Serikali achana na kujenga barabara za mwendokasi

kiwiko

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
1,308
2,070
Ni kupoteza muda na fedha.

Tatizo la Dar sio usafiri wala daladala. Tatizo ni barabara finyu zisizoendana na uwingi wa magari.

Mfano mzuri ni kuanzia Kimara mpaka Kibaha foleni imepotea baada ya kujengwa barabara ya njia nane. Kwa nini zisijengwe barabarani kuu zote kama hivo muone kama kutakua na foleni tena.

Ujenzi wa mwendokasi haujasaidia kumaliza foleni na infact barabara zenye mwendokasi ndio foleni imekua kali zaidi kutokana na barabara kufinywa.

Barabara ya mbagala nayo imekua kero baada ya kujengwa mwendokasi.

Jengeni barabara za njia nane acheni daladala zifanye kazi kuliko hio mwendokasi iliogeuka adhabu kwa wananchi.
 
Yaani umeongea ninachojisemea Kila siku, mbaya Zaidi plan iliyopo barabara ya mikocheni baada ya mwendokasi itakuwa njia moja Kila upande na njia kati mwendokasi, vivyo hivyo Tabata hadi Segerea Huku ni kujirudisha nyuma na kuongeza foleni, Sio lazima Watu wote kupanda mwendokasi
 
Hapo ni kujirudisha nyuma bora wabomoe barabara za mwendokasi zilizopo ili barabara zibaki njia sita.
 
Kuna Plan kuwa mbovu na kuna execution kuwa mbovu ingawa proposed plan ni nzuri....

Niambie kwanza on paper Mwendokasi ni nini? Na the best way ya kuondokana na congestion ni ipi ? Ushasema tatizo ni ufinyu wa Barabara ambazo haziendani ni wingi wa magari (Kwahio unadhani the cheapest long term alternative ni kufanya nini )?
 
Mwendokasi lengo lake sio kuondoa foleni... mwendokasi lengo hasa ni kutoa huduma ya uhakika na nafuu kwa wakazi WA Dar..

Daladala sio reliable kila ruti...na zinapandisha nauli hasa usiku na kuamua kupaki wakijisikia...
Public transport zinahitajika kila nchi ...

Barabara finyu ni tatizo lingine ..
Na mwendokasi ni kitu kingine
 
Ni kupoteza muda na fedha.
Tatizo la Dar sio usafiri wala daladala. Tatizo ni barabara finyu zisizoendana na uwingi wa magari.
Mfano mzuri ni kuanzia Kimara mpaka Kibaha foleni imepotea baada ya kujengwa barabara ya njia nane. Kwa nini zisijengwe barabarani kuu zote kama hivo muone kama kutakua na foleni tena.
Ujenzi wa mwendokasi haujasaidia kumaliza foleni na infact barabara zenye mwendokasi ndio foleni imekua kali zaidi kutokana na barabara kufinywa. Barabara ya mbagala nayo imekua kero baada ya kujengwa mwendokasi.
Jengeni barabara za njia nane acheni daladala zifanye kazi kuliko hio mwendokasi iliogeuka adhabu kwa wananchi.
Ukijua lengo la mwendokasi basi utakuja kuedit uzi wako....

1. Barabara hata ujenge njia 20 itafikia kipindi kutakua na foleni.
2. Foleni nyingi hutokea kwenye intersections. Mfano foleni ya ubungo imetatuliwa na just overpass mbili.
3.
 
Mwendokasi lengo lake sio kuondoa foleni... mwendokasi lengo hasa ni kutoa huduma ya uhakika na nafuu kwa wakazi WA Dar..

Daladala sio reliable kila ruti...na zinapandisha nauli hasa usiku na kuamua kupaki wakijisikia...
Public transport zinahitajika kila nchi ...

Barabara finyu ni tatizo lingine ..
Na mwendokasi ni kitu kingine
Hiyo huduma,inayotolewa mbona ni mateso
Ngoja ruti ya mbagala ianze abiria lazima wangoe siti

Ova
 
Mwendokasi lengo lake sio kuondoa foleni... mwendokasi lengo hasa ni kutoa huduma ya uhakika na nafuu kwa wakazi WA Dar..

Daladala sio reliable kila ruti...na zinapandisha nauli hasa usiku na kuamua kupaki wakijisikia...
Public transport zinahitajika kila nchi ...

Barabara finyu ni tatizo lingine ..
Na mwendokasi ni kitu kingine

Huduma ya uhakika na bora ya usafiri haiwezekani kama foleni bado ni tatizo…
 
Sio shida kwan mixed lane kwa sasa zna njia mbili kwenda na kurudi ,traffic inatokea coz ya sababu nje ya alizotoa mleta mada
 
Ukijua lengo la mwendokasi basi utakuja kuedit uzi wako....

