Serikali ikajifunze toka St. Francis Sekondari Mbeya kuboresha ufaulu wa kidato cha nne

Mimi ndani ya st Francis hakuna maajabu zaidi in kuwa wanchukua wanafunzi cream kwenye mchujo wao that period sasa kama wanaenda kwenye interview watoto 5000 alafu wao wanahitaji 100 huoni kwamba watachukua wanafunzi bora tupu. Ambao ukiwachukua ukawapeleka hata shule yenye mazingira ya wastani wataperform

Kama st Francis in bora na wao wawe wanapelekewa wanafunzi kwenye mgawanyo wa serkali then wawabadilishe na kufaulu
Huu ukweli wanausema wachache sana.Ishi milele mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna jipya lolote la kujifunza pale, hizo shule zinabebwa na kuchukua cream tu. Advance watoto wengi huenda shule wanazopangiwa za serikali na shule za serikali hufanya vyema. Mfano mwaka Jana shule iloongoza ni kisimiri. Kwa hiyo na shule za private waende wapate semina pale? Haya mambo yapo wazi hayahitaji semina wala Nini. Maana hata walimu wakienda semina ila bado serikali ina mambo mengi ya kufanya.tatizo watu wengi mmekazania sana walimu bila kujua Kuna factors nyingine kubwa zaidi

Napendekeza
1. Shule za serikali zichuje kwa wastani Kama binafsi
2. Shule za serikali zitengewe hela ya kutosha ili kuwapa mitihani ya Mara kwa Mara watoto
3. Shule zote zifanywe za bweni ili watoto wapate muda mwingi wa kujisomea
4. Serikali iboreshe maslahi kwa walimu wake
5. Serikali itenge hela ya kutengeneza library na kununua vitabu vya kutosha

Alafu baada ya hapo ndo tuje tuwalaumu walimu. Mazingira ya kujifunzia mabaya mnakazania walimu. Natamani ck moja tuchange hela ya kutosha tuwatoe walimu wa St Francis tuwape shule moja ya kata. Shule haina maktaba, watoto wanatoka mbali, wengine wanakuja form one hawajui kusoma af watoe hizo one zao sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu watakaofeli huo mchujo waende wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na hilo umesahahu kwamba hiyo shule inachukua wanafunzi vipanga tuu.. unataka hawa vilaza wasome wapi?

Kuna wanafunzi hata ukeshe unafundisha wanapata zero kama kawaida.

Cha msingi serikali
1. Iboreshe mazingira ya shule
2. Vitendea kazi
3. Walimu wawe wa kutosha.
4. Umeme

Asilimia 100 ya wanafunzi wa ST Francis Girls Mbeya wamepata daraja la kwanza kwenye mtihani wa kidato cha nne matokeo yaliyotangazwa Leo tarehe 09/01/2019

Wanafunzi walikuwa 91 na wote wamepata division one

Shule imeongoza kitaifa masomo saba ikiwemo chemistry na Biology

Asilimia 92 yaani 92%wamepata division one ya point 07 mpaka 10

Asilimia zaidi ya 62 yaani 62% wamepata division one ya point 7

Kwa ufupi division one point saba au single digit ya 7 ndio idadi kubwa ya wanafunzi wamepata daraja hilo

Zaidi ya wanafunzi 62 wamepata division one ya point saba kati ya wanafunzi wote 91

Hii shule ina miaka zaidi ya ishirini ikifanya vizuri zaidi, kwanini serikali haiendi kujifunza huko Mbeya kwenye shule ya kanisa Catholic

Serikali inakwama wapi? Mbeya sio mbali ni kumtuma Ndalichako Waziri akajifunze mazingira na aina ya walimu hapo

Zaidi ya miaka ishirini shule inakimbiza mchakamchaka

Nilipoangalia shule za kata huko Dsm na Ruvuma niliamua kufunga website

Nilipoangalia shule za wilaya na mikoa zile kubwa kubwa zimejaa division Four na zero

Serikali inakwama wapi kwenda St Francis Mbeya kujifunza nauli kwa basi ni elfu 40,000 tu Fedha za kitanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasiwe na MCHUJO tuone ubora wa hayo mazingira.Angalau wachukue wanaojua kusoma na kuandika kisha wawatengeneze kwa kutumia ubora wa hayo mazingira wapate Div.1 darasa zima.Changa la macho...!

