Serikali inaposhughulikia suala la wafanyabiashara Kariakoo ingetufikiria na sisi wafanyakazi, tunaonewa sana

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,647
1,885
Serikali inaposhughurikia swala la wafanyabiashara kariakoo ingetufikiria na sisi wafanyakazi: tunaonewa sana kwa kweli.

Mifano iko wazi:

1. Kwa mfano, daktari akilala zamu anapolipwa call allowance lazima akatwe VAT
2. Daktari au nesi akilipwa extra duty allowance lazima akatwe VAT
3. Mwalimu akisahihisha mitihani na akapewa hela ya kusahihisha mitihani lazima akatwe VAT

Kila kitu anachopewa mfanyakazi lazima alipe VAT.

Ndiyo maana wafanyakazi wengi ni maskini kwa sababu makato ya Serikali ni makubwa mno jameni.serikali itufikirie kwa kweli.

Mimi nalipwa milioni 4 kama mshahara, PAYe kila mwezi nakatwa milioni 1, sijajua mfanyabiashara yeye kwenye faida ya 4 million anakatwa kiasi gani. Halafu hakuna mfanyabiashara ambaye ni mwaminifu hata 95% kuonyesha mapato yake halisi.

Niombe Serikali tukufu ya mama yetu Samia ifute VAT kwa watumishi wa umma na sekta binafsi Ili wafanyakazi waweze kujitoa kwenye dimbwi la umaskini.
 
Kwenye hyo milion 3 inayobaki uwe unanikatia na mm sh 30 kila mwezi mkuu kazi yangu iwe kuja kufanya usaf wa garden hapo nymbn kwako
 
Wafanyakazi hamuwezi kuitikisa serikali kama walivyofanya wafanyabiashara. Kwasbb ni waoga, hamna umoja na mmejaa unafiki.

Mnatumika vibaya na serikali kupora haki za wapiga kura wakati wa uchaguzi mkuu . Na ninyi ndiyo mnatunga kanuni kandamizi za biashara.

Siwapendi wafanyakazi,
 
Serikali inaposhughurikia swala la wafanyabiashara kariakoo ingetufikiria na sisi wafanyakazi: tunaonewa sana kwa kweli.

Mifano iko wazi:

1. Kwa mfano, daktari akilala zamu anapolipwa call allowance lazima akatwe VAT
2. Daktari au nesi akilipwa extra duty allowance lazima akatwe VAT
3. Mwalimu akisahihisha mitihani na akapewa hela ya kusahihisha mitihani lazima akatwe VAT

Kila kitu anachopewa mfanyakazi lazima alipe VAT.

Ndiyo maana wafanyakazi wengi ni maskini kwa sababu makato ya Serikali ni makubwa mno jameni.serikali itufikirie kwa kweli.

Mimi nalipwa milioni 4 kama mshahara, PAYe kila mwezi nakatwa milioni 1, sijajua mfanyabiashara yeye kwenye faida ya 4 million anakatwa kiasi gani. Halafu hakuna mfanyabiashara ambaye ni mwaminifu hata 95% kuonyesha mapato yake halisi.

Niombe Serikali tukufu ya mama yetu Samia ifute VAT kwa watumishi wa umma na sekta binafsi Ili wafanyakazi waweze kujitoa kwenye dimbwi la umaskini.
Katiba Mpya! Katiba Mpya!

Pole sana, lakini wengi wenu hamjui - sio kila sheria ni halali au ya haki. Nyingine ni sheria haramu na dhulumat. Kuna sheria hazina/hazitoi haki 100%. Ndio maana nyingine Mahakama huzifuta au kuamuru zibadilishwe.

Ndio maana tunataka Katiba Mpya, ili baadaye tutunge sheria nzuri, kali na za haki.
Mwenye haki apate haki na mhalifu aadhibiwe; tofauti na ilivyo sasa.
 
Back
Top Bottom