Serikali: Kila mtanzania atapaswa kumiliki laini moja ya simu, ukitaka ya pili unaomba TCRA

Kama unatumia serengeti huruhusiwi kunywa castle au ukitumia uhai hurusiwi kunywa Kilimanjaro
Unajiita una akili
 
Lakini kweli simu ni mawasiliano hivi kweli Unaweza kuongea na simu mbili Kwa wakati mmoja? Halafu hivi ukiulizwa sababu za kuwa na laini mbili ni zip? Sidhani kama kuna mwenye jibu litalojitosheleza
Umeacha tabia yako ya kukojoa kitandani?
 
Hivi yule msanii aliyewatungia wapinzani wataisoma # natamani kujua Hali yake kwa sasa teh teh!

Ova
 
BINAFSI SIONI TATIZO LA MTU KUWA NA LAINI ZAIDI YA MOJA CHAMSINGI LAINI ZOTE AWE AMEZISAJILI KWA MAJINA YAKE NA VITAMBULISHO VYAKE.

WATU WANA LAINI TOFAUTI KWA MATUMIZI TOFAUTI.KWA MFANO,MTU ANAKUWA NA LAINI KWA SHUGHULI KAMA ZA MPESA,AIRTEL MONEY,TIGO PESA
AU SHUGHULI ZA KIKAZI TU,MFANO VYUONI KUDAHILI WANAFUNZI NK,
VILEVILE LAINI KWA AJILI YA MATUMIZI YA KAWAIDA KUWASILIANA NA NDG NK.

IKUMBUKWE MITANDAO INAZO BEI TOFAUTI ZA VIFURUSHI NA INTERNET BUNDLE.

INA MAANA WATU PIA HAWATARUHUSIWA KUWA NA GARI ZAIDI YA MOJA? PIKIPIKI ZAIDI YA MOJA NAYO ITAKATAZWA.

USHAURI WANGU KWA VIONGOZI WANGU.
LAINI ZIENDELEE KWA SABABU ZINALIPA KODI.KILA MTUMIAJI ANAPONUNUA VOCHA AU KUFANYA MAWASILIANO KWA LAINI YOYOTE ANALIPA KODI SIONI TATIZO HAPO.
HUO NI MCHANGO WANGU NAOMBA UPOKELEWE.
 
Ametoa sababu zozote zilizopelekea hayo maamuzi?

Simu nazo wanataka tumiliki ngapi?
Basi wafungie mitandao yote ubaki mmoja tu wanaoutaka wao.
Wakiamka wanakurupuka na matamko, nchi nyingine watu hufanya upembuzi yakinifu na utafiti wa muda mrefu ili kutoa mapendekezo ya kutekeleza jambo flani kwa manufaa flani, na wadau watapewa muda wa wao kutoa maoni yao na mawazo yao kufanyiwa kazi.

Sasa huku kwetu ni tamko tu, mitandao ipo mingi ina maana raia ana uwezo wa kumiliki laini nyingi kwa kadili ya makampuni ya Simu yalivyo.
 
DAR: Serikali imesema itaanza kudhibiti umiliki holela wa 'line' za simu na hivyo chini ya usajili wa 'line' kwa alama za vidole mtu akitaka kusajili 'line' zaidi ya mbili itabidi ajaze fomu ya kueleza kwa nini anataka 'line' ya pili.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Atashasta Nditiye aliyeeleza kuwa katika udhibiti huo watashirikiana na NIDA kupitia vitambulisho vya Taifa.

Amesema kuwa mtu akitaka kusajili 'line'ya pili ya simu Kampuni za simu zitamuona na kujua kuwa tayari ana 'line' ya kwanza, hivyo lazima atajaza fomu maalum kueleza kwa nini anataka 'line' ya pili.

Aidha, Naibu Waziri amesema kuwa kabla ya mwaka huu kuisha 'line' za
simu zitaanza kuuzwa kwenye maduka rasmi na mtu anayesajili atachukuliwa alama za vidole na picha yake


Hii itaathiri ununuzi wa simu ...Baadhi wana simu hadi tatu na pengine hata nne...mauzo ya simu za mkononi yatapungua mno...na mapato ya taifa kupitia kodi kwa simu (kama zipo) nayo yatapungua...serikali ifikirie kwa makini suala hili..mimi binafsi ninavyo 'vitochi' vyangu vitatu na line tatu...
 
Back
Top Bottom