Serikali ipo tayari kukutana na Chadema...kulikoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ipo tayari kukutana na Chadema...kulikoni?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Dec 7, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  SERIKALI imesema iko tayari kukaa meza moja na chama cha upinzani cha Chadema au taasisi nyingine yoyote itakayotaka kujadiliana kuhusu mustakabali wa taifa.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira alisema kuwa serikali iko tayari kwa mazungumzo hayo iwapo yataweka mbele maslahi ya taifa.


  Kauli ya Wassira imetolewa wakati Chadema ikiendelea na msimamo wake wa kutoyatambua matokeo ya uchaguzi wa urais, ikitaka kuundwa kwa tume huru ya kuchunguza utangazaji wa matokeo hayo; kuandikwa kwa katiba mpya na kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi.


  Chadema, ambayo ilitangaza msimamo huo mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu, ilithibitisha kwa vitendo kauli hiyo wakati wabunge wake walipotoka kwenye ukumbi wa Bunge wakati Rais Jakaya Kikwete akianza kukihutubia chombo hicho.


  Baadaye, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza kuwa chama hicho kiko tayari kukaa meza moja na serikali au taasisi yoyote kujadili suala hilo kwa kuzingatia maslahi ya taifa.


  Lakini katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alibeza kauli hiyo ya Mbowe kwa kusema kuwa chama hicho tawala hakina muda wala sababu ya kuketi pamoja na wapinzani hao na kwamba baada ya rais kupatikana, siasa sasa zinahamia bungeni.


  Jana Waziri Wassira alitoa kauli tofauti na ya katibu wake mkuu alipoiambia Mwananchi kuwa wako tayari kukaa meza moja na Chadema, chama au taasisi yoyote ikiwamo za dini na kwamba mazungumzo watayoyalenga ni yale yatakayohakikisha yanaweka mbele maslahi ya taifa.


  "Lakini nasisitiza serikali haina mgogoro na viongozi wa dini au chama chochote bali milango ipo wazi kwa vyama vyote 18 na taasisi zote," alisema waziri huyo ambaye aliwahi kuwa kwenye upinzani baada ya kuihama CCM na kujiunga na NCCR-Mageuzi miaka ya tisini.


  "Majadiliano yasichukue sura ya kisiasa au udini kwa kuwa kufanya hivyo hakutafanikisha kufikiwa kwa maslahi bora ya baadaye ya nchi.

  "Lengo la serikali ni kuhakikisha taifa hili linalifikishwa mahali ambapo amani na utulivu itaendelea kuwepo."

  Hata hivyo, Waziri huyo alisema kama kutatokea matatizo au kutoelewana, serikali ina njia na taratibu zake inazozitumia kukutana na walengwa kutatua hali hiyo na kwamba hatua hizo huwa hazitangazwi kwenye vyombo vya habari.


  Wakati akifafanua msimamo huo wa Chadema kwa waandishi wa habari, Mbowe alisema mazungumzo watakayoyalenga ni yale yatakayohakikisha kuwa madai yao yanafikiriwa kwa kina huku maslahi ya taifa yakiwekwa mbele.


  Mbowe alisema wanafurahi kuona kuwa kitendo chao cha kutoka bungeni wakati wa hotuba ya Rais Kikwete kimesaidia kuibua mjadala mzito nchini ambao iwapo utapewa nafasi ya kujadiliwa bila kuweka ushabiki wa kisiasa, nchi inaweza kupata mabadiliko makubwa siku za usoni.


  Alitoa mfano kauli ya waziri mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba na Jaji Mkuu Augustino Ramadhani ambao walikaririwa wakisema kuwa suala la katiba mpya ni muhimu.


  "Maoni kama haya, ambayo yanatoka kwa watu wazito kama hawa, yanaonyesha kuwa kitendo chetu kimeamsha mjadala wa maana kwa taifa hili," alisema.


  Chadema, ambayo ilionekana kama haingesimamisha mgombea urais baada ya Mbowe kuamua kugombea ubunge wa Jimbo la Hai, iliibukia kuwa mpinzani mkuu wa CCM baada ya kumtangaza mbunge wa zamani wa Karatu, Dk Willibrod Slaa kuwa mgombea urais.


  Dk Slaa, ambaye alikuwa akivutia maelfu ya watu kwenye mikutano yake ya kampeni ambako alikuwa akihubiri elimu ya bure na upunguzaji wa bei za vifaa vya ujenzi, alitangaza kutokubaliana na mwenendo wa utangazaji matokeo ya uchaguzi wa rais na kuitaka Tume ya Uchaguzi (Nec)kusimamisha zoezi hilo.


  Lakini Nec iliendelea na utangazaji matokeo na baadaye kumtangaza Jakaya Kikwete kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais, tamko ambalo liliifanya Chadema kutangaza msimamo wake wa kutotambua matokeo ya uchaguzi wa rais.


