Serikali imdhibiti Maulid Kitenge na kundi lake la wahuni wanaojiita Wasafi Jogging Group

Acha yawakutebkama wale wa Mwanza walivyogongwa na gari,kama lengo ni mazoezi kwa nini easitafute kiwanza wawe Wana kimbia kwa kuuzinguka uwanja hata mala 200.
 
Mwaka 1994 nchi ya Tanzania ilimpoteza mwanariadha mahiri hayati Simon Robert Naali kwa ajali ya gari wakati akifanya mazoezi barabarani huko Arusha. Hizi jogging za kwenye lami ni hatari sana kiusalama na kiafya. Mazoezi ya kwenye lami husababisha injuries za miguu ambazo huchukua muda kupona. Wanariadha professional huwa wanakimbia kwenye lami kimkakati sana ila karibu 90% hufanyia mazoezi kwenye rough roads na uwanjani.
 
Kuna siku bodaboda alilazimisha kukatiza wanapopita, wakampiga bao la mgongoni. Alisimama akaangalia kwa uchungu halafu akatikisa kichwa akaendelea na safari.
Aliwadharau sana.
Aisee, nahsi ni boda boda mwenye akili nyingi hakutaka kupambana na kundi la wajinga wengi.
Nasikia Kitenge anazunguka sana duniani, je ni nchi gani kakuta kundi kubwa la watu linakimbia mabarabarani?
 
Huyu jamaa Kwa kutambua kwamba nchi Sasa Ina mbululaz wengi wanaojipendekeza Kwa watu maarufu huku wakijiita machawa akaanzisha kundi la kukimbia mchakamchaka barabarani.

Mazoezi ni muhimu Kwa afya ya mwili na akili, lakini yasifanywe kihuni, yafanywe mahali sahihi na salama Kwa wafanya mazoezi wengine na jamii Kwa ujumla.

Kitenge na wahuni wenzake wamekuwa kero Kwa wakazi wa maeneo ya Oyster Bay na Masaki na watumiaji wengine wa Barbara wa maeneo hayo.

Kitenge na wahuni wenzake wamekuwa wakikimbia katikati ya barabara huku wakisababisha usumbufu Kwa watumiaji wengine wa barabara, hususani watumiaji wa vyombo vya moto, Kwa kuwazuia kutumia barabara kikamilifu.

Kitenge na wahuni wenzake wamekuwa wakitumia barabara kukimbia, barabara zinajengwa Kwa gharama kubwa ili zipitishe magari Kwa haraka.

Kitenge ni kero, huyu atakuja kusababaisha majanga Kwa hao wahuni wake, amini nawaamnia Kuna siku mtasikia hao mbuzi wa Kitenge wanaokimbia mabarabarani kama wehu wamegongwa na gari na wamekufa na wengine kujeruhika.

Kwa kuepusha haya yasitokee, Kitenge adhibitiwe haraka.
Shida yetu wabongo ndio hii.. Tushamiliki KA-IST tuu tayar tunaona barabara zote za lami, changarawe na vumbi ni kwa ajili yetu tuu. Watembea kwa miguu wapite misituni wakiwa wanaenda makwao.


#Nina shida na pesa.
 
Back
Top Bottom