Serikali iwalipe wakulima wa zao la korosho madeni ya mwaka 2018

DustBin

JF-Expert Member
Jun 3, 2021
544
558
Nawasalimu kwa jina la JMT..

Kama kichwa kinavyojieleza. Kwanza nianze kwa kusema kwmba mimi sio mkulima wa zao hilo, lakini pia sio mwenyeji wa mikoa yenye umaarufu wa kilimo cha zao hilo. Hivyo naandika haya sio kwamba nina maslahi yangu, hapana..! Nimeona niwasemee wahusika kwani nina amini wenye jukumu watasoma uzi wangu na kuchukua wazo langu huwenda likaleta natija, na hayo ndio yatakua mafanikio yangu ya uandishi.

Juzi wakati napata kifungua kinywa kwenye mgahawa mmoja hivi wa watu wa kawaida (second class) nilikaa meza moja na watu wawili, mmoja akiwa wa makamo kidogo na mwingine anaendana na rika langu. Katika mazungumzo huyu wa makamo akasema "hivi kaka pesa zetu zile za 2018 serikali itatulipa kweli?" Akimuuliza mwenzi huku akikunja chapati alizokua akizisindikiza kwa hai ya rangi. Yule mwenzie akasema "Mzee wangu acha tu..! Hizi pesa kama zingekua sisi ndio tunadaiwa na serikali, tungadaiwa na tozo ya kichelewesha kulipa, lakini tuendelee kumuomba Mungu huenda siku moja wakatukumbuka."
Niligundua kuwa wao ni wakulima au walijihusisha na masuala ya zao hilo la korosho kutokana na maongezi yao yaliyoendelea. Mimi sikutaka nidakie maongezi yao ili niweze kupata taarifa za kutosha. Mwisho wakawa wanalalamika tu kwamba fedha zao za halali hawana uhakika kama watazipata. Nikasikia wanataja majina ya watu maarufu nabkuonesha namna hani wasivyolisemea jambo lao kwa serikali, nikahisi waliowataja watakua ni wabunge wao.

Kiufupi kuna baadhi ya watanzani wenzetu bado hawajaanza kuihisi ile Kasi Ienezayo Tabasamu (KAITA), miongoni mwa kundi hilo ni wakulima wa zao la korosho ambao mwaka 2018 waliuza korosho zao na bado hawajalipwa. Na wengine waliambiwa hawatolipwa kwa kigezo walishukiwa hienda hizo korosho hawakuzivuna kwenye mashamba yao bali itakuwa wamezinunua kwa njia waliyoiita chomachoma..! Mbali na kuwakagua na kukagua mashamba yao na kujirodhisha kuwa korosh zie zimetoka kwenye mashamba yao bado hawajalipwa gedha yao mpaka hiyo juzi nilipokua nawasikia hao jamaa wakilalamika.

Nije kwa upande wa Serikali yetu inayoongozwa na Mheshimiwa Raisi Samia Suluhu Hassani ambae kwa kauli zake ameweka bayana kiwa serikali yake haiitaji dhulma. Kwa kauli hiyo hiyo Mama naomba usikilize kilio hiki cha hawa wakulima waliouza korosho zao mwaka 2018 mpaka leo hawajalipwa...!

Bila shaka nina imani hili litaangaliwa na kupewa kipaumbele...!! Kazi Iendelee...
 
Bana shangazi apambane sana alete pesa kulipa ndugu zake huko na yeye chini kwa chini...
 
Back
Top Bottom