Serikali inaendelea kufanya ubaguzi kwenye ajira. Kama una div 1&2 au bachelor degree jua upo kwenye risk ya kutoajiriwa

Tangu ile moment wakati tupo chuo nilipoona wanaCCM ambao hawana mkopo wanaambiwa waandike majina ishu zao za mikopo zishughulikiwe na ukweli walikuwa wanashughulikiwa, sijawahi kuwa na na hawa so called serikali. Ubaguzi hautakaa uishe....
 
Ukweli mtupu asilimia kubwa ya watu tuliosoma kwa bidii ndo tuna hustle sana kwenye sekta ya kutafuta ajira, failure wote wanamaisha mazuri, ila tuliokuwa tunafuhuru tu ajira zinatupiga chenga, Mana saiz ajira zinaishia veta na diploma, Kwenda form six ni kupoteza mda , hakuna professional yoyote unayopata ndani ya hiyo miaka miwili.
 
Nimesema suala hili kwa muda mrefu.mimi napendekeza kustaafu iwe hata 45yrs.tatizo litakwisha.Au iwe ajira za mkataba wa miaka 10-15tu.
 
Umeongea vizuri kiongozi.Mimi huwa nashangaa matangazo ya kazi wanahitaji watu wenye cheti cha atec 1 ya nbaa wakati kimsingi nbaa hawatoagi cheti cha atec 1.!!nbaa wanatoa cheti kwa atec 2 na CPA tu.Sasa jiulize ina maana watu wa serikali hawajuhi kuwa nbaa hawatoi cheti cha atec 1???
 
Iko hivi,polisi wanawataka waliofeli maana hawawezi kuhoji chochote. Akiambiwa piga,anapiga. Lipua,analipua. Ajiri mtu mwenye masters yake sasa,lazima ahoji. After all,msomi siku zote Ana exposure yakutosha. Ndio maana ukiangalia vikosi vvyetu,utagundua Kuna tatizo kubwa Sana.
 
waziri simbachawene amesema wana ajiri wenye division zero ili wakashike silaha na kulinda benki kwahiyo ww na One yako kaa kwa kutulia hizi ajira ni special kwa failures tu
 
Nilikomaa kusoma hadi varsity huko nitatoka na GPA 3.8 but job niliyopata ni ya kisenge.Niliomba chance huko jeshini (JW,Magereza hadi Polisi) hata nafasi ya kuitwa kwenye interview sikuipata.

Rafiki yangu tuliyekuwa naye Form 6 na akaishia hapo,yeye alichukuliwa JW huku mimi nikiachwa.Sasa jamaa ni Luteni na anakula maisha ile mbaya kiasi kwamba ananitimulia vumbi kwa mbali mno.

Sisi wenye nyota za kunguni tumeshakoma!
 
Hadi 45
 
Taratibu zakazi huwa haziangalii daraja ya masomo ya juu huwa unatangaza kuanzia hapa.
Kama kazi inahitaji kijana waelimu ya chini hutangazi.
Unaweza kusema sifa ni mtu kuwa na certificate ya Form IV
watakao kuja unafanya usaili>
Wewe una degree jee huoni kazii itakuwa umeover qualified na mshahara utakao pata utaku wachini sana?
Kwanini uka apply hii kazi na msuali mengine lakini hutangazi kuwa nataka watu daraja gani tuu.
 
Nina division four yangu safi ya form four, sasa hivi nipo ofisi nyeti ya serikali napiga kazi😏
 
Hivi kama unamchukuwa kijana wa dv4 una mpa kaz anaifanya vizuri alafu una mchukia wa dv1 anafanya kama darasa la Saba wewe unge muajiri nani? Elimu imeimgiliwa mm naona sawa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…