Sent using Jamii Forums mobile app
We nae em tumia akili..shule za private ziko kwaajili ya kibiashara pia, mchujo kuwepo kwenye shule zao ni sehemu ya mkakati wa biashara yao ya kutoa elimu kwa umma, hakuna anayefanya biashara hlf hana mkakati wa kupata faida!

Huu uozo wa kata hauleti pato serikalin hivyo wana carefree kwenye ishu za elimu, swala la msingi kwenye kata ni takwimu za wanaojiandikisha shule ziongezeke ili zipatikane hoja za kusimamia wakati wa uchaguzi!
 
Kwa mantiki hiyo ya mchujo hapo mchango wa shule na mazingira yake ni kiduchu sana.
Mkuu mbona kidato cha sita shule za serikali hufanya vzr. Mfano mwaka Jana kisimiri waliongoza. Kumi Bora walikuwepo kibaha na tabora boys. Ni hyo ni Kwasababu form six wanaofika ni Kama tayar wamechujwa maana bila div one, two au three hupangiwi shule. Lakin kingine shule hiz za advance ni za bweni watoto hupata muda wa kujisomea kuliko nyingi za kata ambazo ni kata.

Mkuu shule za kata Kuna watoto wanaenda form one hawajui kbs kusoma mwalimu awafanyaje Sasa? Kule St Francis sio mchezo wanachuja balaa, peleka mtoto wako uone. Kuna watoto wanachujwa hizo shule na wanahamia kwingine wanapiga one. Pale hawafundishi mandezi uliza wenye watoto kule. Kila mwaka mchujo na wastani upo juu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasiwe na MCHUJO tuone ubora wa hayo mazingira.Angalau wachukue wanaojua kusoma na kuandika kisha wawatengeneze kwa kutumia ubora wa hayo mazingira wapate Div.1 darasa zima.Changa la macho...!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa wasiwe na mchujo kivipi wakati wao ni wafanyabiashara?

Yaani waanze sera za kuwaonea huruma watoto ambao shule kwao kama bangi na serikali ili iwe zoa zoa kama shule za kata?

Kama nilivyosema hapo juu kuwa matokeo ya hii shule ya mambo mengi na mambo yote yapo kimkakati
1. Wanafanya mchujo mzuri na kuwapata wanafunzi walio bora
2. Wana walimu wazuri walio na moyo na kazi na wameipenda kazi yao
3. Wanajali maslahi ya waalimu wao
4. Watoto wanawekewa mazingira mazuri ya kujisomea na ikiwemo kuwekewa vifaa vya kufundishia
5. Ufuatiliaji wa wazazi ni mzuri
6. Wana mitihani karibu kila mwezi ili kujua mwenendo wa kila mwanafunzi na maendeleo kiujumla kitaaluma

Yaani hao watu wana deserve na sio kwamba nasimuliwa ila naongea kwa ushahidi naifahamu hiyo shule vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We nae em tumia akili..shule za private ziko kwaajili ya kibiashara pia, mchujo kuwepo kwenye shule zao ni sehemu ya mkakati wa biashara yao ya kutoa elimu kwa umma, hakuna anayefanya biashara hlf hana mkakati wa kupata faida!

Huu uozo wa kata hauleti pato serikalin hivyo wana carefree kwenye ishu za elimu, swala la msingi kwenye kata ni takwimu za wanaojiandikisha shule ziongezeke ili zipatikane hoja za kusimamia wakati wa uchaguzi!
Kama ni hivyo basi upuuzi kulinganisha matokea ya pande hizi mbili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu watakaofeli huo mchujo waende wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa hapo ndo tunapo kosea mkuu, elimu ni haki ya kila mtu ila mtu akifeli tusimlazimishe.. shule za serikali zina dhalilika sana mara nyingi tu wakaguzi wanaleta ripoti kuwa wanafunzi wa kidato cha pili asilimia kadhaa hawajui kusoma na kuandika kwa ajili ya hizi huruma za kusema ataenda wap ataenda wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asilimia 100 ya wanafunzi wa ST Francis Girls Mbeya wamepata daraja la kwanza kwenye mtihani wa kidato cha nne matokeo yaliyotangazwa Leo tarehe 09/01/2019

Wanafunzi walikuwa 91 na wote wamepata division one

Shule imeongoza kitaifa masomo saba ikiwemo chemistry na Biology

Asilimia 92 yaani 92%wamepata division one ya point 07 mpaka 10

Asilimia zaidi ya 62 yaani 62% wamepata division one ya point 7

Kwa ufupi division one point saba au single digit ya 7 ndio idadi kubwa ya wanafunzi wamepata daraja hilo

