Serikali Iondoe Makato ya Miti Kilimo cha Tumbaku

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MHE. EMMANUEL CHEREHANI - SERIKALI IONDOE MAKATO YA MITI KILIMO CHA TUMBAKU

Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Kahama-Shinyanga Mhe. Emmanuel Cherehani katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni ameuliza swali Wizara ya Kilimo na kujibiwa na Naibu Waziri Kilimo Mhe. Anthony Mavunde.

"Wakulima wa Tumbaku wamekuwa wakikatwa makato makubwa sana ya upandaji wa miche ya miti ambapo ni zaidi ya shilingi 813 kwa kila mche mmoja, kwanini Serikali isiondoe makato hayo kwa wakulima wa Tumbaku ili waweze kupanda miti kwa hiyari yao bila makato yoyote"? - Mhe. Cherehani

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imesema kuwa imepokea ushauri uliotolewa na Mbunge wa jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Peter Cherehani aliyeomba kuondolewa kwa makato makubwa kwa wakulima wa zao la Tumbaku yanayotokana na upandaji wa miche ya miti ambapo kwa bei ya sasa ni zaidi ya sh 813 kwa kila mche mmoja.

Akijibu swali hilo bungeni jijini Dodoma Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde amesema kuwa "Tumepokea ushauri wa Mhe. Mbunge na tutakaa kikao na wadau kuweza kukubaliana kwa pamoja, kwahiyo tumechukua ushauri"

#USHETUYETU
#TANZANIAYETU
#KAZIIENDELEE
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-04-19 at 19.56.45.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-19 at 19.56.45.jpeg
    24.5 KB · Views: 15
Makampuni ya tumbaku waweke utaratibu wa kupanda exotic trees kwa ajili ya kukaushia tumbaku. Utumiaji wa indigenous trees upigwe marufuku kuokoa misitu yetu.
 
Back
Top Bottom