KERO Kero Barabara ya Kilwa eneo lijulikanalo kama Kokoto kuelekea daraja la Mzinga jijini Dar

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba kuulizia, ni nini hasa kinachoshindikana kwa serikali kukijenga kipande hiki cha Barabara kisichozidi hata kilomita mbili na kuondokana na usumbufu unaosababisha msongamano wa magari katika eneo hili?

Kipande hiki ni chembamba na kina mteremko mkali na daraja ambapo mara kwa mara husabanisha foleni hasa magari makubwa yanaposhindwa kupanda kilima ama kuharibika.

Eneo hili ni nyeti kwa sababu ndiyo lango kuu la kupitisha magari karibu yote yanayoelekea mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na hata Mbeya kutokea Dar na pia nchi za Msumbiji na Malawi.

Iwapo tumeweza kujenga fly-over kadhaa na hata madaraja kama vile daraja la mto Wami na madaraja ya baharini na ziwani kwa gharama kubwa, je nini hasa kinaifanya serikali kushindwa kuona kipaumbele juu ya barabara hii na hususan kipande hiki kifupi? Je Waziri wa Ujenzi hajaona umuhimu wa kufanya marekebisho makubwa na kuondoka kero hii kwa watumiaji?

Karibu tushirikishane kwa maoni na ushauri zaidi, Ahsante.
 
Uko sahihi mkuu, hicho kipande nakifahamu sana maana ni njia yangu kuelekea Mikoa ya home..
Sometimes natoka home kisemvule kuelekea city centre hapo kokoto panasumbua sana..
Serikali ifanye juu chini itengeneze hii barabara kutoka Rangi3 hadi mkuranga
 
Back
Top Bottom