Serikali haioni hivi vichwa vilivyopo JamiiForums?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Kwanza, ninaipongeza kwa kumteua Mkurugenzi wa JF, Maxence Mello kuwa mjumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi. Naamini hawajakosea kumteua mtajwa.

Lakini inafahamu kuwa kuna vichwa vingine kibao, tena wanaotumia verified Id hivyo si kazi kuwapata, ambao wangeweza kuwa na mchango mkubwa katika nchi endapo wangepewa nafasi Serikalini?

Nitawataja alau wawili, wengine watatajwa na wana JF wengine.
 
Paschal Mayalla:
1. Ni msomi mwenye taaluma ya Sheria na uandishi wa habari

2. Ni Mwandishi wa Habari mwenye uzoefu wa miaka mingi

3. Ni mtu jasiri anayejiamini

4. Ni kada wa Chama Tawala asiye mwoga kukisemea pale inapobidi

5. Alishawahi kugombea nafasi ya ubunge EALA lakini kura hazikutosha

6. Anafaa kuwa Msemaji wa Serikali, Mwandishi wa Rais, Mbunge, Waziri, Katibu Tawala wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi wa TBC, Mkurugenzi wa Manispaa au Jiji na nafasi zinginezo zinazofana na hizo.
 
Nje ya Mada. Wenye Multiple IDs hapa JamiiForums wanawezaje Kuzimiliki, wakati Mimi GENTAMYCINE hii moja tu niliyonayo inanitoa Jasho?
 
Mshana Jr:
Japo ni mwana CHADEMA, lakini linapokuja suala la maslahi ya Taifa, masuala ya vyama huwekwa pembeni. Serikali isione aibu kumtumia kwa sababu tu ya itikadi zake za kisiasa. Mbona ilimchukus Profesa Kitila Mkumbo alipokuwa bado ni mwanachama wa ACT WAZALENDO, Anna, n.k. japo waliishia kuhamia CCM?

1. Ni mtu mwelewa mwenye exposure kubwa

2. Uandishi wake unaonesha kuwa ni msomi anayejitambua na mwenye uelewa wa mambo mengi

3. Ni Mtanganyika Mzalendo

4. Ni mtu anayesimamia kile anachokiamini. Akiamua kukosoa hufanya hivyo bila aibu. Kwa ufupi si mnafiki, ni mtu jasiri

5. Anaweza kuteuliwa kushika nafasi zisizo za kisiasa kama Ukatibu Tawala wa Mkoa, Ukurugenzi wa Masharika ya Umma, Mjumbe wa Bodi, ubalozi, n.k.
 
Back
Top Bottom