Serikali ianzishe Education Cost Sharing kupitia simu za mkononi kugharamia elimu ya msingi na elimu ya juu kwa Watanzania wote

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,998
144,329
Kwanza naomba ieleweke hii sio kodi bali ni kuchangia elimu au tunaweza kuita kuchangia Mfuko wa Elimu kwa watanzania kugharamia elimu ya shule ya msingi na elimu ya juu.

Napendekeza kila mtanzania mwenye kumiliki simu ya mkononi achangie shilingi 10,000 kwa mwaka mzima na fedha zitazopatikana zitumike kugharamia elimu ya shule ya msingi na elimu ya juu.

Kama sikosei, watanzania wanaomiliki simu za mkononi wanafikia 40, 000,000 hivyo kwa mwaka mzima serikali inaweza kukusanya 400,000,0000,0000.

40,000,000 x10,000 =400,000,000,000.

Wazo hili likikubalika, tunafuta madeni yote ya Bodi ya Mikopo na Bodi ivunjwe na kisha kuunda chombo kipya na kukipa jukumu la kusimamia ukusanyaji wa michango hiyo na kutoa fedha kugharamia elimu ya msingi na elimu ya juu.

Kuna watu watasema huku ni kumuongezea mzigo mwananchi, lakini tujiulize kipi bora kuchangia kwa njia hii au kila mtu abebe mzigo wa kulipa ada kivyake hasa kupitia makato katili ya Bodi ya Mikopo kwa elimu ya juu?

Tukumbuke elimu ya msingi ni ya lazima kwa kila mtanzania, hivyo wote tunapaswa kuchangia hata kama unasomesha watoto wako katika shule za private.

Tukumbuke pia tutakuwa tumesaidia watanzania wenzetu masikini wa huko vijijini na ambao pengine wangetuomba fedha sisi ndugu zao wa mijini kusomesha watoto wao.

Pia lazima tuelewe huku mijini barabara ni zuri, shule ni nzuri, n.k kulinganisha na huko vijijini, ingawa na wao wanalipa kodi kama sisi wa mijini, ila vijijini kumesahaulika. Kwa msingi huo, sio vibaya hata kama wao ndio watafaidika zaidi kwa upande wa elimu bure.

Halikadhalika, kwa upande wa kutoa elimu bure vyuo vikuu na kufuta madeni yote ya Bodi ya Mikop kutatufaidisha watanzania wote wa mijini na vijijini, masikini na matajiri.

Hivyo, ni bora utaratibu wa kisheria uwekwe ili kila mwenye kumiliki simu achangie mfuko huu wa elimu utaoundwa kisheria.

Tusisaha pamoja na uwepo wa elimu bure, michango mashuleni bado ipo na juzi serikali imetamka kuwa ilitangaza elimu bila ada na si elimu bure kwahiyo hakuna tunachokwepa.

Utaratibu uwe ni kuchangia wastani wa shilingi 833 kwa mwezi na itakuwa nafuu kuliko kila mtanzania kubeba mzigo wa elimu ya mwanae au ndugu yake kivyake.

Fedha ambazo sasa zinatumika kughramia elimu bila ada zielekezwe kwenye sekta nyingine kama afya kwa maana ya kujenga mahospitali, kununua madawa, n.k na faida hii itatugusa watanzania wote matajiri na masikini.

Tukumbuke hata misaada tunayopewa na nchi wahisani ni kodi za wananchi wa mataifa hayo na sio zipo tu kwasababu zipo.

Hatuna teknolojia, viwanda na karibu kitu tunaagiza kutoka nje, hivyo ni bora tutafute namna ya kujikwamua ila pasipo kuumizana, vinginevyo deni la Taifa litafika mahali pa kutisha na tukajikuta tuna Bajeti za kulipa madeni zinazoongezeka kila mwaka badala ya kupungua.

Tunaweza kuanza kwa kufanya majaribio na tukiona chanzo hiki ni endelevu na cha uhakika, basi ndio tufikie hatua ya kuivunja HESLB na kuunda chombo kipya.

Education cost sharing pia inaweza kuwa introduced katika mauzo na manunuzi ya bidhaa zingine kama vile mauzo ya ardhi/viwanja, n.k mbali mradi tu tuzo ziwe rafiki kwa wananchi na malengo yatimie.

Faida moja ya kuwa na nchi kubwa yenye population kubwa(kwa mtazamo wangu), ni uwezekano wa ku-share burden ya kugharamia huduma ambazo ni muhimu kwa jamii ila ni za ghali(mfano elimu ya juu na afya) kwa kuchangia kidogo kupitia huduma muhimu lakini zenye gharama nafuu(mfano kupitia umiliki wa line za simu za simu).

Penye nia pana njia.
 
