BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 328
- 414
SERIKALI IZINGATIE HAYA SAKATA LA KUPANDA BEI YA MAFUTA NCHINI ILI YASHUKE.
Na Bwanku M Bwanku.
Jana Ijumaa Mei 06, 2022 kwenye Gazeti la TANZANIA LEO Ukurasa wa 6 nimechambua Vita ya Urusi na Ukraine ilivyopaisha Sakata la Kupanda kwa Bei ya Mafuta kwenye Soko la Dunia kulikoathiri Bei Duniani kote ikiwemo nchini kwetu ambako Bei imeendelea kupanda na kupaa mwezi hadi mwezi. Kupitia Makala hii na kwa unyenyekevu mkubwa sana, nimeishauri Serikali yangu kuzisitisha kwa muda au kuzifuta baadhi ya tozo na kodi kwenye Mafuta hasa zile zisizoenda moja kwa moja kwenye Maendeleo ili kumtua mzigo huu mzito Mtanzania wa kupaa kwa Bei ya Mafuta.
Tanzania mpaka sasa ina tozo na kodi zaidi ya 19 kwenye Mafuta hivyo licha ya Bei ya Mafuta kupanda kwenye Soko la Dunia lakini Kodi na tozo hizi zinachangia pia pakubwa kupandisha Bei nchini, hivyo Kodi kama ya TASAC, EWURA, TBS, Excise Duty na zingine kama hizo ambazo haziendi kwenye Maendeleo moja kwa moja, Serikali ichukue hatua ya kuzisimamisha kwa muda au kuzifuta kwa kipindi hiki cha mpito ambacho Dunia na Taifa linapitia kupaa kwa Bei ya Mafuta ili ku-rescue situation kwasababu Bei hizi zinavyozidi kupanda, inazidi kupandisha Bei ya bidhaa na huduma pia na kuzidi kuongeza ugumu wa maisha maana mafuta ni Runner wa Uchumi.