Serikali imewezesha kushuka kwa bei ya mafuta

MoureenAbel

Member
Sep 24, 2021
29
43
Kupanda kwa bei ya mafuta kuna athiri kwa ujumla maisha ya wananchi, kwa sababu kunapelekea kupanda kwa gharama za vitu vingine. Lakini licha ya kuwa inaonekana bei ya amefuta imepanda, kwa namna nyingine unaweza kusema bei imeshuka.

Imeshuka kwa sababu serikali imeondoa ada ya mafuta ya TZS 100 kwenye kila lita moja ya petroli na dizeli. Hii ina maana kwamba, katika eneo ulilopo, kama bei ukomo ya juu ya petroli ni 2510, kama serikali isingetoa ada hiyo ingekuwa 2610. Kama dizeli ni 2332, kama ada isingetolewa ingekuwa 2432.

Kwa hiyo sawa, tunakubali bei imepanda, lakini walau serikali imeonesha jitihada ya kupunguza makali kwa sababu soko la dunia ndilo linaamua bei ya mafuta.

 
Bei ipi ya mafuta iliyoshuka?Kama mwezi uliopita mafuta yalikuwa chini na mwezi huu yamepanda hakuna namna mtadanganya mafuta yameshuka.

Hizi kelele za mama anafanya kazi hazisaidii kitu,Chanzo cha mafuta kupanda ni Serikali ya CCM yenyewe hamwezi kujitetea
 
Yani mnaleta uongo wa kitoto kwamba bei ilikuwa 2610 😅😅😅 ila mmeondoa shilling 100? Kwa kupunguza gharama bei ilitakiwa iwe 2310 kwa sasa.

Acheni uhuni hii aina tofauti na mfanyabishara akiongezewa kodi kuijumlishia kwenye bei ya bidhaa ili mlaji ailipe😅! Wakiongezewa kodi mfano TzS 50 tu kwenye uzalishaji kama bidhaa ilikuwa sh450 basi itauzwa tzs 500 hio hela hawalipi wao!
 
Back
Top Bottom