Mundungus Fletcher
JF-Expert Member
- Jun 7, 2009
- 327
- 79
Mpango huu wa serikali hauna tija na ni ufujaji wa rasilimali ya nchi. Nina uhakika wataalam hawajashauri njia hiyo ya kutatua kero ya foleni.
Nimeesikia mapendekezo ni kujenga fly over pale ubungo na tazara. Cha kujiuliza ni kwamba zitakuwa na tija? Kumbuka hapatakuwa na flyover pale shekilango, wala magomeni au fire au hata makutano ya morogoro na bibi Titi. Je, traffic itakayopita ubungo toka mbezi itaflow vipi katika junctions hizo? Nikitafakari sana nakumbuka ule utaratibu wa njia tatu wa enzi za Lowassa!
Naishauri serikali hii ya ccm iache kukurupuka na ifanye mambo kwa kuzingatia ushauri wa kitaalam na kwa kufanya tafiti. Hizo pesa za fly over zitumike kuboresha feeder roads kwanza!
kaka hujasoma nyakati tu... hawa jamaa hawana nia ya kupunguza foleni ila wanataka kutumia fly over kwa ajili ya kuombea kura... trust me.. ni kama U Dom walijenga kwasababu walijua wataambia watanzania angalia tumejenga chuo kikubwa... ndo hivyo hivyo watakavyosema 2015 kuhusu hizo fly over... wait and see