Serikali kuanza kujenga barabara za juu kupunguza msongamano wa magari Dar!

Mpango huu wa serikali hauna tija na ni ufujaji wa rasilimali ya nchi. Nina uhakika wataalam hawajashauri njia hiyo ya kutatua kero ya foleni.

Nimeesikia mapendekezo ni kujenga fly over pale ubungo na tazara. Cha kujiuliza ni kwamba zitakuwa na tija? Kumbuka hapatakuwa na flyover pale shekilango, wala magomeni au fire au hata makutano ya morogoro na bibi Titi. Je, traffic itakayopita ubungo toka mbezi itaflow vipi katika junctions hizo? Nikitafakari sana nakumbuka ule utaratibu wa njia tatu wa enzi za Lowassa!

Naishauri serikali hii ya ccm iache kukurupuka na ifanye mambo kwa kuzingatia ushauri wa kitaalam na kwa kufanya tafiti. Hizo pesa za fly over zitumike kuboresha feeder roads kwanza!


kaka hujasoma nyakati tu... hawa jamaa hawana nia ya kupunguza foleni ila wanataka kutumia fly over kwa ajili ya kuombea kura... trust me.. ni kama U Dom walijenga kwasababu walijua wataambia watanzania angalia tumejenga chuo kikubwa... ndo hivyo hivyo watakavyosema 2015 kuhusu hizo fly over... wait and see
 
Hzo flyng over ztajengwa dar ipi hii ambayo ni unplanned au ndo hyo Kigambon new city?
 
Mipango mingi utekelezaji hafifu..
Mara mradi wa mabasi yaendayo kasi, mara Flyovers, mara upanuzi wa barabara nk.. Jamani em rekebisheni hizi barabara za uswazi ndipo mfikirie hayo magorofa yenu ya angani..
Miafrika ndivo tulivyo.

tatizo kila mpango ukiwekwa watu wanaenda mahakamani.. Mabas ya kasi watu hawakukubaliana na fidia wakaenda mahakaman ukasitishwa. Barabara za mitaan zinatakiwa kuendelezwa na halmashauri za manispaa ndo hazitengenezwi wanakimbilia kuweka mabango tu. Flyovers zitajengwa watang'ang'ania kuweka mabango. Mie simo
 
Mpango huu wa serikali hauna tija na ni ufujaji wa rasilimali ya nchi. Nina uhakika wataalam hawajashauri njia hiyo ya kutatua kero ya foleni.

Nimeesikia mapendekezo ni kujenga fly over pale ubungo na tazara. Cha kujiuliza ni kwamba zitakuwa na tija? Kumbuka hapatakuwa na flyover pale shekilango, wala magomeni au fire au hata makutano ya morogoro na bibi Titi. Je, traffic itakayopita ubungo toka mbezi itaflow vipi katika junctions hizo? Nikitafakari sana nakumbuka ule utaratibu wa njia tatu wa enzi za Lowassa!

Naishauri serikali hii ya ccm iache kukurupuka na ifanye mambo kwa kuzingatia ushauri wa kitaalam na kwa kufanya tafiti. Hizo pesa za fly over zitumike kuboresha feeder roads kwanza!

Hii yote ni zile ahadi za Mkubwa za wakati wa Campaing ....sasa anagalia kitu kinacho kuja hapo.......vitu havitafanyika kitaaluma ili tu watu wapate cha kuwaeleza wapiga kura 2015.....hakuna atakaye fikiria juu ya miaka 10 -15 au 20 ijayo....Swali la kwanza la kujiuliza hivi feeder roads zote za Dar zinapitika?......zimejengwa kwa kiwango gani? kujenga Fly overs wakati mipango miji yenyewe issue....Bila ya kufanya maamuzi magumu ya kubomoa badhi ya mitaa... na maeneo mingine ili kuwa na mpango mzuri wa jiji bado ni bure.......!!!! Serekali ilitakiwa kujipanga kwa kuupanga upya mji wa Dar... na sio kukimbilia kujenga Fly overs pekee....take it from me hata baada ya ujenzi wa hizi fly overs katika junction pekee zitawezesha kuhamishia foleni sehemu nyingine tuu kwahiyo foleni bado Dar haitaisha.......
 
