Serikali inawabagua wanafunzi wa shule binafsi; ushahidi huu hapa

Umeandika upumbavu mtupu. Serikali iko sahihi 100% kufanya hivyo. Tena wamechelewa mno kuanza huo utaratibu. Kama ulisomesha mtoto private peleka mtoto private. Acha hao watoto wa St Kayumba waliofanya vizuri na wao wakasome shule bora zinazoitwa teule. Ila ninaisihi sana serikali kuendelea kupambana kuboresha shule za serikali. Anayesoma Kigogo Sec awe na mazingira mazuri kama wa Tanga tech au Ilboru sec.
 
Hesabu bila kufuata ufaulu? Kwa hizi hizi shule teule zinagwa nafasi za masomo kwa uwiano?
Hizo shule teule ni chache mpendwa! Ukisema utumie vigezo unavyovisema wewe maanake kwanza hazitatosha kwa hiyo uwiano ni mhimu ili kila upande upate! Kinachofanyika shule za private zina nafasi zao za kwenda huko hivyo hivyo na shule za umma zina idadi yao! Kutokana shule za private ni wengi wanafaulu ndo maan wanagawana wawili wawili mkuu! Shule za umma wanaofaulu kwa ufaulu wa juu ni wachache ndo maana wale wanaofaulu kwa kiwango hata cha B wanabahatika maana nafasi zao wengi hawafaulu kwaviwango vya juu!!


Sio kila kitu kuilaumu serikali mambo mengine tunapaswa kuipongeza
 
Sasa hapa umeandika utopolo gani? Hebu tuliza akili kwanza uje na hoja yenye mashiko. Kama unatetea huu ujinga kwanini wasitunge mitihani ya aina mbili:

1. Mitihani ya kubet kwa wanafunzi wa shule za kata.
2. Mitihani migumu kwa wanafunzi wa shule binafsi.

Kwanini wanafunzi wote watungiwe mitihani ya kubet halafu wengine wabaguliwe. Tumia akili mkuu.
 
Usidanganyike Darasa la 7 Hakunaga kufaulu ni Uchaguzi tu

Ukiwajua.Wajumbe wa Kamati ya Selection Ndio utanielewa
 
Weka hizo hesabu..!! huwezi taja hesabu halafu huiweki, inakuwa porojo tu..!!
 
Tuipongeze kwa ubaguzi huu? Kwanza wao wanatungiwa mitihani kwa lugha ya Kiswahili ambayo ni nyepesi ukilinganisha na wale wa shule za private wanaotungiwa mitihani kwa lugha ya Kingereza (lugha ngumu). Sasa iweje wabaguliwe kwa kuwekewa idadi sawa ya nafasi bila kufuata ufaulu? Huu ni upumbavu na ujinga wa kiwango cha lami unaofanywa na serikali ya mchongo ya CCM.
 
Hayo matokeo yanaonesha ufaulu wa jumla.

Huwezi jua ni wanafunzi gani waliofaulu kuliko wote mfano waliopata A masomo yote,

Hao ndo wanaenda shule teule.
 
Hivi umekielewa kilichoandikwa au umedandia tu..!!??

Nakutolea mfano, Philaldephia primary school ilipo Kongowe ya Mbagala ni PRIVATE, lakini wanafunzi wake karibu wote wenye wastani wa A, wamepelekwa Mwandege kutwa ya serikali..!!
 
Hayo matokeo yanaonesha ufaulu wa jumla.

Huwezi jua ni wanafunzi gani waliofaulu kuliko wote mfano waliopata A masomo yote,

Hao ndo wanaenda shule teule.
Mkuu acha uvivu....pitia hayo matokeo uone uovu wa serikali yako. Wanafunzi waliopata B wa shule za kata wameenda shule teule huku wanafunzi waliopata A wa shule binafsi wamepelekwa sjule ya kata Changanyikeni. Huu ni ujinga usiovumilika. Acha kutetea uhuni na upuuzi wa serikali ya CCM.
 
Hivi umekielewa kilichoandikwa au umedandia tu..!!??

Nakutolea mfano, Philaldephia primary school ilipo Kongowe ya Mbagala ni PRIVATE, lakini wanafunzi wake karibu wote wenye wastani wa A, wamepelekwa Mwandege kutwa ya serikali..!!
Mweleweshe aelewe na kama haelewei muwekee matokeo mkuu. Unajua watu wengine ni wagumu sana kuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…