Serikali ipo tayari kukutana na Chadema...kulikoni?

Hii niserekali ya ajabuajabu, jana alikuwa Makamba, leo Wasira kesho ni Chilingati na keshokutwa Selina kombani! Yaani ni kuongeaongea mpaka 2015

Wasira sasa hivi anafanya kazi zake kama PR wa serikali. Nadhani kauli hii imetoka kwenye kinywa sahihi.
 
Nafikiri kuna pressure za ndani na nje ambazo zimeanza kuisumbua serikali, kwanini imebadilika ghafla namna hii, halafu nafikiri pia uchaguzi wa Ivory Coast umechangia pressure, Tanzania mbali ya kuwa na matatizo ya uchaguzi bado vyama vya upinzani havikwenda nje ya sheria vina solve kwa ustaarabu na si kutoa watu mabarabarani au kujitangaza washindi kama ilivyofanyika Ivory Coast, mataifa yameliona hilo.
 
Kwanza maongezi yaanze mengine yatajulikana at least Wassira kaonyesha kuwa na busara zaidi Makamba na Kombani
 
Hizi siri zinatufanya tuwalipe DOWANS bilion 185 kama tumesimama vile Ah!
 
Serikali always it capitalizes on mambo haya ni siri inauma sana.Ila tuombe mungu atuweke hai tuje tushuhudie aibu watayopata hawa kina JK, Nkapa na wengine maana yote yatawekwa wazi.Lakini cha kusikitisha ni kuwa hatutawashuhudia akina RA kwani wana uraia wa nchi mbili hawana muda wataanza mbele.
 
Tayari Dhamiri zimeanza kuwasuta Kikwete na serikali yake!!!!! Wanaona mbele giza zito!!!!!, ndiyo maana wameanza kutafuta pa kupumulia na kutokea!!! Wasubiri vikao vya bunge vianze basi, mbona mapema mno?????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!Inafikia mahali mwizi anajuta kwa nini ameiba!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kikwete tayari ameanza kuona dalili mbaya si mbali kutoka hapa! Yeye akitaka watanzania wamsamehe na kusahau, afanye haraka kutekeleza sera ya Chadema kuhusu kuundwa Tume Huru ya Uchaguzi, na mchakato wa dhati Kuandika Katiba Mpya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! ili kabla ya 2015 tuwe na Tanzania Mpya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Huwezi kuwa na Tume huru ya uchaguzi kwa katiba iliyopo. Kwanza uanze mchakato wa Katiba utakaotengeneza mazingira ya kuwa na Tume huru ya uchaguzi. Uhuru wa Tume ya Uchaguzi utategemea sana na madaraka atakayokuwa nayo rais juu ya uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Uchaguzi na ushiriki wa wasimamizi wa uchaguzi - yaani wakurugenzi wa miji na manispaa mbalimbali nchini - ambao kimsingi wanawajibika kwa wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa.
 
Mijusi Kafiri imebanwa kwenye mlango na macho yamewatoka pima, huku wakiachia unyende.

Wabunge wa Upinzani kama kweli ni Wapinzani basi waungane na CDM ili kuzidi kuongeza Pressure.

Hawa watu hawana aibu. Kama unategemea dhamira iwasute, basi imekula kwako na utasubiri sana.

Nafikiri tunaendelea vizuri. Slaa na kundi lako kaza kamba. Mliokuwa mnaona hii njia si nzuri, jibu mnalo sasa.

Mgomo baridi kwa Kikwete utamlazimisha tu akae chini na kubadili mambo Tanzania.
 
Tayari Dhamiri zimeanza kuwasuta Kikwete na serikali yake!!!!! Wanaona mbele giza zito!!!!!, ndiyo maana wameanza kutafuta pa kupumulia na kutokea!!! Wasubiri vikao vya bunge vianze basi, mbona mapema mno?????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!Inafikia mahali mwizi anajuta kwa nini ameiba!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kikwete tayari ameanza kuona dalili mbaya si mbali kutoka hapa! Yeye akitaka watanzania wamsamehe na kusahau, afanye haraka kutekeleza sera ya Chadema kuhusu kuundwa Tume Huru ya Uchaguzi, na mchakato wa dhati Kuandika Katiba Mpya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! ili kabla ya 2015 tuwe na Tanzania Mpya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Hawa watu hawana Dhamiri hata kidogo, na kama ipo basi imejaa kutu. Hawana utu zaidi ya kujali matumbo yao wenyewe tu. Hawana uchungu na wananchi wa Tanznaia hata kidogo. Wanachofanya ni kwa sababu hawana njia ya kutokea kwa sababu wamekaliwa kooni kila kona. Ukweli unabaki pale pale kua CCM na serikali yake hawana nia ya kuongea na chadema. Kinachofanyika sasa ni kijaribu kudanganya jumuiya ya kimataifa kuwa wana mapenzi mema na taifa hili na kuonyesha kua wana nia ya kuongea na chadema.