barabara za juu hapa anamanisha kuvuka junction tu na kwa maana hiyo ni fupi(span less than 1 kilometer). kwa maana hiyo siyo gharama kihivyo. Zinabebwa na nguzo tu. Serikali inaweza kufanya hivyo na kupunguza foleni kwenye junction lakini huko yanakoelekea magari je?(mjini) .maana huko sasa yataingia kwa haraka zaidi na kwa wingi.FOLENI ZAIDI MJINI
 
hawa jamaa hawana nia ya kupunguza foleni ila wanataka kutumia fly over kwa ajili ya kuombea kura... trust me..

Trust me, hata hayo maandamano ya CDM hayana lengp la kutatua shida za watanzania bali kuombea kura tu.
 
Badala ya kukimbilia hizi flyovers kwa nini wasiimarishe feeder roads? Mfano
Mwananyamala-Sinza
Makongo-Kimara
Wazo-Kibaha
 
Mwacheni Magufulu wa watu atujengee barabara za kuruka...

Wataka Kuruka wakati Kutambaa shida ndugu yangu!Dr.Magufuli angeomba orodha ya barabara mbovu ambazo zikijengwa msongamano utaisha,Jamvi halikopeshi?
Mie Mkweche sipendi kuishi Dar ajili ya Msongamano!
Chanzo Msongamano ni kwamba barabara chache!
 
Mh.Magufuli amedai bungeni kwamba serikali itaanza ujenzi wa barabara za juu Dar! Mie Mkweche najiuliza kweli kunahaja ya kujenga barabara za juu wakati barabara nyingi za mitaa ni Mbovu? kwanini zisijengwe za mitaani kwanza ili kupunguza msongamano maneke ubovu wa barabara za mitaani ni chanzo namba moja cha msongamano dar
wakijenga barabara za mitaa hawatapata nafasi nzuri ya kuiba hela umma so lazima washinikize miradi mikubwa ambayo mwisho siku itakua muda mrefu nao watakua washachota mipesa kibao kupitia project hizo....Umesahau richmond ? Yangu macho...
 
Nifahamuvyo mimi kuna sababu za msingi zilizofanya serikali iombe msaada Japan. Hii ni sababu wajapan ndio wametoa pesa ya kugharamia upembuzi yakinifu na wako tayari kutoa pesa za kujenga fhizo flyovers. Inawezekana kabisa kuna watanzania huko ughaibuni wenye utaalam wa kujenga hizo barabara za juu. Swali ni kwamba tukiwatumia hao nani atagharamia?
<br />
<br />
unadhan hao wajapan wanasaidia burebure? Ni just xchange of our natural resources kwa msaada.
 
Hebu tusiibeze serikali wakati inapotaka kufanya mambo ya maana. Flyovers Dar ni muhimu na sioni kwa nini mtu atilie shaka kwamba serilkali haitaweza. Tuipe muda serikali ijenge hizi flyovers
Endelea kulaka, tunauliza uwezekano wa kufanikiwa kwa hizo fly over ikiwa za kawaida zimeshindikana, we unasema tunaibeza! Na unashauri eti tuicha ifanye kazi yake, hebu tuambie mradi wa maana uliofanikiwa zaidi ya kuishia wizi mtupu. Sleep well!!!!
 
Hivi ni kweli wanajanvi kuwa wajapani hutoa pesa za miradi kama hiyo na kuisimamia?kama jibu ni ndio barabara ya kilwa kuanzia round about ya bandari hadi mbagala ilijengwe chini ya viwango Magufuli na wizara yake wamekataa kuipokea sasa wajapani haohao kupitia JICA wanakuja na hizo barabara za juu aaaaah!!!!!!Mungu atunusuru zikijengwa chini ya viwango tumekwisha tutaporomoka na magari na kuongeza idadi ya yatima.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom