Donkey
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 1,431
- 1,449
Unajua watu wanasema tunazalisha mchele mwingi. Je mnazalisha na kugawana Kwa watu wenye uhitaji na uhaba wa Chakula. Lishe katika familia nnyingi ni ngumu sana. Watu wanakula mlo mmoja na watoto wengi wanakwenda shule bila kula chochote mpaka mchana au jioni akirudi nyumbani, na anaweza kurudi nyumbani akakuta swaumu bila mfungo kamili. Halafu watoto wengi wanatembea umbali mrefu kwenda shule na kurudi nyumbani. Utakuta wengi wanasimamisha magari njiani wapate msaada wa usafiri, Chakula na usafiri ndiyo changamoto kubwa inayowaathiri wanafunzi wengi kutokuwa makini kwenye masomo.Huo mchele umepewa jina, unaitwa mchele wa bashe, magufuli naye alipewa samaki, samaki wale wa wachina wakaitwa samaki wa magufuli. Sasa kama hawautaki huo mchele watupe sie wengine tuule tuone kama tutapata madhara