Sikubaliani na Spika Tulia Ackson suala la mabasi kusafiri usiku

kwenda21

JF-Expert Member
Mar 11, 2014
3,420
3,391
MABASI KUTEMBEA KWA SAA 24

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson ameishauri Wizara ya Mambo ya Ndani kuangalia upya amri inayokataza mabasi ya abiria kutembea barabarani baada ya saa 6 usiku.

"Nafikiri hili jambo nimewahi kulisemea mahali pengine, ni muhimu Serikali ilitazame kwa ujumla wake. Tunazuia magari saa 6 kwa sababu ipi? Kwa sababu madereva ni walewale wanaotuendesha sisi na wanao endesha hayo magari mengine, madereva wanapitia masomo yaleyale. Kama kuna mahali pana mapungufu tuyafanyie kazi hayo mapungufu"

Ameongeza, "Lakini kuzuia abiria halafu anakaa hapo halafu gari inaondoka baada ya saa 4 labda saa 10 inaondoka au saa 11 inaondoka, sasa sijui tunakuwa tumezuia nini, hasa katika kapindi hiki ambacho Serikali inafanya juhudi kubwa sana ya kuboresha miundombinu ya barabara."
---

Naona Spika anasisitiza hili suala kuwa basi zisafiri usiku, mimi nasema hapana, kwanza atuambie sababu ya yeye kusisitiza hili jambo ni kwanini hasa na kuna nini?

Pili anajua ugumu wa night shift? Anajua madhara ya kutokulala usiku? Je, barabara zetu zina traffic light za kutosha Dar kwenda mikoani? Usalama wetu utakuaje?
 
  • Natamani iimarike hata dakika hii.
  • Wale wa Iringa - Dom; Moshi - Dar, Mbeya - Dar n.k wanayafurahia maisha ya kuanza safari saa 1,2 usiku.
  • Abiria wa on- transit za ndani tutapumua. Inakera aisee unafika mkoa flani saa 9 jioni unaambiwa hakuna basi ya kwenda mikoa mingine mpaka siku inayofuata asubuhi. Inatishia tu kuzururazurura.
 
Naona Spika anasisitiza hili swala kuwa basi zisafiri usiku, mimi nasema hapana, kwanza atuambie sababu ya yeye kusisitiza hili jambo ni kwanini hasa na kuna nini?

Pili anajua ugumu wa night shift? Anajua madhara ya kutokulala usiku? Je, barabara zetu zina traffic light za kutosha Dar kwenda mikoani? Usalama wetu utakuaje?
Kuna matajiri wapo nyuma yake.Nilimwamini sana kuwa ni mkweli kwa Sasa naona nae anatumiwa na watu kwa manufaa yao binafsi.Angetwambia kwanza .Je ajali zimeisha?
 
Safari za usiku ni muhimu sana... Mimi napenekeza ziwepo.. imagine mtu umepata dharula upo dar kesho inabid ufike mbeya. Unapanda chap usiku.

Safari za mchana zina garibu zaid ya siku mbili kwenda sehemu na kurudi.
 
Naona Spika anasisitiza hili swala kuwa basi zisafiri usiku, mimi nasema hapana, kwanza atuambie sababu ya yeye kusisitiza hili jambo ni kwanini hasa na kuna nini?

Pili anajua ugumu wa night shift? Anajua madhara ya kutokulala usiku? Je, barabara zetu zina traffic light za kutosha Dar kwenda mikoani? Usalama wetu utakuaje?

Binafsi naunga mkono kwa asilimia 100% kwa mabasi kutembea usiku ila ya anze kwa njia ambazo ni salama ni kimaanisha route kama za Dar/ Moro/to Dodoma, Dar/Moshi to Arusha; Morogoro/Moshi to Arusha nk
Zile route ambazo sio salama kwa sababu mbali mbali ziachwe kwanza.

Nafikiri inadumaza maendeleo kwa kuwa na watu /wazalishaji karibia 20,000 kila siku wapo barabarani mchana kutwa kama Abiria - hawafanyi kazi.

Wafanya Biashara; wanataka kusafiri usiku ili ikifika asubuhi wafunge mzigo jioni waondoke na sio kupoteza muda mwingi barabarani mchana kutwa.

Nchi za wenzetu, miji hailali kwa sababu kazi zote na usafirishaji zinaendelea.

Na kuthibiti mwendo: Mabasi yawahi kuondoka kati ya 18h00 hivi na 20h00 ina maana hayatakuwa na haja ya kukimbia sana kwani yakifika yanakokwenda usiku 03h00 - 04h00 abiria hawatapenda. Abiria watataka yafike kumekucha

Na hii haimaanishi kuwa mabasi hayatatembea mchana; Mabasi yataendelea kuwepo Mchana na usiku. Abiria atachagua analotaka
 
Naona Spika anasisitiza hili swala kuwa basi zisafiri usiku, mimi nasema hapana, kwanza atuambie sababu ya yeye kusisitiza hili jambo ni kwanini hasa na kuna nini?

