Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,842
- 10,765
Lazima kuwe na chombo cha ku regulate operation ya makanisa ya kilokole. Mimi naona watu wakishaingia huku especially wanawake wanatekwa ufahamu kabisa.
Mimi kuanzia leo nimempiga marufuku mke wangu kwenda kwenye kanisa lake kama anataka kuendelea kuishi na mimi arudi kanisa la lutheran ambako tumefungia ndoa yetu takatifu.
Yani mke wangu amekuwa mjinga kabisa na haya makanisa muda wote ni kukimbilia kanisani tu, atafunga bishara yake haraka haraka ahakikikishe anakimbilia kanisani. Leo hii mtoto anaumwa lakini anamwacha hata kumpa dawa kisa eti anakwenda kanisani. Kuna mtu wa maana sana anakuja home kwa ajili ya mkutano wa kibishara lakini mama anaona akimbilie kanisani. Yani nyumba chafu, kitanda hakitandikwi kisa kanisa.
Nasema haya makanisa yakome yanapoteza wake zetu.
Yaani makanisa yaadhibiwe kwa sababu ya mkeo? Hata hiyo ndoa yako si takatifu kama unavyodhani, unless ni ya ki-dotcom. Unakiuka misingi ya ndoa halafu unasingizia ulokole? Mbona ki-takwimu asilimia kubwa ya wanawake waliookoka ni wake bora? Waume zao hawana presha tena. Wewe utakuwa na tatizo, acha kunyoosha kidole kushambulia institutions kwa upungufu wako.