Olengurumwa: Uhaini waliopewa akina Dkt. Slaa unatia doa taifa na taswira ya Rais

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa amesema.

Pamoja na serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu kupongezwa na wadau mbali mbali wa haki za binadamu katika maeneo mengi ikiwemo kutoa uhuru wa kujieleza na kutoa maoni uhuru, sakata la kukamatwa wakosoaji wakubwa wa mkataba wa bandari Balozi Mstaafu Dkt. Willbroad Slaa, Wakili Boniface Mwabukusi na Mdude Nyagali kunaweza kutia dosari mazuri hayo pamoja na kuchafua taswira ya Rais Samia kimataifa endapo akikubali watuhumiwa hao kuwa na kesi ya uhaini.

Amesema, itakuwa ni historia katika awamu hii ya sita na pia itakuwa ni kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi kupata watu wanashtakiwa kwa makosa ya uhaini.

"Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni na kueleza fikra zake, katiba imetulinda, Wakili Mwabukusi, Mdude na Balozi Dkt. Slaa walikuwa wanafanya kwa mujibu wa katiba na kama kuna mahali popote waliteleza kwa maneno ya hapa na pale isiwe ni sababu ya kuwafungulia kesi kubwa kama hii na kuwazuia wao na Watanzania wengine wasikosoe" alisema Wakili Olengurumwa na kuongeza

"Kuanza kuwakamata wote wanaopinga mkataba wa bandari kuanzia kwa Wakili Madeleka sasa Slaa na wenzake litatutia doa kama Taifa, tunawashauri viongozi wetu kabla ya kufika mbali katika hatua hii ,hawa watu wasifunguliwe jalada la uhaini.”
 
Kwa Hili hata Mimi sioni sababu ya kupoteza Fedha Kwa kesi Hii..Tutadharaulika saaana kimataifa.Polisi Hasa IGP atumie Hekima Kwa Hili.Hata wananchi hawatawaamini ,,ni Vizuri kuaminika
Tuna tatizo la watu kuongozwa na hisia badala ya logic. Hii poor conclusion isiyo na grounds imara.
Mihemko inatupeleka chaka, watu warudi darasani kusoma falsafa.
 
Ukicheka na nyani utavua mabua. Hawa kina Dr Slaa wameshindwa kutumia uhuru wa maoni ipasavyo. Wameshindwa kuuelewa uungwana wa Rais Samia wakadhani ni UDHAIFU.

Wacha wanyee ndoo na nchi itulie. Mwambieni Olengurumwa aache vyombo vifanye kazi. Kama ana utetezi aende Mahakamani
 
Tunapotezaje pesa wakati watu wanahamasisha mapinduzi?
Hivi Mapinduzi unayajua weye au unayasikia tu unafikiri ni kama mchezo wa kuigiza wa Kaole group.

74EABEA3-628A-416A-9F31-ABC4AAA3B664.jpeg
 
Ukicheka na nyani utavua mabua. Hawa kina Dr Slaa wameshindwa kutukia uhuru wa maoni ipasavyo. Wameshindwa kuuelewa uungwana wa Rais Samia wakadhani ni UDHAIFU.

Wacha wanyee ndoo na nchi itulie. Mwambieni Olengurumwa aache vyombo vifanye kazi. Kama ana utetezi aende Mahakamani
nchi haiwezi kutulia kwa mtindo huo. Hakuna anayetaka kuipindua serikali. ambacho hakitakiwi ni mkataba mbovu wa bandari. kufunga watu sio suluhisho. inatujengea chuki zaidi baina yetu, tunajichafua kimataifa. wanaomshauri Rais wanampoteza. majitu machumia tumbo ndio yanayoiharibu hii nchi.

Mkataba na DPW uvunjwe, watu waachiwe huru, maisha yaendelee! VINGINEVYO.
 
Kauli zenye kuhamasisha umma, kuandamana na kuyatwaa madaraka, pengine watu wanashindwa kuelewa, mapinduzi sio lazima silaha za moto au majeshi yatumike, umma unaweza kuchochewa na kauli za kichochezi na hatimaye serakali ikapinduliwa!

Kauli, kauli, kauli..
 
Kwa Hili hata Mimi sioni sababu ya kupoteza Fedha Kwa kesi Hii..Tutadharaulika saaana kimataifa.Polisi Hasa IGP atumie Hekima Kwa Hili.Hata wananchi hawatawaamini ,,ni Vizuri kuaminika
Hatuna IGP mweledi. Kingai siyo mweledi
Pale anapaswa kutenguliwa apishe wenye uwezo wa kazi.

JEshi la.polisi linahitaji maboresho makubwa kimfumo na kiutendaji.
 
wa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni na kueleza fikra zake, katiba imetulinda, Wakili Mwabukusi, Mdude na Balozi Dkt. Slaa walikuwa wanafanya kwa mujibu wa katiba na kama kuna mahali popote waliteleza kwa maneno ya hapa na pale isiwe ni sababu ya kuwafungulia kesi kubwa kama hii na kuwazuia wao na Watanzania wengine wasikosoe" alisema Wakili Olengurumwa na kuongeza

Serikali inashangaza sana ,yaani unamshitaki mtu kwa makosa ya uhaini kisa ametamka kwenye Luninga au interview au kwenye whatsapp ,hivi walifatilia mapinduzi aliyofanya Mu7 wa UG au Desire Laurent Kabila? Kwani kuna nia ovu kwenye yale matamshi? Alipanga mikakati gani ,hivi watu watatu wanaweza kumpindua rais ikulu?
 
Serikali inashangaza sana ,yaani unamshitaki mtu kwa makosa ya uhaini kisa ametamka kwenye Luninga au interview au kwenye whatsapp ,hivi walifatilia mapinduzi aliyofanya Mu7 wa UG au Desire Laurent Kabila? Kwani kuna nia ovu kwenye yale matamshi? Alipanga mikakati gani ,hivi watu watatu wanaweza kumpindua rais ikulu?
Kuna mtu nimemuuliza hapo juu kama anayajua mapinduzi, awaulize kina John Okello na kina Karume.
 
Back
Top Bottom