Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 12,152
- 20,326
Kwa pamoja Jukwa la Katiba Tanzania, Tume ya haki za Binadamu, Tanganyika Law society na Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania wametoa tamkonna kuitaka mamlaka za serikali kuwaachia huru watuhumiwa wa Uhaini Dr Wilbroad Peter Slaa, Wakili Mwabukusi na Mwanaharakati Mdude Nyangali.
Sehemu ya tamko hilo inasema walikamatwa kwa tuhuma za uchochezi na baadae kubadilishiwa tuhuma kuwa za uhaini kitu kinachoonesha kuwa wanabambikiwa kosa kwa mijibu wa sheria za Kimataifa za upelelezi.
Hata hivyo wao kwa pamoja wanaamini kutoa maoni kuhusu mkataba wa DPW na Tanzania ni hako ya kila raia.
Wito wao kwa pamoja
1. Kuwaachia bila masharti kwa kuwa hawana hata dosari inayoonesha kosa la uhaini.
2. Wito kwa DCI ni kuwa imwachie mara moja Wakili Madeleka kwa kuwa wanaamini kukamatwa kwao kuna uhusiano na utoaji maoni kuhusu mkataba wa DPW na Tanzania.
3. Msisitizo umewekwa kuheshimu mapendekezo ya tume ya Haki Jinai ya Jaji Chande, kwa jeshi la polisi kutenda kwa weledi na kuepuka kubambikia keshi wananchi.
4. Wito kwa wanasiasa kuepuka kutoa matamko yanayochochea uvunjifu wa haki za binadamu.
Sikiliza mwenyewe hapa.
View: https://www.youtube.com/live/duzaiz4qjL4?feature=share