Pili anajua ugumu wa night shift? Anajua madhara ya kutokulala usiku? Je, barabara zetu zina traffic light za kutosha Dar kwenda mikoani? Usalama wetu utakuaje?
kwani umelazimishwa kupanda magari ya usiku
 
Naona Spika anasisitiza hili swala kuwa basi zisafiri usiku, mimi nasema hapana, kwanza atuambie sababu ya yeye kusisitiza hili jambo ni kwanini hasa na kuna nini?

Pili anajua ugumu wa night shift? Anajua madhara ya kutokulala usiku? Je, barabara zetu zina traffic light za kutosha Dar kwenda mikoani? Usalama wetu utakuaje?
Huwezi kujua umuhimu wa kusafiri Usiku kama wewe huwa unasafiri kwa mwaka mara moja kwenda kuangalia tu familia,nitakupa mfano

Mtu anatoka Mozambique saa 11 asubuhi anaingia Songea Saa 1 usiku inabidi alale aondoke na gari ya kesho yake ya saa 12 asubuhi na anaingia tena Dar usiku na inabidi alale tena,huko kulala wanalala guest na ni zaidi ya alfu20,na hata ukimaliza kufunga mizigo yake inabidi tena alale ili aondoke asubuhi kutoka Dar kuludi Songea

Ukipiga hesabu wametumia wastani wa alfu60 na kupoteza mda bila sababu,kila mwezi yuko njiani,anapoteza wastani wa 1,800,000 kwa mwaka
Wakati nikitoka Mozambique kupitia Malawi,utatoka huku saa 12 ya asubuhi unaingia Lilongwe saa 1 ya usiku,saa 2.ya Usiku kuna basi linalotoka Lilongwe to Dar anaingia border saa 11 alfajiri
Umeona faida ya kusafiri Usiku
 
Lingeanza hata leo,saa moja Usiku unapanda gari mbezi, alfajiri uko Mbeya,unamaliza mishe zako,jioni unapanda gari kwenda Dodoma unapiga mishe zako jioni unapanda gari kwenda Arusha etc ......ni kutengeneza mazingira mazuri tu safari za usiku zinarahisisha mtu anayeenda mara moja na kuondoka........mfano unaenda Mbeya na huhitaji kulala inapunguza gharama sana
 
Huwezi kujua umuhimu wa kusafiri Usiku kama wewe huwa unasafiri kwa mwaka mara moja kwenda kuangalia tu familia,nitakupa mfano

Mtu anatoka Mozambique saa 11 asubuhi anaingia Songea Saa 1 usiku inabidi alale aondoke na gari ya kesho yake ya saa 12 asubuhi na anaingia tena Dar usiku na inabidi alale tena,huko kulala wanalala guest na ni zaidi ya alfu20,na hata ukimaliza kufunga mizigo yake inabidi tena alale ili aondoke asubuhi kutoka Dar kuludi Songea

Ukipiga hesabu wametumia wastani wa alfu60 na kupoteza mda bila sababu,kila mwezi yuko njiani,anapoteza wastani wa 1,800,000 kwa mwaka
Wakati nikitoka Mozambique kupitia Malawi,utatoka huku saa 12 ya asubuhi unaingia Lilongwe saa 1 ya usiku,saa 2.ya Usiku kuna basi linalotoka Lilongwe to Dar anaingia border saa 11 alfajiri
Umeona faida ya kusafiri Usiku
Uko sahihi kabisa mkuu, inapunguza gharama na muda
 
Mimi sipandi pia

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
Yaani Siyo Gari zote zitakuwa zinasafiri Usiku,hapana utakuwepo utaratibu wa mda Mabasi kuondoka stendi,mfano unakuta Songea to Dar kuna kuanzia gari ya kuondoka saa 12 ya asubuhi saa 4 asubuhi saa 8 mchana saa 12 jioni na saa 2 usiku.Sasa mwenyewe utachagua

Kwanza itapunguza msongamano wa magari njiani,tofauti sasa hivi ambapo mabasi yanaondoka kwa mda mmoja yakipishana sana ni dakika, matokeo yake yanajazana barabarani na kusababisha ajali
 
Kuna matajiri wapo nyuma yake.Nilimwamini sana kuwa ni mkweli kwa Sasa naona nae anatumiwa na watu kwa manufaa yao binafsi.Angetwambia kwanza .Je ajali zimeisha?
Labda nikulize swali,una kundi la mifugo mingi,halafu njia ya kwenda malishoni ni nyembamba,utaifungulia kwa mkupuo,au utaifungulia kwa makundi,

Jibu utaifungulia kwa makundi ili kupunguza msongamano, Angalia fujo inayotokea Stendi ya Magufuri mabasi yanapoondoka asubuhi,Naamini gari zikianza kusafiri usiku ajali zitapungua
 
Hiyo nzuri sana, binafsi huwa nasafiri sana usiku kwa noah za kibo. Wakianzisha mabasi itakuwa njema sana kwa kurahisisha shughuli.
Kuna siku nilikuwa nahitajika dodoma siku ya 2 saa 3 asubuhi na hapo mchana bado nina mishe nyingine.

