Serikali ya Rais Samia kuajiri wa hudumu wa Afya Ngazi ya jamii zaidi ya 137,000

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,100
49,795
Serikali imesema itafundisha na Kuajiri wahudumu ngazi ya jamii Zaidi ya 137,000 ndani ya miaka 5 ijayo kuanzia mwaka ujao wa 2024/25 sawa na Watumishi zaidi ya 27,000 Kila mwaka.

Lengo la Serikali ni kuhakikisha Kada hii inatambulika na kuhakikisha Kila Kijiji kinafikiwa na Huduma Bora za Afya.

My Take
Vijana msipopata kazi awamu hii ya mama basi mjue ndio imewakata.

Slogan nj Ile Ile, Samia maneno machache vitendo vingi.Matendo yanaongea Kwa Sauti kubwa kuliko mdomo.Kazi iendelee.

=======

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imepanga kufundisha na kuajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii 137,294 ndani ya miaka mitano, Ili kuhakisha kila mwanachi anafikiwa na huduma za afya nchini.

Hayo yamesemwa Novemba 22, 2023 na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitwaa (OR-TAMISEMI) anayeshughulikia Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe Dkt.Wilson Mahera wakati wa kikao kazi cha kupitia mtaala utakaotumika kufundishia wahudumu hao leo jijini Dodoma.

Dkt Mahera amesema kuwa lengo la serikali ni kuboresha huduma za afya nchini ili ziendane na uwekezaji mkubwa wa ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya unaoendelea kwa kasi nchini.

‘’ Leo tumekusanyika hapa ili kupitia huu mtaala utakaotumika kuwafundishia wahudumu wetu,tunatarajia kuanza na wahudumu 28,000 mwaka 2024 na tutaendelea kadri tutakavyopata fedha.Tunategemea kuwa na wahudumu wawili katika kila kitongoji kwa upande wa vijijini na mtaa kwa upande wa mijini na kila mhudumu atahudumia nyumba zisipungua 70”.

Dkt. Mahera ameongeza kuwa wahudumu hao watapewa mafunzo kwa muda wa miezi sita na kisha kuajiriwa rasmi na serikali.

“Wahudumu hawa baada ya kupata mafunzo ambayo yatakuwa ya nadharia na vitendo wataingizwa kwenye mfumo rasmi wa serikali na wataboreshewa maslahi yao ili waweze kufanya kazi kwa bidii.Wahudumu hawa watasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na upungufu wa wahudumu katika sekta ya afya nchini ili tufikie lile lengo la huduma ya afya kwa wote” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kinga kutoka wizara ya afya Dkt.Ntuli Kapologwe, amesema kuwa wahudumu hao watajikita kwenye afua zaidi ya nane watakaosaidia kutambua magonjwa mapema ili wananchi wapate matibabu mapema.

“Pamoja na huduma za kitabibu,wahudumu hawa watatumika kutoa huduma za chanjo ,masuala ya lishe,ustawi wa jamii , kukabiliana na majanga kwenye ngazi ya jamii na kutoa elimu ya afya kwa umma.Mpango huu utaleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini na utakuwa wa mfano katika nchi zetu za Afrika.”

Chanel ten
 
Upuuzi mwingine wa ccm, tunajivunia serikali kuajiri!

Wenzetu akili kubwa wanajivunia kutengeneza ajira viwandani, serikali kuwa mtoa ajira sio jambo la kujivunia, sasa chukulia serikali iajiri wanajeshi, polisi, maofisa utamaduni, wakirugenzi nk, wote hawa wanatoa bidhaa gani ya kuingiza pesa ya kigeni, None! Hawa, wote ni walipwa mishahara tu, kazi yao kutoa huduma hapa hapa nchi ni kwa mwananchi! Na je kama mwananchi mwenyewe ni choka mbaya, hizo huduma atalipia vipi?
Yanaanza kuja Mambo ya kipuuzi, ruzuku, na tasaf.

Tumeambiwa juzi na kikwete, Mfanyabishara hanspope alihamisha kampuni yake kwenda South Afrika, kukwepa uozo wa hapa Bongo. Kwanini serikali haiwapi au kuweka vivutio kwa kampuni kama General Motors, Toyota, Tesla, samsung, zifungue viwanda hapa nchini?

Badala yake wapo tayari kutoa mbuga zetu kwa mabwanyenye ya kiarab, ambayo hayafanyi chochote zaidi ya kujenga misikiti na kuendeleza uislam(Ghadafi na u tajiri wake wote, kitu pekee alichoipa TZ, ni misikiti pale Dodoma!) Unajiuliza kama angetujengea chuo cha IT, au kiwanda cha magari na vipuri, tungekuwa wapi!

Ukienda South Afrika, ma kampuni makubwa yote yana branches pale. Sisi na uchawa wetu tunajivunia hivi viajira uchwala na misifa kibao kwa Samia!
 
🗑️🗑️🗑️
 
Habari kama hizi ni nzuri sana hasa kwa watu wenye akili ndogo!

Kuajiri watu Serikalini kunaendana na ukuaji wa uchumi. Tumeanza kuona ukamilishaji tu wa miradi kama SGR umeanza kukwama (Rejea taarifa ya Yapi Merkez kupunguza wafanyakazi kutokana na ukata).

Sasa mazombie hayana hata uwezo wa ku-analyze huo uwezo wa Serikali kuajiri watumishi laki moja na elfu thelathini na Saba (137,000) unatoka wapi?!

Kutawala wapumbavu ni rahisi sana!
 
Ni huduma gani bora za afya zitatolewa na hao Community Health Workers, tuanzie hapo kwanza.
 
Inamaana wataenda kupewa semina upya hawa community health au watafundishwa upya
 
wataenda kupewa mafunzo ya miezi sita ambapo mitatu itakuwa theory na mitatu practical... Vile vile wataingizwa kwenye mfumo wa utumishi wa umma kama wafanyakazi wa sekta ya afya....
 
Back
Top Bottom