Serikali ipige marufuku makanisa ya kilokole

Serikali ipige marufuku makanisa ya kilokole

Status
Not open for further replies.
Sio siri ulokole umeshavunja ndoa nyingi hapa nchini. Hapo waanzilishi wa haya makanisa watasema wanajenga au wanabomoa? Wawe wanaweka na semina za ndoa na malezi sio kufukuza pepo tu.

Seminars huwa zinakuwepo sana tu mkuu...
 
Ni kweli kuna tatizo.
Kuna makanisa ati asili yake ni brazil.na mchungaji ni mbrazil.
Kuna mengi ya south na nigeria.
Haya ya nigeria yana walaghai wasichana wadogo na kuwafanya kama slave wa ngino.
Wanawatumia kupata permit za kukaa Tz
Ipo haja ya kuangalia vibali hivi vya makanisa ya nje ya kilokole.
Watu wanafanywa mazuzu hawataki kazi hawataki dawa.
Kuna watu wanakufa kijinga ati wakiumwa badala ya kwenda hospital wanafanyiwa maombi.
Hata lile kanisa la yule mama lwakatare ni hatari namfahami dada mmoja alikufa hivi hivi baada ya kukatazwa kula dawa na badala yake wwchungaji fake ati wanamuimbew
 
Kabla ya makanisa kufungwa ufungwe kwanza wewe mwenyewe.Huyo mkeo umshukuru Mungu kwanza anaujua hata mlango wa kanisa au unataka aende kama madada poa?.Soma andiko hili likusaidie hapo ulipo usiwe na hasira maana uzungumze naye atakuelewa maana ulimpenda toka mwanzo ndiyo maana ulikuwa husemi sasa labda unakata kona umeanza kumchukia?

SOMA MHUBURI SURA YA 9 NA MSTARI WA 9.

Msatari unasema;

Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye,siku zote za maisha yako ya ubatili wako,ulizopewa chini ya ya jua;siku zote za ubatili wako,kwa maana huo ni sehemu yako ya maisha; na katika taabu zako ulizozitaabika chini ya jua.Amen
 
Lazima kuwe na chombo cha ku regulate operation ya makanisa ya kilokole. Mimi naona watu wakishaingia huku especially wanawake wanatekwa ufahamu kabisa.

Mimi kuanzia leo nimempiga marufuku mke wangu kwenda kwenye kanisa lake kama anataka kuendelea kuishi na mimi arudi kanisa la lutheran ambako tumefungia ndoa yetu takatifu.

Yani mke wangu amekuwa mjinga kabisa na haya makanisa muda wote ni kukimbilia kanisani tu, atafunga bishara yake haraka haraka ahakikikishe anakimbilia kanisani. Leo hii mtoto anaumwa lakini anamwacha hata kumpa dawa kisa eti anakwenda kanisani. Kuna mtu wa maana sana anakuja home kwa ajili ya mkutano wa kibishara lakini mama anaona akimbilie kanisani. Yani nyumba chafu, kitanda hakitandikwi kisa kanisa.

Nasema haya makanisa yakome yanapoteza wake zetu.

Unafahamu kuna uhuru wa kuabudu?
tatizo lako na mkeo usilete huku Kama umeshindwa kuongoza nyumba yako.
mke wako ni mchafu wa kawaida usisingizie makanisa ya kilokole
pole sana na mkeo huyo usiwapangie wengine nyumba zao
ahaaaaaa yakushinde mwenyewe
 
Lazima kuwe na chombo cha ku regulate operation ya makanisa ya kilokole. Mimi naona watu wakishaingia huku especially wanawake wanatekwa ufahamu kabisa.

Mimi kuanzia leo nimempiga marufuku mke wangu kwenda kwenye kanisa lake kama anataka kuendelea kuishi na mimi arudi kanisa la lutheran ambako tumefungia ndoa yetu takatifu.

Yani mke wangu amekuwa mjinga kabisa na haya makanisa muda wote ni kukimbilia kanisani tu, atafunga bishara yake haraka haraka ahakikikishe anakimbilia kanisani. Leo hii mtoto anaumwa lakini anamwacha hata kumpa dawa kisa eti anakwenda kanisani. Kuna mtu wa maana sana anakuja home kwa ajili ya mkutano wa kibishara lakini mama anaona akimbilie kanisani. Yani nyumba chafu, kitanda hakitandikwi kisa kanisa.

Nasema haya makanisa yakome yanapoteza wake zetu.

Jumamosi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta mjini Arusha, umeshuhudiwa umati wa wanawake ! walijaza uwanja woote na wengine kubakia nje.
Somo lilikuwa jini mahaba !
Jamaa kapiga sadaka zaidi ya milioni 70 !
Daaah.......walokole nouuma !
 
Tatizo sio makanisa ya kilokole, tatizo ni mkeo... Mchunguze huenda kuna bwana kamzuzua ila mkeo anazuga kwa gia ya ulokole
 
Ki msingi haya makanisa ni mazuli tena yanafa cz wanamwabudu MUNGU wa kweli. Shida ni mkeo hajajielewa na haplay part yake kama mkeo mi nakushauli jalibu kwenda kusali hapo siku 1 lzma umwone MUNGU akikubdilisha mkuu

Yaani mungu ambadilishe aache kumkemea mkewe juu ya uchafu wa nyumba na kutoangalia mtoto ama?
 
Unapozungumzia makanisa ya kilokole unahitaji kuwa specific. Yapo makanisa ya kilokole ambayo ni institutionalized: FPCT, TAG, PAG, EAGT, yote hayo ni mifano ya makanis ya kilokole ambayo sio ya kuyaweka katika kapu moja na makanisa ya watu binafsi. Mke wako anaenda ulikole gani?
 
........duuh ! umetoka Mirembe boarding, sasa hivi wamekupangia Day !??
.......mbona tutakoma !
Hawa nao tuwaiteje?

chained-muslim-women.jpg
 
Jumamosi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta mjini Arusha, umeshuhudiwa umati wa wanawake ! walijaza uwanja woote na wengine kubakia nje.
Somo lilikuwa jini mahaba !
Jamaa kapiga sadaka zaidi ya milioni 70 !
Daaah.......walokole nouuma !
Kumbe ndivyo mnavyo wafanya wake zenu? Halafu mnawafunika na migauni myeusi. Hakika kuna njama ya chuki kwa kwenye dini yenu.

10151826_1408974669364037_919610535_n.jpg
 
Je Biblia Takatifu imekataza hayo yote?
 
Daah sasa mbona Kanisa hapo halihusiki na chochote?? Wewe kama unataka si umzuie mkeo asiende huko lakin sio Makanisa yafungwe kisa mkeo hatulii nyumban coz kama Makanisa ya kilokole yakifungwa je kwa waumini wengine itakuwaje? Bro think twice i hope wewe ni mtu makini lakin jaribu kuwa mtu mwenye privacy na mkeo, kama ni ushauri embu jaribu kutafuta watu wenye hekima wakupe mawazo kuliko kuleta uzi sehemu kama hii ambayo sometimes mtu unakuwa na shida serious lakin hupati majibu stahili
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom