Serikali iangalie Watoza Ushuru wa Mbeya wanatunyanyasa Wafanyabiashara wa mbao

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Sisi Wafanyabiashara wa mbao tuliopo Mbalizi, Mbeya Vijijini tuna malalamika kuhusu Watoza Ushuru wanaosimama kwenye mageti.

Wanatengeneza mazingira ya rushwa kwa kutaka kutupiga faini na kututaka tukate ushuru wa TP (Transportation Permit) mara mbilimbili.

Utaratibu uliopo tunaopewa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ni kuwa unaweza kukata TP popote ulipo ambapo kuna ofisi yao kwa kuwa ni fedha ya Serikali, ukionesha risiti inakuwa sawa, unachotakiwa ni kueleza tu wakati wa kukata TP kuwa unaenda kuchukua mbao wapi na ngapi.

Mara ya kwanza tulikuwa tunakata pale Airport ya zamani Mbeya Mjini, kisha unaenda kubeba mbao hata kama ni Chunya, kwa kuwa TP ilikuwa inajieleza ratiba na idadi ya mbao, baadaye utaratibu ukabadilika na maafisa wa kukata TP akawa Mbeya Vijijini na Ileje.

Mfano ukikata TP upande wa Kata ya Ileje, ukisafirisha mzigo ukifika geti la Mbeya DC napo wanataka ulipe ushuru kwa mara nyingine, tofauti na hapo wanakutoza faini ya shilingi milioni 1.

Tunaomba upande wa misitu Wilaya ya Mbeya DC warekebishe utaratibu huu kwa kuwa unatuumiza Wafanyabiashara.

Tukiuliza ofisini wanasema wao hawajawatuma maafisa wa getini kufanya hivyo wanavyofanya, watoza ushuru ni changamoto.

Kitu kingine unaweza kuwaambia kuwa unaenda kuchukua mbao 1000, lakini ukifika unakuta kuna mbao 800 au 700 wao wanakulazimisha ukate ushuru mzigo wote hata kama hujapata idadi ya mbao ambazo hauna.

Usumbufu upo zaidi karibu na geti la Izumbwe lililopo karibu na Mbalizi, wanataka ulipe ushuru 105,000 kama haufanyi hivyo hauwezi kupita na mzigo au utoe rushwa ndio upite.
 
Back
Top Bottom