Serikali kuanza kujenga barabara za juu kupunguza msongamano wa magari Dar! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali kuanza kujenga barabara za juu kupunguza msongamano wa magari Dar!

Discussion in 'Major Projects in Tanzania' started by MKWECHE, Aug 2, 2011.

 1. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mh.Magufuli amedai bungeni kwamba serikali itaanza ujenzi wa barabara za juu Dar!
  Mie Mkweche najiuliza kweli kunahaja ya kujenga barabara za juu wakati barabara nyingi za mitaa ni Mbovu?
  kwanini zisijengwe za mitaani kwanza ili kupunguza msongamano maneke ubovu wa barabara za mitaani ni chanzo namba moja cha msongamano dar
   
 2. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Barabara za chini zimewashinda za juu wataziweza?
  Ni sawa na kutaka kujenga choo kabla ya nyumba
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Aug 2, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Nilisikia kuwa barabara za juu zimeanza kujengwa, mbona mimi sijaona zikijengwa huko TAZARA ama Ubungo? Hili si changa la macho kweli?
   
 4. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Foleni zinaboa dsm jamani. Ubungo-posta saa moja na nusu.!
   
 5. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mshauri wao sijui ni Nani!Kila wakiwaza utatuzi wa Jambo inakuwa ni tatizo zaidi!
  Barabara za chini bado sasa wanakimbilia za Juu!
   
 6. m

  mamanalia JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2011
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 671
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hawa watu walioshindwa hata kuunganisha tegeta na mbezi kimara ndo wataweza kujenga fly over kweli!
   
 7. JS

  JS JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hizo fly overs hizo msishangae baada ya muda pot-holes kibao mpaka mnaona magari ya wanaopita chini.......kwi kwi kwi kwi
   
 8. d

  dotto JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Watatumia ndege zipi kuzipitia. Msongamano DAr haumalizwi na hizo ndege za barabara bali kuwa na usafiri wa uhakika wa mabasi yanayochukua idadi kubwa ya abiria. Wana Dar wengi wamenunua magari yao ili waweze kufika kazini bila jasho la kubanana na kukanyagana kwenye aka vipanya na pia kusubiria magari ambayo nayo hayapo kwa wakati. Leo hii kukiwa na public transport ya uhakika hakuna mtu anayeweza tumia mafuta,tyre na matengenezo mengineyo kwenye gari anayetaka kwenda na gari ofisini. Umbumbumbu wa MAgufuri na wenzake ndo unaowapofusha na barabara za juu angani. Hiyo option ni baada ya kuona kuwa hakuna alternative nyingineyo. Kuna mabarabara mengi tu DAR mabovu ambayo yangeimarishwa pia. Vipaumbele vyao 10% za flayover!
   
 9. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Magufuli pamoja na jitahada zake za kufanya mambo kama yanavyotakiwa naona anaanza kudanganywa na mafisadi. Iwaje serikali iwaombe wajapan waje kujenga barabara za juu wakati Watanzania wengi ndio waliobobea shughuli za kujenga barabara za juu hususan Canada, USA, UK, nk. Hivi anaona watanzania ni vilaza kiasi hicho? What is very special kuhusu barabara za juu? Huu ni wizi namshauri awasiliane na wabongo kwenye nchi tajwa hapo juu wamsaidie na waweze kuwekeza kwa Watanzania wenyewe na sio kila kukicha kuwatajirisha wageni.

  Swala lingine ni la kujenga nyumba 47/48 Dar na mbili Idodomia. Hivi mandate ya serikali kujenga nyumba haiko chini ya NHC? Kwa nini kila wizara inataka kujenga nyumba zake na sio kutumia shirika la NHC? Je wamegundua nini ambacho NHC hawawezi kufanya? Au ndio danganya toto ile ile ya kukwapua mpunga wa walipa kodi?
   
 10. m

  mafutamingi JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 171
  Trophy Points: 60
  Hebu tusiibeze serikali wakati inapotaka kufanya mambo ya maana. Flyovers Dar ni muhimu na sioni kwa nini mtu atilie shaka kwamba serilkali haitaweza. Tuipe muda serikali ijenge hizi flyovers
   
 11. m

  mafutamingi JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 171
  Trophy Points: 60
  Nifahamuvyo mimi kuna sababu za msingi zilizofanya serikali iombe msaada Japan. Hii ni sababu wajapan ndio wametoa pesa ya kugharamia upembuzi yakinifu na wako tayari kutoa pesa za kujenga fhizo flyovers. Inawezekana kabisa kuna watanzania huko ughaibuni wenye utaalam wa kujenga hizo barabara za juu. Swali ni kwamba tukiwatumia hao nani atagharamia?
   