Unadhani kama waliweza kudanganya kupeleka bajeti iliyochakachuliwa kwa jumuiya ya kimataifa wanashindwa kufanya igizo la kukutana na Chadema? Hawa watu ni wasanii by default. Hawana lolote, na wanajua kuwa kikombe cha usanii, ubadhirifu na uchakachuaji wao kumejaa na kufurika.
 
Kisiasa zaidi, yaani uhuru wetu tulivyoupata kwa domo ndivyo na nchi tunavyoiongoza kwa domo tu, wana utashi wa kweli?
 
Tuwe na mipango; What we will do if a year after election will pass away and no any agreement about new KATIBA?
 
Swala hapa hakuna kulemba CCM wameshaona madai ya CDM kuhusu katiba mpya ni ya msingi ndo wanajifanya wanataka mazungumzo.Swala liwekwe bayana tunataka katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi na sio usiri siri,Duh CCM mnataka kuchakachua mpaka maongezi..!
 
Bara HAKUNA mambo ya MWAFAKA wa viongozi kugawana madaraka bila kushirikisha wananchi kama ambavyo CCM walivyoamua kuridhiana kule Visiwani.

Hapa wenye mada za Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi ni si Vijana kupitia CHADEMA. Hivyo hakuna usiri wowote katika mazungumzo. Kila kitu kweupe mchana sote tuuone. Sisi tunataka mabadiliko ya kweli na wala si kuanza na mianya ya mikutano ya siri, HAPANA!!!

Bahati nzuri sana, CHADEMA hawawezi kuruhusu mambo kama hayo ya usiri usiri katika mambo ya msingi kama haya.
zanzibar hawakuamua viongozi kuunda serikali ya umoja wakitaifa bali wananchi walipiga kurayamaoni kuamua yes or no,nawale wa yes walishinda,na ndio sasa wameunda serikali ya umoja wakitaifa,usikurupuke mkuu fatilia kwa undani kuhusu zenj ndio badae uandike.
 
Makamba alisema hawana haja ya kukutana na mpinzani yoyote kujadili haya masuala leo waziri kutoka chama hicho anasema vinginevyo...
Wanaendelea kurukaruka..wananchi tunataka mjadala utakaozaa Katiba mpya..

Aliyesema anae taka kukutana na serikali hapo mwanzoni sio Mbowe ????, hebu kuweni ni fikra sahihi. Alichosema Wasira ni kuwa wao wapo tayari kukutana na si CHADEMA tu bali na hata vyama vingine vilivyo bakia + taasisi zingine, milango ipo wazi, ila mazungumzo yawe ni kwa maslahi ya Taifa na yasiwe vilevile ya udini, hapo kuna shida gani???. Suala la mwafaka halipo CHADEMA ilishindwa kwenye uchaguzi huru na wa haki wao watulie wajipange kwa ajili ya 2015.
 
Swala hapa hakuna kulemba CCM wameshaona madai ya CDM kuhusu katiba mpya ni ya msingi ndo wanajifanya wanataka mazungumzo.Swala liwekwe bayana tunataka katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi na sio usiri siri,Duh CCM mnataka kuchakachua mpaka maongezi..!

Hivi wewe upo Tanzania kweli ? suala la katiba mpya serikali imeisha sema halipo, waziri wa sheria ameisha litolea kauli, sasa kama CHADEMA mwataka kwenda kwa ajili ya kuzungumzia katiba mpya watakuwa wehu basi, mtu umeisha ambiwa hilo halipo.
 
Huwezi kuwa na Tume huru ya uchaguzi kwa katiba iliyopo. Kwanza uanze mchakato wa Katiba utakaotengeneza mazingira ya kuwa na Tume huru ya uchaguzi. Uhuru wa Tume ya Uchaguzi utategemea sana na madaraka atakayokuwa nayo rais juu ya uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Uchaguzi na ushiriki wa wasimamizi wa uchaguzi - yaani wakurugenzi wa miji na manispaa mbalimbali nchini - ambao kimsingi wanawajibika kwa wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa.

Kutengeneza katiba mpya ni gharama na inachukua muda sio chini ya miaka 10, kwa hiyo msijidanganye kuwa 2015 tutakuwa na katiba mpya. Suala la katiba mpya halikuwa kwenye ilani ya CCM , na wao hawafanyi mambo kwa shinikizo za watu wasio itakia mema nchi hii
 
Back
Top Bottom