Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,372
Kwanza naomba ieleweke hii sio kodi bali ni kuchangia elimu au tunaweza kuita kuchangia Mfuko wa Elimu kwa watanzania kugharamia elimu ya shule ya msingi na elimu ya juu.
Napendekeza kila mtanzania mwenye kumiliki simu ya mkononi achangie shilingi 10,000 kwa mwaka mzima na fedha zitazopatikana zitumike kugharamia elimu ya shule ya msingi na elimu ya juu.
Kama sikosei, watanzania wanaomiliki simu za mkononi wanafikia 40, 000,000 hivyo kwa mwaka mzima serikali inaweza kukusanya 400,000,0000,0000.
40,000,000 x10,000 =400,000,000,000.
Wazo hili likikubalika, tunafuta madeni yote ya Bodi ya Mikopo na Bodi ivunjwe na kisha kuunda chombo kipya na kukipa jukumu la kusimamia ukusanyaji wa michango hiyo na kutoa fedha kugharamia elimu ya msingi na elimu ya juu.
Kuna watu watasema huku ni kumuongezea mzigo mwananchi, lakini tujiulize kipi bora kuchangia kwa njia hii au kila mtu abebe mzigo wa kulipa ada kivyake hasa kupitia makato katili ya Bodi ya Mikopo kwa elimu ya juu?
Tukumbuke elimu ya msingi ni ya lazima kwa kila mtanzania, hivyo wote tunapaswa kuchangia hata kama unasomesha watoto wako katika shule za private.
Tukumbuke pia tutakuwa tumesaidia watanzania wenzetu masikini wa huko vijijini na ambao pengine wangetuomba fedha sisi ndugu zao wa mijini kusomesha watoto wao.
Pia lazima tuelewe huku mijini barabara ni zuri, shule ni nzuri, n.k kulinganisha na huko vijijini, ingawa na wao wanalipa kodi kama sisi wa mijini, ila vijijini kumesahaulika. Kwa msingi huo, sio vibaya hata kama wao ndio watafaidika zaidi kwa upande wa elimu bure.
Halikadhalika, kwa upande wa kutoa elimu bure vyuo vikuu na kufuta madeni yote ya Bodi ya Mikop kutatufaidisha watanzania wote wa mijini na vijijini, masikini na matajiri.
Hivyo, ni bora utaratibu wa kisheria uwekwe ili kila mwenye kumiliki simu achangie mfuko huu wa elimu utaoundwa kisheria.
Tusisaha pamoja na uwepo wa elimu bure, michango mashuleni bado ipo na juzi serikali imetamka kuwa ilitangaza elimu bila ada na si elimu bure kwahiyo hakuna tunachokwepa.
Utaratibu uwe ni kuchangia wastani wa shilingi 833 kwa mwezi na itakuwa nafuu kuliko kila mtanzania kubeba mzigo wa elimu ya mwanae au ndugu yake kivyake.
Fedha ambazo sasa zinatumika kughramia elimu bila ada zielekezwe kwenye sekta nyingine kama afya kwa maana ya kujenga mahospitali, kununua madawa, n.k na faida hii itatugusa watanzania wote matajiri na masikini.
Tukumbuke hata misaada tunayopewa na nchi wahisani ni kodi za wananchi wa mataifa hayo na sio zipo tu kwasababu zipo.
Hatuna teknolojia, viwanda na karibu kitu tunaagiza kutoka nje, hivyo ni bora tutafute namna ya kujikwamua ila pasipo kuumizana, vinginevyo deni la Taifa litafika mahali pa kutisha na tukajikuta tuna Bajeti za kulipa madeni zinazoongezeka kila mwaka badala ya kupungua.
Tunaweza kuanza kwa kufanya majaribio na tukiona chanzo hiki ni endelevu na cha uhakika, basi ndio tufikie hatua ya kuivunja HESLB na kuunda chombo kipya.
Education cost sharing pia inaweza kuwa introduced katika mauzo na manunuzi ya bidhaa zingine kama vile mauzo ya ardhi/viwanja, n.k mbali mradi tu tuzo ziwe rafiki kwa wananchi na malengo yatimie.
Faida moja ya kuwa na nchi kubwa yenye population kubwa(kwa mtazamo wangu), ni uwezekano wa ku-share burden ya kugharamia huduma ambazo ni muhimu kwa jamii ila ni za ghali(mfano elimu ya juu na afya) kwa kuchangia kidogo kupitia huduma muhimu lakini zenye gharama nafuu(mfano kupitia umiliki wa line za simu za simu).
Penye nia pana njia.