Ngorongoro hali mbaya: Maulid Kitenge ataka hatua za dharura zichukuliwe kuwanusuru Wamasai

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
877
955


Kituo cha Wanahabari watetezi wa Rasilimali na taarifa (MECIRA) kimeitaka serikali kuchukua hatua madhubuti za haraka na dharura ili kunusuru maisha ya wananchi jamii ya kimasai wanaoishi katika tarafa ya Ngorongoro iliyopo ndani ya hifadhi ya Ngorongoro sambamba na kunusuru mazingira na uhifadhi wa eneo hilo unaoonekana kuathiriwa kutokana na muingiliano wa shughuli za kibinaadamu ikiwemo ufugaji uliopitiliza.

Makamu mwenyekiti wa kituo hicho mwanahabari mkongwe Maulid Kitenge ameyasema hayo kwa niaba MECIRA muda mfupi baada ya kamati tendaji ya taasisi hiyo kutembelea hifadhi hiyo kujionea utalii na maisha ya wananchi husika kuzingatia ukweli kuwa hifadhi ya Ngorongoro ndio hifadhi pekee nchini inayohusisha maisha ya binaadamu, mifugo na wanyama

Miongoni mwa mambo yaliyomsikitisha Kitenge ni jinsi wakazi wa maeneo hayo wanavyoishi kwa kukosa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo maji, barabara, Hospital n.k

Kitenge ameishauri Serikali kuwatafutia mahali salama pakuishi kwakazi waliopo hifadhini ili wapate huduma umuhimu za kijamii na waweze kuendelea kama binadamu wengine.

Nae Mjumbe MECIRA Oscar Oscar ameshangazwa baada ya kutembea umbali zaidi ya Km 45 lakini hajaona Wanyama zaidi ya pundamila kuchanganyika na mbuzi, ng’ombe kitendo ambacho kinahatarisha afya za wanyapori na usalama wao,

Pia ameogopeshwa na kasi ya ongezeko la wanyama wa kufugwa ng’ombr mbuzi kitu kinachosababisha Wanyamapori kukimbia, na kugombania malisho
 
Wao wanasema wamefika, na wanapigana wasiondoke,hata sie watanzania wenzako tuko nao bega KWa bega ,Kitenge anawashwawashwa nini?masai tribe SIO watu wa anasa hata walioko mjini huwezi jua wanalalaga wapi,na ndo maana kabila hili limebaki kuwa la kipekee

Waachwe nao ni watanzania, tunazo hifadhi ngapi tz? Lakini pia mbona wemeshiriki kutunza wanyama

Ngorongoro iwe aridhi ya wanasai period, na mbunga wakabidhiwe moja KWa moja
 
Binaadamu wana hali mbaya sana kuliko wanyama....wanaotakiwa Kuokolewa sasa ni wamasai si wanyama

Jenga Hoja
Hivi lini mmesikia wamasi wanasema Wana Hali mbaya, Kama kweli Wana Hali mbaya why hawataki kuondoka,

Ni mafisadi yanayotaka jimilikisha mbuga Ili kufanya ujangili, ndo wanakuja na propaganda mfu pitia KWa wamasai ,Ili wakatekeleze ushetan wao
 
Kupanga ni kuchagua kwa kipato utaliii na uhifadhi endelevu hakuna mjadala. Ina bidi Wananchi na mifugo wapishe wapishe kwa resettlement plan ya haki, wapewe eneo la pembezoni lenye ecolojia similar lenye mipaka.

Wakati wa vijiji 1974 Mwl. Nyerere aliwapeleka baadhi wakazi Kilimanjaro Tanga na Morogoro kuwagawia mashamba. Maamuzi sahihi yafanyike haraka.
 
Back
Top Bottom