naona hua taarifa za kutosha, karudie kufanya utafiti
pili muulize vizuri mkeo Mungu gani anayemwambia asimtibu mwanao, asitandike kitanda wala kufanya usafi. Mungu mwenyewe kabla ya kuwatembelea waisraeli aliwataka kufanya usafi maeneo yote, aliwaagiza kuchimba shimo kujisaidia na kufukia kinyesi, kufua nguo na kuoga na kuhakikisha mazingira yote kuwa safi. nina shaka ameangukia katika makanisa ya wachungaji wa mshahara. hakuna kanisa la kilokole la namna hiyo. kaa na mkeo muulize vizuri akueleze anasali wapi lete taarifa kamili tukupashe habari.
hata Yesu alipokuja alisisitiza usafi ndio maana alifikia mahali akawaosha mikono na miguu wanafunzi wake, unajua hilo.Mungu wetu ni msafi na ni mwanamazingira wa kwanza. hakuna kiumbe yeyote aliyewahi kuipamba dunia na kuifanya kuwa safi kumpita Mungu