Serikali: Kila mtanzania atapaswa kumiliki laini moja ya simu, ukitaka ya pili unaomba TCRA

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,795
11,958
DAR: Serikali imesema itaanza kudhibiti umiliki holela wa 'line' za simu na hivyo chini ya usajili wa 'line' kwa alama za vidole mtu akitaka kusajili 'line' zaidi ya mbili itabidi ajaze fomu ya kueleza kwa nini anataka 'line' ya pili.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Atashasta Nditiye aliyeeleza kuwa katika udhibiti huo watashirikiana na NIDA kupitia vitambulisho vya Taifa.

Amesema kuwa mtu akitaka kusajili 'line'ya pili ya simu Kampuni za simu zitamuona na kujua kuwa tayari ana 'line' ya kwanza, hivyo lazima atajaza fomu maalum kueleza kwa nini anataka 'line' ya pili.

Aidha, Naibu Waziri amesema kuwa kabla ya mwaka huu kuisha 'line' za simu zitaanza kuuzwa kwenye maduka rasmi na mtu anayesajili atachukuliwa alama za vidole na picha yake

 
Wafanye hivi wafukuze hayo makampuni ya simu tubaki na TTCL..Kuna vijiji mpaka sasa tukienda kutembea line moja tu inashika..Tena vingine mpaka sasa kuna vijiji havina mawasiliano.Mnaacha mambo kama hayo mnahangaika na line ......matokeo ya kuwa na watu ambao ........................................
 
Back
Top Bottom