Watanzania wakamuliwe halafu mafisadi waendelee kutumbua kodi ?

Kama mmeishiwa hoja heri muache ccm iendelee kutawala.
Hata misaada tunayopewa na nchi tajiri ni kodi za raia wa nchi hizo hivyo tusijisahau sana.
 
... kwa hili siungi mkono bro! Wengine wazaliane ovyo wengine wachangie kusomesha? Kila mtu abebe mzigo wake tafadhali. Hii itachochea uzaaji ovyo; no family planning, no what! Unapokuwa chumbani na mkeo/hawara fikiria mara mbili mbili "yatokanayo" sio kujiendea tu!
 
Sioni kama kuna mantiki yoyote ya kukamua wananchi kodi kwenye simu wakati huko kwenye simu kwenyewe wanakatwa VAT kwenye Vocha, wanakatwa kwenye miamala ya simu nk.

Kwanini tusitumie utalii kama source ya income ya kuweza kuhudumia elimu,

Tukiweza kupata watalii milioni 3 tu kwa kwa mwaka hata hilo wazo la kukamua wananchi 10k a year kwenye simu halitakuwepo.
 
Hata misaada tunayopewa na nchi tajiri ni kodi za raia wa nchi hizo hivyo tusijisahau sana.
Mkuu mimi nadhani kabla ya kufungua tena ''tobo'' jingine la kuwakamua wananchi tujaribu kupangilia vizuri kilichopo. Nasema hivyo kwa sababu Tanzania tatizo letu kubwa ni matumizi.

Kuna mifano mingi ya matumizi mabaya. Mfano: Wilaya zimejaa viongozi wengi wanaolipwa na hapo hapo ''kupiga'' fedha nyingi za umma bila kuwa na umuhimu.

Je hatuwezi kuwapunguza? Bunge letu ni kubwa na limeajaa wabunge wengi ambao hawana faida yoyote zaidi ya kupokea mshahara na posho. Je hatuwezi kuwapunguza?

Serikali inanunua magari mengi ya kifahari bila sababu. Je, hatuwezi kununua magari ya kawaida? Viongozi wengi wa serikali wanasafiri kwa kutumia business class kwenye ndege na kulala hotel za gharama.

Je, hatuwezi kurekebisha? Mifano ipo mingi sana na fedha zinazopotea ni nyingi kuliko zinazotumika kihalali.
 
Kwa mentalily hizi, tutabaki kuishi kwa madeni kama nchi mpaka siku Yesu anarudi.
Kwanza hiyo idadi uliyoweka ni ya simu au lines? Halafu hivi unafikiri hiyo elfu kumi uliyopendekeza ni fedha kidogo sana?

Kifupi mapendekezo yako hayafai kabisa!
 
Kwanza naomba ieleweke hii sio kodi bali ni kuchangia elimu au tunaweza kuita kuchangia Mfuko wa Elimu kwa watanzania kugharamia elimu ya shule ya msingi na elimu ya juu...
Huna akili kabisa, kukopa ukope wewe huko Helsb alafu deni tukulipie sisi. Cost sharing ya nini wakati tunalipa kodi na mapato yanapatikana.
 
Kwanza hiyo idadi uliyoweka ni ya simu au lines? Halafu hivi unafikiri hiyo elfu kumi uliyopendekeza ni fedha kidogo sana?

Kifupi mapendekezo yako hayafai kabisa!
Ni ndogo sana ukilinganisha na gharama za elimu tunazolipa ila hatutaki tu kufikiri kwa mapana.

Usipochangia unafungiwa line yako na kuweka mechanisms zingine za kuwabana watu wachangie.
 
tuisaidie serikali kwenye elimu ya msingi na sekondari, kila mwenye mtoto agaramie kumsomesha mtoto wake angalau hadi sekondari (ada za shule ya msingi hadi sekondari sio aghali)

huwezi kuwa na mtoto tokea shule ya msingi hadi chuo kikuu hujamgharamia kwa chochote kwenye masomo alafu uje utarajie aje kushindana na mtoto ambaye kuanzia shule ya chekechea analipiwa sh mil+.

elimu bure inaua elimu yetu. kitu kizuri lazima ukigaramie japo kidogo
 
Kwa mentalily hizi, tutabaki kuishi kwa madeni kama nchi mpaka siku Yesu anarudi.
Hakuna cha mentality nchi hii fedha nyingi huwa zinahudumia watu ambao kimsingi hawana lolote wanalofanya zaidi ya kupiga pesa.

Hivi ulisikia vizuri bajeti ya TAMISEMI ambayo kuna billions za pesa zilielekezwa kukarabati na kujenga makazi ya wakuu wa mikoa, wakurugenzi, das na ras ?.