Nilivyorudi nikafanya kazi fasta mpaka saa 5 usiku, nikachukua boda hadi kibo. Pale tukapata noah kama saa 7 hivi hadi dodoma, tulikuwa abiria watano, dereva akatuambia tulipie 30k badala ya 25k kwa sababu haitamlipa inabidi iwe na abiria 6 mpaka 7 ndio tungelipa 25.
Uzuri wake hakuna aliyekuwa na njaa kati yetu, tukasema piga moto.

Dereva alipiga moto bila kupakia mtu, breki ya kwanza CBE saa 2 kasoro asubuhi.
Nilifanya yaliyonipeleka saa 11 jioni nikamaliza. Nikasema silali, nikarudi palepale CBE. Pale tukapata alphard watu kama 8. Saa 12 tukaondoka, saa 6 usiku mbezi. Hakuna basi lililotupita njiani.
 
Labda nikulize swali,una kundi la mifugo mingi,halafu njia ya kwenda malishoni ni nyembamba,utaifungulia kwa mkupuo,au utaifungulia kwa makundi,

Jibu utaifungulia kwa makundi ili kupunguza msongamano, Angalia fujo inayotokea Stendi ya Magufuri mabasi yanapoondoka asubuhi,Naamini gari zikianza kusafiri usiku ajali zitapungua
Usafiri wa mabasi usiku ulisimamishwa mwaka 1992 baada ya ajali mbaya sana ya Basi la super star kutoka Dodoma kwenda Dar.Kwa Sasa hali ya usalama kwa usafiri wa mikoani siyo nzuri.Tunapoteza ndugu zetu kila siku na bado hatujapata ufafanuz wa kuzuia hizo ajali.Na ajali hizo zinatokea mchana.Kwa hiyo vifo vya barabarani wakati wa mchana mnaona havitoshi mnataka viongezeke zaid na zaid.Kuna malori mengi yanaua watu kwa kugonga mabasi kila siku mchana.Je usiku Itakuwa vip?Na naona hata polisi wapo kimya tu wanafurahia vifo vya watu.Tungetafuta kwanza ufumbuz wa kupunguza ajali na baadae ndio tuone umuhimu wa safari za usiku.
 
Hawa madereva machizi wa mabasi na ubovu wa barabara bora tubaki kusafiri mchana tu
 
Route za usiku safi sana, kuna michongo ya kazi unapata saa 10 jioni afu interview ni kesho yake asubuhi saa mbili, pakiwa na mabasi yanayofanya safari za usiku inakua poa sana
 
Usafiri wa mabasi usiku ulisimamishwa mwaka 1992 baada ya ajali mbaya sana ya Basi la super star kutoka Dodoma kwenda Dar.Kwa Sasa hali ya usalama kwa usafiri wa mikoani siyo nzuri.Tunapoteza ndugu zetu kila siku na bado hatujapata ufafanuz wa kuzuia hizo ajali.Na ajali hizo zinatokea mchana.Kwa hiyo vifo vya barabarani wakati wa mchana mnaona havitoshi mnataka viongezeke zaid na zaid.Kuna malori mengi yanaua watu kwa kugonga mabasi kila siku mchana.Je usiku Itakuwa vip?Na naona hata polisi wapo kimya tu wanafurahia vifo vya watu.Tungetafuta kwanza ufumbuz wa kupunguza ajali na baadae ndio tuone umuhimu wa safari za usiku.
Unajua watu wasiojua udereva vizuri na matumizi ya vyombo vya moto barabarani,wanaamini ukiendesha gari mchana kuna usalama zaidi kuliko Usiku,si kweli,

Kwanza barabara kama ya lami mchana inakuwa na joto zaidi kuliko usiku,na hii hupeleka gari kupata moto matairi ambayo ndiyo kisababishi cha asilimia kubwa kwa ajali.

Pili dereva anaasilimia kubwa ya kusinsia mchana kuliko usiku,hasa sehemu zenye joto kali

Ni rahisi kuona kitu kilichombele yako kwa umbali mrefu zaidi kuliko mchana,sababu gari ikiwa mbele yako unaanza kuiona mbali zaidi,tofauti na mchana
 
Back
Top Bottom