 12. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Lakini bwana Kaka kabla ya kukimbilia huko kwenye Fly Overs Umejiridhisha kwamba Barabara zote za Kawaida Zinapitika vizuri?Au Ubovu wa barabara nyingi ndo unatufanya sote tupende kupita barabara nzuri!Serikali imalizie barabara za chini kwanza!
  Tuipime vipi wakati Kipimo Chaonesha za Chini Bado
   
 13. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #13
  Aug 2, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi nadhani serikali imeomba msaada kwa Serikali ya Japan ili ku finance Mradi wa ujenzi wa fly overs. Kwa maana hiyo Japan iki finance italeta na wataalamu wake. Sijui kama hao wataalamu wa kitanzania walioko huko ughaibuni wataweza ku finance hiyo miradi?

  Kuhusu suala la nyumba mimi najua NHC wanajenga nyumba kibiashara zaidi ila TBA wanajenga nyumba kwa ajili ya biashara na kwa ajili ya viongozi wa serikali. Labda sasa hizi taasisi ziunganishwe kwa kuwa zote ni za serikali kama ilivyokuwa Msajili Jumba na NHC.
   
 14. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,601
  Likes Received: 2,458
  Trophy Points: 280
  Mipango mingi utekelezaji hafifu..
  Mara mradi wa mabasi yaendayo kasi, mara Flyovers, mara upanuzi wa barabara nk.. Jamani em rekebisheni hizi barabara za uswazi ndipo mfikirie hayo magorofa yenu ya angani..
  Miafrika ndivo tulivyo.
   
 15. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #15
  Aug 2, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Nadhani anachozungumzia Magufuli ni suala la "Funding" kwenye mradi wenyewe. Kama serikali haina fedha zake yenyewe inabidi iombe ufadhili kutoka nje, na kwa hili Japani kupitia JICA ndio wanaoombwa kusaidia gharama za ujenzi. Ikumbukwe kuwa ni JICA hao hao waliotayarisha na kuandaa "[FONT=&amp]Dar es Salaam Urban Transport Policy and Master Plan" kwa gharama ya serikali ya Japani. Kama ilivyo kawaida Serikali ya Japani hutumia washauri na wakandarasi kutoka Japani katika miradi yaake yote ya ujenzi wa barabara inayoifadhili[/FONT] hapa Tanzania.

  Na hata kama serikali ingekuwa inatumia fedha zake yenyewe, bado kusingekuwa na uhakika kwa watanzania kutumika katika ujenzi huo, ukizingatia kuwa sheria ya manunuzi kwa miradi mikubwa kama hiyo inataka kufanyike ushindani wa kimataifa "International Bidding".
   
 16. simeu

  simeu Member

  #16
  Aug 2, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo Magufuli naona anadanganyika sana na ka imani wananchi walikonako kwake, yeye anajibu kwa hisia sana kiasi kwamba anapindikua kuweka mbwebwe nyingi ambazo zinaweza ruin reputatiion and trust wadanganyika waliyonayo kwake.
   
 17. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #17
  Aug 2, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  A ENDELEA KUWA NA MAFUTA MINGI MWISHO WAKE HEART ATTACK. VYA KUNYONGA VIMEWASHINDA VYA KUCHINJA MTAWEZA? KWA KIPI ZAIDI WAKATI 40pc YA BAJETI MNASUBIRI KUTOKA SCANDINAVIAN COUNTRIES? HEBU JENGENI BARABARA YA MBEZI TO MAJUMBA 6 KWA KIWANGO CHA LAMI HALAFU MUONE.
   
 18. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #18
  Aug 2, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145

  na barabara za juu zitasaidia.. nashangaa sana kuna watu JF wanapinga huu mpango dah!...
   
 19. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #19
  Aug 2, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Waziri amesema kazi ya kujenga barabara za mitaa ni kazi ya halmashauri za ilala,temeke na kinondoni na si kazi ya wizara.pia amewataka wabunge wa dar wanatakiwa kuungana na kuzisimamia manispaa.
   
 20. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #20
  Aug 2, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Kupinga barabara za juu DSM ni kupinga maendeleo,huwezi kuwaweka wafanyakazi masaa matatu katika foleni na ukasema unataka uchumi wa nchi ukue,Kujenga barabara za juu ni moja kati ya ufumbuzi wa tatizo lakini kuna haja ya kupanua mji kwa maana ya baadhi ya ofisi na shughuli nyingine kuhamia nje ya mji sio kila kitu Posta na Kariakoo tu.SHIDA YANGU NI JE SERIKALI HII YA ****** ILIYOKOSA UELEKEO INAWEZA KWELI KUJENGA HIZO BARABARA AU NI SIASA NYEPESI TU WANAFANYA?
   
Loading...