Tubadili kwanza mfumo wa matumizi yetu kabla hatujafikiria hata hicho chanzo chako cha mapato.

Kama mwanachadema hukutakiwa kufikria namna bora ya kuwakamua wananchi nilitegemea utakuwa na wazo bora zaidi ya kuwaibia wananchi.

Kuwatoza wananchi fedha kwenye simu zao wakati kipindi wananunua walilipa VAT, vocha wanalipa VAT, miamala ya fedha mingine wanalipa kodi ni kufanya ujambazi wa kitaasisi
 
Huna akili kabisa, kukopa ukope wewe huko Helsb alafu deni tukulipie sisi. Cost sharing ya nini wakati tunalipa kodi na mapato yanapatikana.
Mna mapato gani nyie kama nchi?Mnafikiri tutapiga hatua kama nchi kwa bajeti hizi tegemezi?

Ukweli ni kwamba, watanzania hampendi kulipa kodi na watanzania wanaolipa kodi ni asilimia ndogo sana ya watanzania wote wanaoingiza kipato.

Tuko tayari kuchangia harusi na vitu vya aina hiyo kuliko hata kuchangiana kwenye mambo ya elimu.

Ukitaka kujua au kuolewa, michango utaipata ila ukikwama ada ya mtoto hata ndugu kwenye kuchangia unaweza usiwaone.

We have mental stupidity katika hili.
 
Nafikiri tungeachana na manunuzi ya magari ya kifahari na ya gharama kwenye office za umma...

Haiwezekani mara mkurugenzi anunue na kutembelea gari la millioni 400 huku kukiwa na tatizo la maji na wanafunzi wanakaa chini...

Tuanzie hapo kupinga matanuzi tujikite kwenye uhalisia!

Na napendekeza mishahara yote kwa viongozi wa umma wa ngazi ya juu iwekwe wazi nikimaanisha hata makato ndio mjionee huyo mwananchi anayeenda kubanwa mbavu anatendewa haki?
 
Upi utakuwa utaratibu wa kuhakikisha kila mtanzania anachangia? na wale wasiokuwa na uwezo huo wafanyweje hasa huko vijijini? watu wanaweza kimbia nyumba zao wakiona migambo wanaulizia risiti za malipo.

Hicho kiasi kitachopatikana umekipigia hesabu vizuri, lakini ukumbuke kitakabidhiwa kwa mchwa wanaotafuna kila kitu, upi utakuwa utaratibu mzuri wa kuhakikisha kiasi kinachopatikana kinatumika kwa lengo kusudiwa?
 
Kwanza naomba ieleweke hii sio kodi bali ni kuchangia elimu au tunaweza kuita kuchangia Mfuko wa Elimu kwa watanzania kugharamia elimu ya shule ya msingi na elimu ya juu...
wazo ni zuri ila sio kila anaemiliki simu ana uwezo mkubwa kihivo, pia sio rahisi sana serikali kuchangiwa maaana kuna watu wnaweza fanya yao
 
Ni ndogo sana ukilinganisha na gharama za elimu tunazolipa ila hatutaki tu kufikiri kwa mapana.

Usipochangia unafungiwa line yako na kuweka mechanisms zingine za kuwabana watu wachangie.
Tuna michango mingi sana nchi hii, karibu kila huduma unayonunua kuna michango imeambatanishwa! Iwe umeme, maji, mafuta nk.

Tafadhali lipia elimu yako! Bora ungependekeza fedha ya mkopo wa elimu iongezwe ili watu wengi zaidi wanufaike!
 
Mkuu mimi nadhani kabla ya kufungua tena ''tobo'' jingine la kuwakamua wananchi tujaribu kupangilia vizuri kilichopo. Nasema hivyo kwa sababu Tanzania tatizo letu kubwa ni matumizi. Kuna mifano mingi ya matumizi mabaya...
Unachosema ni sahihi kabisa, na kwa nchi hii, tunahitaji sheria ya kunyonga kudhibiti wizi na ufisad serikalini vinginevyo wizi na ufisadi haviwezi kwisha nchi hii.

Tukiudi kwenye mada, kama ni kukamuliwa, basi tunakamiliwa kwenye matumaizi kama ya kutuma na kupokea fedha kupitia simu za mkononi ila tumeshazoe na tunaomba kawaida tu, ila wanaofaodika ni makampuni ya simu ingawa serikali pia inapata kodi.

Kuna gharama tunazoweza kuipunguzia serikali na mtanzania mmoja mmoja iwapo tutakuwa tayari kubeba gharama hiyo kama Taifa kama ambavyo tunachangia harusi na kuwezesha harusi kufingwa pasipo Bwana harusi na ndugu zake kubeba gharama hiyo peke yao.
 
Back
Top Bottom