kali linux
JF-Expert Member
- May 21, 2017
- 2,303
- 6,123
Hata steve jobs mwenyewe hakutaka watoto wake watumie iPhoneSijui serikali inasubiri nini, ukizingatia kwamba kampuni inayounda simu za iPhone inamilikiwa na watu wenye utata wa kijinsia.
Na sisi kama Tanganyika tumedhamiria kulinda maadili yetu kwa jasho na damu. Lazima tupinge kweli kweli hadi mishipa ya shingo ipasuke.
Ni unajisi, hatuwezi kuruhusu matumizi ya iphone huku tukijua kuwa waundaji wake wanajihusisha na yale maswala! Kwanini? Turudi posta na kwenye umizimu.
Hatuwezi kukataa nguruwe kisha tukala mchuzi wake.
Mimi na wanakijiji wenzangu wa ardhi ya mbambadu tumedhamiria kupambana na kila picha ya upinde tutakayoiona popote hata kwenye gazeti. Tutafoka.
Serikali ya mama samia ihakikishe inafungia simu zote za iphone. Tulinde MILA zetu za kitanganyika.