Unalizungumziaje suala hili katika uchaguzi wa wanafunzi Kidato cha Tano?

crankshaft

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,410
3,376
Nilikuwa napitia majina ya wanafunzi waliochaguliwa katika shule bora za serikali nchini. Kwa asilimia zaidi ya 90 wamejaza watoto wanaotoka shule za binafsi /private. Na kama unavyojua hizi shule hufaulisha sana. Unakuta shule moja watoto wote wamepata one kali.

hii inamzibia mtoto wa shule ya kata. Yaani pamoja na kupambana na changamoto zilizopo katika shule hizo halafu akapata one ya single digit hawezi kupata nafasi hiyo.

kwa nini serikali isiangalie namna ya kumsaidia huyu mtoto ikampa favor katika uchaguzi ? Unakuta shule nzima one za single digit zipo tano lakini wote wanatupwa shule za kawaida. Unalionaje hili jambo?
 
Hii dunia kwenye maisha ni Survival of the fittest. Walio juu kiuchumi watapata vinono vingi, wa chini inabidi wapambane mara mbili ya hao wa juu ili angalau wapate nusu ya mabaki ya vinono kutoka kwa hao wa juu.

Wapo wanafunzi private ambao hawataenda hizo shule za serikali na hizo nafasi zitabaki kwa hao wa kata.

images (2).png
 
Nilikuwa napitia majina ya wanafunzi waliochaguliwa katika shule bora za serikali nchini. Kwa asilimia zaidi ya 90 wamejaza watoto wanaotoka shule za binafsi /private. Na kama unavyojua hizi shule hufaulisha sana. Unakuta shule moja watoto wote wamepata one kali.

hii inamzibia mtoto wa shule ya kata. Yaani pamoja na kupambana na changamoto zilizopo katika shule hizo halafu akapata one ya single digit hawezi kupata nafasi hiyo.

kwa nini serikali isiangalie namna ya kumsaidia huyu mtoto ikampa favor katika uchaguzi ? Unakuta shule nzima one za single digit zipo tano lakini wote wanatupwa shule za kawaida. Unalionaje hili jambo?
Nikiri, mimi ni mmoja wa Wanafunzi waliowahi kusoma hizo shule Maalum (special school).

Kwa level ya Kidato cha 5 na 6, hakuna umaalum. Walimu ni wale wale wa shule za kawaida. Hakuna vipindi vya ziada.

Msuli wako na jitihada ndizo zitaamua ufaulu wako. Special school watu wanasoma mno. Kukaa darasani kuanzia saa moja usiku mpaka saa 12 asubuhi ni jambo la kawaida sana.

Unafuu pekee wanaoupata labda ni kwa kukutana wanafunzi wenye uwezo wa hali ya juu kwa pamoja. Wanafundishana na kueleweshana.

Lakini bado wapo wanafunzi wanaosoma shule za kawaida wanaopasua mno. Kwa viwango vya kutisha ambayo baadhi ya wanafunzi wa Special schools hawajaufikia.

Shule inachangia sehemu ndogo sana katika ufaulu wa Mwanafunzi hasa kwa shule za serikali za kidato cha 5 na 6. Nidhamu na commitment ya mwanafunzi ndiyo itaamua kila kitu.
 
Nikiri, mimi ni mmoja wa Wanafunzi waliowahi kusoma hizo shule Maalum (special school).

Kwa level ya Kidato cha 5 na 6, hakuna umaalum. Walimu ni wale wale wa shule za kawaidaa ziada.

Msuli wako na jitihada ndizo zitaamua ufaulu wako. Special school watu wanasoma mno. Kukaa darasani kuanzia saa moja usiku mpaka saa 12 asubuhi ni jambo la kawaida sana.

Unafuu wanaoupata labda ni kwa kukutana wanafunzi wenye uwezo wa hali ya juu kwa pamoja. Wanafundishana na kueleweshana.

Lakini bado wapo wanafunzi wanaosoma shule za kawaida wanaopasua mno. Kwa viwangona katika ufaulu wa Mwanafunzi hasa kwa shule za serikali za kidato cha 5 na 6. Nidhamu na commitment ya mwanafunzi ndiyo itaamua kila kitu.

umeongea ukweli mkuu. Lakini hayohayo mazingira ya kumfanya mtoto afaulu ndiyo yanayohitajika. Mwaka jana hizi shule zimetoa 95% ya wanafunzi waliochukua samia scholarship.
 
Back
Top Bottom