Dar na Pwani zaongoza kwa kuwa na Wagonjwa wa Red Eyes, Mikoa 23 yabainika kuwa na maambukizi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,417
5,778
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya, Profesa Pascal Ruggajo, mikoa inayoongoza kwa ugonjwa wa Macho Mekundu (Red Eyes) ni Dar es Salaam na Pwani, ambapo Dar es Salaam imefikia wagonjwa 6,412, Pwani wagonjwa 4,041, Dodoma 363, Morogoro 307, Mtwara 193, Shinyanga 193, Tanga 190, Lindi 101.

Amesema Mikoa mingine ni Katavi ina jumla ya wagonjwa 94, Njombe 81, Ruvuma 77, Arusha 42, Mwanza 40, Mbeya 37, Songwe 33, Rukwa 31, Kilimanjaro 31, Geita 18, Singida 17, Kigoma 13, Simiyu 9, Mara 5 pamoja na Tabora 4.

Hata hivyo, Wizara imeendelea kusisitiza jamii kuzuia kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa huo kwa kuzingatia usafi binafsi na kanuni za Afya ikiwa ni pamoja na Usafi wa mikono na uso, Kuzuia kugusa macho kadri uwezavyo, kunawa mikono na maji tiririka na sabuni au na Kwa kutumia vipukusi mara kwa mara.
 
hizi takwimu za kupika! wamechukua waalioenda tu hospitali! nenda kariakoo katika watu 10 kuna 5 wana Red eye
 
Back
Top Bottom