Zaidi ya wanafunzi 62 wamepata division one ya point saba kati ya wanafunzi wote 91

Hii shule ina miaka zaidi ya ishirini ikifanya vizuri zaidi, kwanini serikali haiendi kujifunza huko Mbeya kwenye shule ya kanisa Catholic

Serikali inakwama wapi? Mbeya sio mbali ni kumtuma Ndalichako Waziri akajifunze mazingira na aina ya walimu hapo

Zaidi ya miaka ishirini shule inakimbiza mchakamchaka

Nilipoangalia shule za kata huko Dsm na Ruvuma niliamua kufunga website

Nilipoangalia shule za wilaya na mikoa zile kubwa kubwa zimejaa division Four na zero

Serikali inakwama wapi kwenda St Francis Mbeya kujifunza nauli kwa basi ni elfu 40,000 tu Fedha za kitanzania
St Francis inachukua wanafunzi ambao wako bright darasa la saba na wanafanya mitihani ya pre form 1/test na wanaopata alama za juu ndio wanaochukuliwa,
Mazingira ya Ile Shule yalivyotulivu huwezi ukalinganisha na shule nyingi za serikali haswa zilizo Mijini/kwenye Majiji,
Walimu walivyo serious kutokana taratibu za kanisa huwezi ukawalinganisha na wa serikali,
Miaka ya zamani wakati tunasoma olevel ndo hiyo shule ilianza na ilikuwa inashinda na shule za serikali kama Mzumbe, Ilboru, Kibaha,
Shule za Serikali hazifanyi vizuri miaka hii kutokana na serikali yenyewe kuweka siasa katika elimu, huwezi ukawa unamtishia mwalimu ilihali hata mshahara unaomlipa ni kiduchu, unabananisha wanafunzi ndani ya chumba kimoja, Mimi nakumbuka wakati tunasoma Olevel Darasa lilikuwa na mikondo 3, na kila mkondo ulikuwa na wanafunzi tusiozidi 30-35 na hiyo ulikuwa shule maalumu yaani zile ambazo zinachukua wanafunzi waliofaulu sana.
Nilichojifunza kwa wale walimu waliotufundisha miaka ile nikuwa ikifika Form 4 term ya II walikuwa wanafunzisha namna ya kujibu maswali katika mitihani ya Taiga NECTA, kwahiyo ilikuwa inatupatia confidence,
Nenda kaangalie Leo namna wanafunzi wa shule za serikali wanavyofundishwa, matatizo ya shule, walimu molal hakuna.
 
Binafsi siamini kama kunauwezekano wa kupata div 1 wote...tena one za saba....big no!!!kuna namna inayofanyika ili kunyanyua matokeo...chukulia mfano huu hai...udsm coet telecom huwa wanachukua one tu tena za point 3 mwisho point 4...lakini bado wakifanya mtihani wa chuo katika mazingira HURU bado matokeo yanakuwa na gredi zote yaani kuanzia pass mpaka first class...tukirudi st Francis kuna maslahi makubwa sana ya watoto wa vigogo maana wengi wanasoma pale hivyo iwezekano wa kuchakachua paper ni mkubwa..

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijui ni kwanini watu hupenda vitu vifanane na wanavyowaza au walivyozoea. Tofauti na hapo haiwezekani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lazima na Muhimu tuwawekee mbadala wale wenye vichwa "nunda" kama mimi in case wameonekana kufeli sio bora liende
Sasa hapo ndo tunapo kosea mkuu, elimu ni haki ya kila mtu ila mtu akifeli tusimlazimishe.. shule za serikali zina dhalilika sana mara nyingi tu wakaguzi wanaleta ripoti kuwa wanafunzi wa kidato cha pili asilimia kadhaa hawajui kusoma na kuandika kwa ajili ya hizi huruma za kusema ataenda wap ataenda wapi

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo mambo ya kulisaidia taifa yaliisha na azimio la Arusha, Kwa sasa mzazi anawekeza katika elimu ya mwanae ili aweze kulinda future yake na hilo la kulisaidia taifa huja kama impact tu.
Kingine huwezi jua impact yao kama huna data za kujua wao wapo wapi na wanafanya nini hivyo ni kheri upunguze kuwa negative. It will save your soul
Kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom