Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
Kampuni tano zimeshaingia kwenye hatua ya manunuizi ili kushinda zabuni ya Ujenzi wa barabara ya njia nne zitakazokuwa za kulipia kutoka Kibaha hadi Morogroro ili kuondoa msomngamano uliopo.
Kamishna wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. David Kafulila amesema hii ni dhamira ya Serikali kutekeleza Ujenzi wa mfumo huo ili kuharakisha maendeleo.
"Kampuni kubwa tisa za kimataifa zilijitokesha, mchakato wa kwanza kwaajili ya kuzitathimini na kuamua ni kampuni zipi ziingie hatua za manununuzi na Kampuni tano zilibaki na ndizo zinaenda kuleta mapendekezo ya manna gani kila moja inafikiri inaweza kujenga Mradi huo.
“Ni mradi mkubwa sana ni Mradi wa Njia nne. Fikra ni kujenga Lami ambayo inaweza kuchukua miaka 30 mpaka 35 bila kufanyiwa marekebisho Makubwa. Kutoka kibaha mpaka Chalinze km 78.9 inaweka ikagharamu takribani dola 340 na kutoka chalinze Morogoro inaweza kugarimu Dola Milioni 500. Unaona kwamba ni zaidi ya Dola milioni 800 kujenga kiwango hicho cha barabara ya Lami.“ Amesema Bw. David Kafulila
Lengo la Serikali ni kuunganisha Dar na Dodoma kwa haraka zaidi. Kafulila amesema taratibu za kupata Mzabuni wa kujenga barabara kutoka Morogoro hadi Dodoma zinaendelea.
"Pesa ambazo Serikali ingezitumia kujenga barabara hizo sasa itazipeleka maeneo mengine. Ndio maana ya ubia, kwamba sekta binafsi inafanya jukumu ambalo Serikali ingefanya ili Serikali ibaki na majukumu ambayo sekta binafsi haiwezi kuingiza mtaji wake. lakini pia haiondoi jukumu la Serikali kuendeleza barabara zake kwani barabara za kulipia zinazoendeshwa na sekta binafsi zinaenda sambamba na barabara zinazosimamiwa na Serikali kuhakikisha Wananchi wanakua na chaguo la kutumia ama barabara ya kulipia au ile ya Serikali isio ya kulipia". Ameongeza David Kafulila