnataka mbembelezweeeee.

Watumishi wa serekali ni wavivu fullstop. Mnafanya kazi kwa mazoea.

Eti ujambazi, yaani unaambiwa jaza majukumu yako hutaki na unaita ujambazi. Badilikeni nyie watu, dunia inaenda kasi sana hii. Acheni kulea ujinga na uzembe
Kikubwa Serikali ilipe watumishi hakuna uhusiano wowote wa mfumo na ulipaji Mishahara maana haijawai kutoa waraka kuwa usipojisajili mshahara wako haupati zaidi ya matamko ya mawaziri. Lakini wengi ni watumishi wa TAMISEMI
 
Unahisi utakwepa hadi lini? Ni suala la muda tu ulimwengu wote unahamia huko
Sio swala kukwepa, mtu yupo kijijini huko hakuna mtandao anajazaje sasa ? Na hapo ndipo kituo cha kazi ??

Haya kujaza kunatakiwa kila siku ulichofanya hiyo pesa ya bando na gharama ziko hivi unafanyaje sasa ?
 
Sio swala kukwepa, mtu yupo kijijini huko hakuna mtandao anajazaje sasa ? Na hapo ndipo kituo cha kazi ??

Haya kujaza kunakiwa kila siku ulichofanya hiyo pesa ya bando na gharama ziko hivi unafanyaje sasa ?
Mnakwepa kusema mlichofanya kila siku. Na ni sababu hamfanyi kitu.

Uvivu tu
 
Wizi mtupu! Huo mfumo wenyewe kama ilivyokuwa kwa Opras, sidhani kama una tija yoyote ile.
Ni kweli kabisa kiongozi, utakuta wanahangaika na kucheza na maneno/ maandishi mengi kwa mtumishi bila kufuatilia utendaji halisi wa kazi ambao ndio huleta tija.

Mfano ukienda shuleni utakuta walimu wengi wako nje wanaandika maandalio ya wiki nzima au zaidi huku wengine wakiwa hata hawajaingia darasani kwa kuwa tu wanajua wadhibiti ubora ndipo wanapokazia kuliko kukagua maudhui na uwasilishaji wake.

Ni Bora wajikite ktk namna ya kupata uhalisia wa kazi kuliko maandishi mengi ya uongo.
 
Mfumo unahitaji access ya kompyuta na internet, je watumishi wote wanayo hiyo access?

Mwisho wa siku watumishi wanakuwa wanashinda kwenye kumpyuta kujaza taarifa, yaani masaa kadhaa yatakuwa yanaisha kwa kazi hiyo.
Seri
Mbona watumishi wapo wengi tu hawajamaliza kujaza na wamepata mshahara.
Kujaza sio tatizo ila tatizo kama hauna role yaani Mkuu wako labda alijisahau kukupa majukumu ndo imekula kwako hivo.
 
Mfumo unahitaji access ya kompyuta na internet, je watumishi wote wanayo hiyo access?

Mwisho wa siku watumishi wanakuwa wanashinda kwenye kumpyuta kujaza taarifa, yaani masaa kadhaa yatakuwa yanaisha kwa kazi hiyo.
Sio Kila mtu atakumbuka kuingia online. Maana majukumu mengi mtu anayafanya kwa njia ya Mkono.
Shida waliopo wizarani wanahisi wote wanafanya kazi hapo . internet ni bure, computer Kila mtu ana yake, Usafiri ni wa umma, allowance zinafanana, kumbe kuna mtu Yuko Masamburai huko Ngorongoro kupata access internet hadi aende Karatu kilomita 90 kutoka hapo alipo.
 
Serikali ya awamu ya Sita iliachana na mfumo wa kujaza OPRASS kwenye makaratasi (nakala ngumu) badala yake ikatambulisha PEPMIS kupitia mfumo Employee Self Service kwa kifupi ESS.

Ikiwa na maana kwamba taarifa muhimu na za Msingi kuhusu Mtumishi zitakua kwenye mfumo huu.
Ikiwemo
  • Kujaza majukumu na utekelezaji wa majukumu yao.
  • Kupata salary slip kupitia mfumo huu
  • Uhamisho na kupata mkopo kupitia mabenki husika.
Kwa mwezi Februari baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa Utumishi Wilaya walilia kukosa mshahara kwa kisingizio hiki kwamba watumishi walio chini ya taasisi zao hasa Halmashauri hawajajisajili kupitia mfumo huu. Huu ni unyang'anyi usiotumia Silaha.

Ikumbukwe mfumo huu ni Mpya na Elimu haijafikia watumishi hasa waliopo vituoni nikimaanisha kwenye Kata na Vijiji na wengi wao ni wale wazee wengine hata matumizi ya smartphone ni shida, mfano Watendaji wa Vijiji wale wa darasa la 7 , hata baadhi ya walimu hawajajua mfumo huu unavyofanya kazi.

Pamoja na changamoto lukuki kuhusu mfumo huu Serikali bado inachukua jukumu la kufungia mshahara wa Mtumishi wake aliyefanya kazi ofisini kwa siku 28 kisa TU hakujaza Sub Activity au Task na Sub Task kwenye mfumo kama kigezo cha upimaji , wakati kazini amehudhuria na amefanya kazi saa kiutumishi na muda mwingine amefanya kwa kupitiliza

Baadhi ya watumishi wanaangukia kwenye changamoto hii kutokana na Wakuu wao wa taasisi, mfano ikiwa Mkuu wa Idara/ Kitengo hakuwahi kukupa Role ama kwa kujisahau au kutokujua jinsi mfumo unavyofanya kazi maana yake mwezi husika hujafanya kazi kwa mwezi husika. Ikiwa hujaingia kwenye mfumo na huja submit sub task kwa Mkuu wako wa kazi unahesabika kuwa hujafanya kazi yoyote.

Pamoja kuwa Serikali ina nia nzuri kuleta huu mfumo isiwe kigezo cha kunyima watumishi mshahara kisa TU hawajapewa role na kujaza majukumu yao au kufanya tathimini kupitia mfumo huu.

Huu ni unyang'anyi usiotumia Silaha.

Baadhi ya Watumishi hao hao wamepanga wengine wanadaiwa kodi za nyumba.

Baadhi Watumishi hao wamefunga Kwaresima na Ramadhani wanahitaji kununua au kuwanunulia wazazi na ndugu zao chakula kwa ajili ya futari. Baadhi ya Watumishi maisha yao ni magumu hakuna mfano wanategemea huo mshahara kununua mahitaji muhimu Baadhi ya Watumishi wamekopa marejesho yanawasuburi.

Hii inaweza kuleta changamoto kwa baadhi ya Watumishi kuanza kuiba hasa kwa wakusanyaji wa mapato ya Serikali ikiwa ni kufidia mshahara wake aliozuiliwa na Serikali hivo kukosesha Serikali mapato.

Rai yangu
Serikali lipeni watumishi mshahara wa mwezi Machi, watumishi wengi watakaoumia sana sana ni wenye Mishahara ya chini.
umeibua changamoto muhimu sana,

hata hivyo lack of seriousness kwa baadhi ya hao watumishi na huenda pia lack of awareness inaweza kuchangia pakubwa wengi wao kuzama au kutumbukia kwenye changamoto hiyo. Watapitia changamoto, lakini jasho lao haliwezi potea ispokua watachelewa kulifurahia

Lakini pamoja na hayo yote, bado haki inakwenda sambamba na wajibu. Ni muhimu kutekeleza wajibu wetu vema ili kupata stahiki na haki zetu kwa usahihi 🐒
 
Wengi mbona mkuu hawana tasks and subtasks kutoka kwa kiongozi wao na wamepata mshahara. Yani walijisajili tu na hawakujaza chochote.
Mfumo upo hivi ukijisajili Mkuu wako anakupa role na anakupa section , km umejisajili na hukupewa section Hilo ndo tatizo hata huku nilipo wengi hawakujaza task wala sub task lkn walipewa section, km una section hata km hukujaza sub activity au task na sub task mshahara unapata
Sijui km tunaelimishan vzr
 
CCM ni majangili kwenye kivuli Cha chama na yamejitengenezea katiba
 
Mfumo upo hivi ukijisajili Mkuu wako anakupa role na anakupa section , km umejisajili na hukupewa section Hilo ndo tatizo hata huku nilipo wengi hawakujaza task wala sub task lkn walipewa section, km una section hata km hukujaza sub activity au task na sub task mshahara unapata
Sijui km tunaelimishan vzr
Kabisa tuelimishane kiongozi. Kumbe sasa sio kujaza tasks and subtasks ndo unapata mshahara ila kujisajili tu. Na je waliopo masomoni wanajazaje tasks and subtasks?.

