Nini mbadala wa Nishati ya kuni katika kilimo cha tumbaku?

Hamza Nsiha

JF-Expert Member
Jul 25, 2022
208
191
Habari ndugu wana JamiiForums, nimekuwa nikijiuliza maswali kadhaa kuhusiana na jitihada za sekta yetu ya Nishati katika kuibua njia mbalimbali ambazo zimekuwa na tija katika utunzaji wa mazingira kama vile Makaa ya mawe, Gesi asilia n.k. Njia hizi zimeleta mapinduzi katika kuinua Tanzania ya kijani kwa kupunguza matumizi ya nishati inayotokana na kuni au mkaa.

La! Hasha, kitu ninachojiuliza zaidi ni kuhusiana na ulimaji wa zao la tumbaku ambalo limeonekana ni zao lenye tija kwa wakulima wake kwani, Raisi wetu amejitahidi kuinua thamani ya zao hili kwa wakulima.

Changamoto ni kuwa ukifanya mahesabu ya haraka haraka ni kuwa ili kukamilisha zao hili hadi hatua ya kuuzwa ni dhahiri kuwa linategemea zaidi nishati ya kuni hivyo huambatana na ukataji wa miti kwa kiasi kikubwa.

Je! Sekta zetu hususani sekta ya Kilimo na sekta ya Nishati kwanini zisingetusaidia kutupatia nishati mbadala kupitia tafiti na majaribio ambayo hayataweza kuathiri ubora wa zao hili? Kwani ni kweli kuwa zao hili ni muhimu lakini pia miti ni muhimu.

Japokuwa, kuna kaulimbiu mbalimbali zinazotumika kama vile kata miti, panda mti lakini ni ukweli kuwa hazifanyi kazi kama ilivyodhaniwa.

Natamani kusikia Nishati Mbadala, tuimarishe Tanzania ya Kijani


 
Back
Top Bottom