Niko kwenye utafiti Binafsi juu ya Biashara ya Kilimo cha zao la Tumbaku.

IamKulwa

JF-Expert Member
Nov 25, 2023
236
550
Salaam wafanyabiashara wenzangu.

Wakuu mimi ni mfanyabiashara kwenye Kilimo (Agribusiness). Nataka kujiingiza kwenye biashara ya Zao la Tumbaku. Toka mwaka jana nimeona kuanza kushamiri kwa biashara ya zao hili. Mwaka huu nimeamua kutafiti mnyororo mzima wa thamani wa biashara hii ili nione wapi naweza patia fursa yake.

Nitaleta mrejesho hapa.
 
Tutashukuru kwa mrejesho wako... although miaka ya nyuma kwetu hili zao lili shamiri...kilichokuja ua hili zao ni kuwa watu walikuwa wanakopeshwa pesa za kulima tumbaku kwa vikundi...so ndani ya kikundi kuna baadh ya members walikuwa wakizingua hawalimi kulingana na hela waliopewa mwisho wa siku wakiuza,,,wale walio lima wanalipa madeni ya ambao hawakulima/kupata mazao vizuri ko ikawa ni zero effort.

So now watu washa achana na zao hilo kabisa saivi wanalima Mhogo tu kama zao la Biashara.
 
Back
Top Bottom