Kingine kwenye load repayment and topup naona wengi wanalalamika haifanyi kazi vizuri yani ipo lakini haifiki mwisho.
 
At some point ni uzembe but mi najiulizaga kwanini serikal ikiwa inataka kuchukua hatua serious kama hii haitoi official statement unakuta kitu kinasemwasemwa tu ila official statement hakuna,ili paswa itolewe official statement irudiwe ata three times kwenye mwezi husika wanaotaka kuzuia,hii wanachukua maamuzi kama cia au mossad inaumiza watu
 
Serikali ya awamu ya Sita iliachana na mfumo wa kujaza OPRASS kwenye makaratasi (nakala ngumu) badala yake ikatambulisha PEPMIS kupitia mfumo Employee Self Service kwa kifupi ESS.

Ikiwa na maana kwamba taarifa muhimu na za Msingi kuhusu Mtumishi zitakua kwenye mfumo huu.
Ikiwemo
  • Kujaza majukumu na utekelezaji wa majukumu yao.
  • Kupata salary slip kupitia mfumo huu
  • Uhamisho na kupata mkopo kupitia mabenki husika.
Kwa mwezi Februari baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa Utumishi Wilaya walilia kukosa mshahara kwa kisingizio hiki kwamba watumishi walio chini ya taasisi zao hasa Halmashauri hawajajisajili kupitia mfumo huu. Huu ni unyang'anyi usiotumia Silaha.

Ikumbukwe mfumo huu ni Mpya na Elimu haijafikia watumishi hasa waliopo vituoni nikimaanisha kwenye Kata na Vijiji na wengi wao ni wale wazee wengine hata matumizi ya smartphone ni shida, mfano Watendaji wa Vijiji wale wa darasa la 7 , hata baadhi ya walimu hawajajua mfumo huu unavyofanya kazi.

Pamoja na changamoto lukuki kuhusu mfumo huu Serikali bado inachukua jukumu la kufungia mshahara wa Mtumishi wake aliyefanya kazi ofisini kwa siku 28 kisa TU hakujaza Sub Activity au Task na Sub Task kwenye mfumo kama kigezo cha upimaji , wakati kazini amehudhuria na amefanya kazi saa kiutumishi na muda mwingine amefanya kwa kupitiliza

Baadhi ya watumishi wanaangukia kwenye changamoto hii kutokana na Wakuu wao wa taasisi, mfano ikiwa Mkuu wa Idara/ Kitengo hakuwahi kukupa Role ama kwa kujisahau au kutokujua jinsi mfumo unavyofanya kazi maana yake mwezi husika hujafanya kazi kwa mwezi husika. Ikiwa hujaingia kwenye mfumo na huja submit sub task kwa Mkuu wako wa kazi unahesabika kuwa hujafanya kazi yoyote.

Pamoja kuwa Serikali ina nia nzuri kuleta huu mfumo isiwe kigezo cha kunyima watumishi mshahara kisa TU hawajapewa role na kujaza majukumu yao au kufanya tathimini kupitia mfumo huu.

Huu ni unyang'anyi usiotumia Silaha.

Baadhi ya Watumishi hao hao wamepanga wengine wanadaiwa kodi za nyumba.

Baadhi Watumishi hao wamefunga Kwaresima na Ramadhani wanahitaji kununua au kuwanunulia wazazi na ndugu zao chakula kwa ajili ya futari. Baadhi ya Watumishi maisha yao ni magumu hakuna mfano wanategemea huo mshahara kununua mahitaji muhimu Baadhi ya Watumishi wamekopa marejesho yanawasuburi.

Hii inaweza kuleta changamoto kwa baadhi ya Watumishi kuanza kuiba hasa kwa wakusanyaji wa mapato ya Serikali ikiwa ni kufidia mshahara wake aliozuiliwa na Serikali hivo kukosesha Serikali mapato.

Rai yangu
Serikali lipeni watumishi mshahara wa mwezi Machi, watumishi wengi watakaoumia sana sana ni wenye Mishahara ya chini.
Uwajibikaji haubembelezwi

Actually wanatakiwa kusainishwa forms kabisa kwamba wasipojaza wawe wamejifukuzisha kazi

Hutu mama tunataka kumfanya bibi yetu mzaa baba….. angekua magu ungekuja kulalama huku?

I think madam president kawa mpole sana, time sasa aanze kututandika
 
umeibua changamoto muhimu sana,

hata hivyo lack of seriousness kwa baadhi ya hao watumishi na huenda pia lack of awareness inaweza kuchangia pakubwa wengi wao kuzama au kutumbukia kwenye changamoto hiyo. Watapitia changamoto, lakini jasho lao haliwezi potea ispokua watachelewa kulifurahia

Lakini pamoja na hayo yote, bado haki inakwenda sambamba na wajibu. Ni muhimu kutekeleza wajibu wetu vema ili kupata stahiki na haki zetu kwa usahihi 🐒
Lakini kumbuka huyo Mtumishi ametekeleza wajibu wake ofisini, mfumo huwezi kumnyima mtu haki kisa TU vigezo vya upimaji hajajaza online .
Ikiwa umeme TU ni changamoto na wananchi tunaivumilia Serikali basi Serikali nayo Ina wajibu wa kuvumilia watu wake maana idadi hiyo ilitakiwa kuimsha Serikali na kuanza kuchukua hatua hata ingetoa alert ya miezi 6 hivi kuwa asiyefanya hivi atafanyiwq hivi.
 
Basi wote hao wana matatizo ya akili na sidhani kama hilo shirika linaingiza faida kwa serikali
Mkuu, reply zako zinaonesha wewe ni spoilt brat, umeishishwa mjini tu.

Ni wazi, watumishi wa serikali ni wavuvi, wezi na wakwamishaji wa maendeleo ya wengine kwa 100%.

Unakufahamu kule kwa waziri mkuu? Umewahi kufika? Hilo ni eneo moja tu la hii nchi ambapo watumishi wa serikali wapo kule, sio INTERNET, Umeme tu wanaupata mara moja kwa wiki!

Unashangaa watu kukosa access ya internet kwenye nchi isiyo na;
  • Umeme wa kutosha mijini, hata baada ya miaka 60
  • Jiji moja tu halijajitosheleza kwa maji safi na salama
  • Road network ni km zisizozidi 100,000 katika pande la nchi lenye zaidi ya sq km 940k
  • Madarasa na madawati ya kutosha
  • Uelewa wa umuhimu wa matumizi ya choo
  • Na udhibiti wa magonjwa ya mlipuko yatokanayo na uchafu
  • Madawa ya kutosha
  • Na wazalendo wanaoweza kudhani MAGARI YA KIFAHALI sio muhimu kuliko vifaa tiba.

Dar es salaam, kwa miaka 60 imeshindikana yote kuwa na umeme, maji, barabara, hospitali, shule etc NDO USHANGAE KUKOSEKANA KWA INTERNET VIJIJINI?

Kaulize waungwana, wakuambie jinsi watu wanavyopoteza muda na nguvu kufuata mishahara yao.
 
At some point ni uzembe but mi najiulizaga kwanini serikal ikiwa inataka kuchukua hatua serious kama hii haitoi official statement unakuta kitu kinasemwasemwa tu ila official statement hakuna,ili paswa itolewe official statement irudiwe ata three times kwenye mwezi husika wanaotaka kuzuia,hii wanachukua maamuzi kama cia au mossad inaumiza watu
Majina yalitolewa tarehe 21 tarehe 23 mtu unakata mshahara wake muda huo huo changamoto bado ni kubwa.
Watu zaidi ya laki wengi mnoooooooo.
 
Back
Top Bottom