  CHANZO: Mwananchi
   
 2. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  source pls
   
 3. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Something is wrong somewhere.
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Dec 7, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Talk is cheap
   
 5. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mwananchi Leo!
   
 6. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Watakaaje na vyama vya siasa na mazungumzo yasiwe ya kisiasa?
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwani iliyokataa kukaa meza moja ni Serikali au Chadema? ndio uliowaona wakitoka Bungeni? nashangaa na huu uandishi! Sio Chadema waliorudi?
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hatutaki mambo ya CUF kuolewa AMA kuwa vimada wa CCM!
   
 9. Sambah

  Sambah Member

  #9
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wanataka mwafaka ndo watakavyo sema kwani kuna ugomvi hapa? haki itendeke majadiliano kujadili nini waafri ni hopeless kabisa. nenda kaangalie kule kenya? nenda kwa mugabe na sasa tz malizia na ivory cost.
   
 10. m

  mams JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Na mtafanikiwa, nyie wote ni wamoja na lengo liwe ni kuwatumikia watanzania
   
 11. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,077
  Likes Received: 4,660
  Trophy Points: 280
  Thanks luteni, And U Dar Es salaam u have mental disorder, almost chizi ww,
  but luteni the biggest, wrong defined & misused word here is MASLAHI YA TAIFA MBELE, tena najisikia vibaya sana
  wanatamka hovyo theoretically while they do opposite, kama maslahi ya Taifa yangewekwa mbele kusingekuwa
  na ufisadi, worst contracts, magari luxury ya bei ya uongo, ATC, TRL, EPA tusingekuwa nayo, na watu wa kuwalaumu ni CCM na serikali yake, sasa Wasira kwanza he should know practical definition what is Maslahi ya Taifa,(najua anajua ila yy anaongea maneno, vitendo tofauti) kila wakati, Maslahi ya taifa, maslahi ya Taifa, but for them opposite is true, no faith on him
   
 12. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Bara HAKUNA mambo ya MWAFAKA wa viongozi kugawana madaraka bila kushirikisha wananchi kama ambavyo CCM walivyoamua kuridhiana kule Visiwani.

  Hapa wenye mada za Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi ni si Vijana kupitia CHADEMA. Hivyo hakuna usiri wowote katika mazungumzo. Kila kitu kweupe mchana sote tuuone. Sisi tunataka mabadiliko ya kweli na wala si kuanza na mianya ya mikutano ya siri, HAPANA!!!

  Bahati nzuri sana, CHADEMA hawawezi kuruhusu mambo kama hayo ya usiri usiri katika mambo ya msingi kama haya.
   
 13. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #13
  Dec 7, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii niserekali ya ajabuajabu, jana alikuwa Makamba, leo Wasira kesho ni Chilingati na keshokutwa Selina kombani! Yaani ni kuongeaongea mpaka 2015
   
 14. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #14
  Dec 7, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  I guess you might be right; these thugs must have been squeezed somewhere.
   
 15. papason

  papason JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280


  ni marufukuuu!!!!!
   
 16. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #16
  Dec 7, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Makamba alisema hawana haja ya kukutana na mpinzani yoyote kujadili haya masuala leo waziri kutoka chama hicho anasema vinginevyo...
  Wanaendelea kurukaruka..wananchi tunataka mjadala utakaozaa Katiba mpya..
   
 17. UWEZO_WAKO

  UWEZO_WAKO Member

  #17
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Hata hivyo, Waziri huyo alisema kama kutatokea matatizo au kutoelewana, serikali ina njia na taratibu zake inazozitumia kukutana na walengwa kutatua hali hiyo na kwamba hatua hizo huwa hazitangazwi kwenye vyombo vya habari.:embarrassed:???!!!!
   
 18. October

  October JF-Expert Member

  #18
  Dec 7, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Serikali haina ujanja, ni lazima ikae chini na Chadema itake isitake.
  Jeuri yao sasa inawatokea puani baada ya kila wanachokishika kuporomoka.Tazama Dowans ilivyowaumbua mpaka wanajikanyaga. Ona uchakachuaji mwingine wa Bajeti iliyowasilishwa kwa IMF na donor community--Hii niaibu ya Karne.
  Ukweli ni kwamba JK na serikali yake wamepoteza uhalali wa kuaminiwa na International Community ndio maana wanajaribu kuja na kauli za kujifanya wanataka kuzungumza na Chadema. Hii yote ni geresha tu kwa vile hawana nia na maslahi ya Taifa hili. Hawafanyi hivi kwa kupenda kwao bali kwa vile maji yamewafika shingoni ndio maana wanafurukuta.
   
 19. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #19
  Dec 7, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,407
  Likes Received: 3,738
  Trophy Points: 280
  Ndiyo kawaida yao............. WANATISHIA NYAU HALAFU WANASIKILIZIA.............
   
 20. nyondoloja

  nyondoloja Senior Member

  #20
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  inashangaza mazungumuzo yanayohusu masiraiya watanzania yawe siri kwafaida yanani?
   
Loading...