Kwenye kila budget zetu zote zina sehemu mbili, budget ya recurrent na budget ya development. Budget ya recurrent, ni budget ya matumizi ya kawaida, hii ni budget tunayojitegemea kutoka vyonzo vyetu vya ndani, na nakisi kwenye recurent, tunakopa!, fedha hizi hazijazuiliwa na wala hatujazuiwa na yeyote kukopa popote!. Umasikini wetu kwa kiasi kikubwa haswa deni la taifa kumetokana na hili, kutumia kuliko uwezo wetu wa kuzalisha!.
Kubwa zaidi ni pale sio tuu tunapotumia kuliko tulichozalisha bali ni pale tunapotumia kile ambacho hatukubudget kama dharura, alafu dharura yenyewe sio majanga kama natural disasters bali sherehe, kama yale maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru!, Tangu ile siku tunapata uhuru, ilijulikana kabisa miaka 50 itakuwa ni lini, lakini we did not budget!, tukaifanya ni dharura!, ni dharura kama hizi, ndizo zinaingilia recurrent na kuifanya kumegwa kwa matumaini itafidiwa baadae!. Hivyo kama ni kweli, wafanyakazi wamekosa mishahara this time, sababu inaweza kuwa ni ile dharura ya ugonjwa ambayo hii ni dharura kweli!.
Budget ya pili ndio ile development, hii ni fedha ambayo haipo, ila tunaibudget according to projections na commitments za nchi wafadhili kugharimia miradi ya maendeleo, na hii ndio tunawatemea zaidi nchi wahisani, wafadhili, mikopo na fedha za ndani. Kusitishwa kwa misaada kwa kiasi kikubwa kutaathiri hii miradi ya maendeleo!. Kwa vile na sisi tunachangia miradi hii kwa fedha zetu za ndani, in this case reallocation is inevitable na ni kitu cha kawaida, lakini siku zote fungu ambalo liko very safe serikalini, ni fedha za mishahara, fedha ambazo zinaweza zikakosekana ni zile za O/C (other charges) lakini sio mishahara!.
Bahati mbaya sina hata mtumishi mmoja wa umma, nimjuaye ambaye ningeweza kumuuliza!.
Pasco