1. Barabara hata ujenge njia 20 itafikia kipindi kutakua na foleni.
2. Foleni nyingi hutokea kwenye intersections. Mfano foleni ya ubungo imetatuliwa na just overpass mbili.
3.

Ukiwa na barabara pana mji mzima hauhitaji tena mradi wa mwendokasi. Pale barabara ya kuanzia kimara to kibaha zile daladala zimegeuka mwendokasi. Tungepanua barabara zetu kusingekua na ulazima wa kuwa na BRT. Na tungetumia gharama kidogo kuliko hio BRT.
 
Sio shida kwan mixed lane kwa sasa zna njia mbili kwenda na kurudi ,traffic inatokea coz ya sababu nje ya alizotoa mleta mada

Njia mbili bado ni barabara finyu kwa miji mikubwa kama Dar….tungeweka kipaumbele kwenye kujenga njia nyingi kusingekua na foleni…miji mikubwa duniani wamejenga barabara pana na flyovers ndio maana miji mikubwa michache duniani ina BRT kwa vile hakuna haja kama una barabara pana.
 
Hapo ni kujirudisha nyuma bora wabomoe barabara za mwendokasi zilizopo ili barabara zibaki njia sita.
Mamlaka zinazohusika zinashindwa kutoa ushauri, Tanroads kunani!? Nimeiona hii michoro acheni kutusababishia usumbufu, barabara bila over taking ni kusababisha usumbufu, Mtu anawahi Mambo yake mtu mbele ameharibikiwa, ana stress zake basi akuzuie kuwahi!? Angalieni Msimbazi na changombe hamuoni huu usumbufu mkajifunza!? My Goodness my country
 
Tujiunge tuwapigie kelele wataamka usingizi WA pono walipo Hawa Tanroads, wanasifiwa for nothing
 
Njia mbili bado ni barabara finyu kwa miji mikubwa kama Dar….tungeweka kipaumbele kwenye kujenga njia nyingi kusingekua na foleni…miji mikubwa duniani wamejenga barabara pana na flyovers ndio maana miji mikubwa michache duniani ina BRT kwa vile hakuna haja kama una barabara pana.
Na ndiposa inabidi kuwepo madaraja mengi (flyovers) kwasabab foleni inasababishw na intersection mkuu hizi roundbout,traffic lights ni kipengele
 
Mamlaka zinazohusika zinashindwa kutoa ushauri, Tanroads kunani!? Nimeiona hii michoro acheni kutusababishia usumbufu, barabara bila over taking ni kusababisha usumbufu, Mtu anawahi Mambo yake mtu mbele ameharibikiwa, ana stress zake basi akuzuie kuwahi!? Angalieni Msimbazi na changombe hamuoni huu usumbufu mkajifunza!? My Goodness my country
Kwa case kama hii sasa tunahitaji kujenga shoulder zenye uwezo wa kuaccess any interuption kweny roadway kam ivo ajali au kuharibika
 
Njia mbili bado ni barabara finyu kwa miji mikubwa kama Dar….tungeweka kipaumbele kwenye kujenga njia nyingi kusingekua na foleni…miji mikubwa duniani wamejenga barabara pana na flyovers ndio maana miji mikubwa michache duniani ina BRT kwa vile hakuna haja kama una barabara pana.
Tuungane tuwaamshe Tanroads usingizini, fikiria Nyerere road, barabara ya airport ilikuwa njia nne 1982, Sasa miala 43 mtu WA Tanroads ameruhusu baada ya mwendokasi Bado iwe njia nne hizo hizo, Hawa Watu wanashida Gani!? Hadi washauriwe na kamati ya Bunge!? Akili zao zipo wapi!?
 
Kwa case kama hii sasa tunahitaji kujenga shoulder zenye uwezo wa kuaccess any interuption kweny roadway kam ivo ajali au kuharibika
Nenda Msimbazi Watu wamekwepa hiyo barabara, Sasa Kuna changombe keko, Sijui ikianza KAZI itakuwaje, watakuwa wameongeza tatizo Kwani njia Ina Malori sana na hakuna Mbadala, Sasa tatizo hilo Hilo wamelileta Tabata, Mikocheni to kawe from Morocco, Mandela road inatakiwa njia Sita, wao wameruhusu njia nne ziendelee, this is Madness with Tanroads, unajenga barabara huna emergency Parking ya lorry bovu with cost na unafikiria Hawa Watu wanataka kupunguza foleni!! My poor Country, my poor Tanroads, always crying for their poorly planning
 
Back
Top Bottom