Hospitali ya Taifa Muhimbili yajibu hoja za Wana JamiiForums kuhusu vifo Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila

siata

Member
Joined
Dec 23, 2010
Messages
30
Points
95

siata

Member
Joined Dec 23, 2010
30 95
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU TUHUMA ZINAZOSAMBAA MITANDAONI KWAMBA WAGONJWA WENGI WANAPOTEZA MAISHA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI-MLOGANZILA.

Dar es Salaam. 06 Januari, 2020


Kumekuwa na taarifa kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Jamii Forum ambazo bila kuchanganua zinatuhumu kwamba Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila inasababisha vifo kwa wagonjwa. Uongozi wa hospitali unapenda kuwahakikishia Umma wa Watanzania kwamba habari hizi si za kweli na hazitoi picha halisi ya huduma ambazo zinazotolewa hospitalini hapa. Takwimu tulizonazo zinaonyesha kwamba wagonjwa wanaotibiwa MNH-Mloganzila wameongezeka katika makundi yote.

Wagonjwa wa nje wameongezeka kutoka 17,115 katika kipindi cha robo mwaka cha Julai hadi Septemba, 2018 kufikia wagonjwa 25,493 katika kipindi cha Julai hadi Septemba, 2019 ambalo ni ongezeko la asilimia 48.8. Aidha, wagonjwa wanaotibiwa na kulazwa wameongezeka kutoka 1,459 katika kipindi cha robo mwaka cha Julai hadi Septemba, 2018 na kufikia wagonjwa 2,795 katika kipindi cha Julai hadi Septemba, 2019 ambalo ni ongezeko la asilimia 91.6.

Wakati huo huo idadi ya vifo (mortality rate) ikipungua kutoka asilimia 14.9 iliyokuwepo katika kipindi cha robo mwaka cha Julai hadi Septemba, 2018 na kufikia asilimia 10.4 katika kipindi cha Julai-Septemba 2019. Aidha, takwimu za MNH-Upanga zinaonyesha kwamba katika kipindi cha robo mwaka cha Julai hadi Septemba 2018 wagonjwa waliolazwa walikua ni 12,375 ambapo kulitokea vifo 1,000 (mortality rate) ambayo ni asilimia 8.1. Vilevile katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2019 MNH Upanga ililaza wagonjwa 17,230 na kati ya hao vifo vilikua 1,673 ambayo ni asilimia 9.7(mortality rate).

Hivyo basi takwimu kati ya MNI-1-Mloganzila na MNI-1-Upanga za asilimia ya wagonjwa waliofariki hazitofautiani sana ambapo MNH-Upanga ni asilimia 9.7 wakati ni asilimia 10.4 katika robo ya Julai — Scptcmba, 2019. Hatua hii inaonyesha juhudi ambazo zinafanyika za kuboresha utoaji wa huduma katika Mloganzila zinazaa matunda. Moja ya sababu ambazo imeelezwa na mtoa taarifa kwamba Madaktari wanaotoa huduma MNH-Mloganzila ni wanafunzi waliopo katika majaribio si za kweli, hivyo tungependa kufafanua kwamba Hospitali ya MNH-Mloganzila ina Madaktari Bingwa 52, Madaktari wa kawaida 50 na kwa sasa ina Madaktari tarajali 53.

Licha ya Madaktari Bingwa hawa walioajiriwa 1VINH-Mloganzila kutoa huduma lakini pia wanashirikiana na Madaktari Bingwa kutoka MNH-Upanga katika kutoa huduma hapa MNH-Mloganzila. Vilevile hospitali hii ina madaktari wawili waliobobea wenye hadhi ya Profesa kutoka Korea nao wapo wanatoa huduma. Hivyo sio kweli kwamba madaktari ambao wapo mafunzoni wanafanyakazi bila usimamizi kwani hospitali imeweka utaratibu wa kila mgonjwa anayefika kupata huduma anaonwa na Daktari Bingwa kwa ajili ya maamuzi.

Wakati uongozi wa hospitali ukifanyia kazi tuhuma na malalamiko yaliyotolewa juu ya utoaji huduma katika taarifa hii, tunapenda kuutarifu Umma kwamba tangu MNH ipewe dhamana ya kusirnamia hospitali hii, turnejielekeza katika kutatua changamoto zilizokuwepo katika utaaji huduma na kwa kiasi kikubwa imeonyesha mafanikio ambayo yanaonyesha kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa na pia kuna ushuhuda wa wagonjwa ambao wametibiwa na kuridhika na utoaji wa huduma zetu.

Tunawahakikishia Watanzania kwamba huduma zinazotolewa katika Hospitali ya MNH-Mloganzila zimeboreshwa na tunawakaribisha Watanzania wenye jukumu la kuelimisha jamii waje kuzungumza na wataalam na waone jinsi huduma zinavyotolewa ili waweze kutoa taarifa sahihi kwa jamii.

Imetolewa na
Prof. Lawrence Museru
Mkurugenzi Mtendaji,

IMG_20200106_142658_234.jpg

IMG_20200106_142658_235.jpg


Pia soma
1) Rais Magufuli, ukiwa unatoka Chato pitia Hospitali ya Mlonganzila iliyobatizwa Vingunguti

2) Mloganzila yakanusha juu ya taarifa za vifo vya wagonjwa

3) Haya yanayosemwa kuhusu Hospitali ya Mloganzila ni kweli?

Nilianza kuisikia zaidi Mloganzila mwakajana, wakati ndugu yangu akiwa amelazwa hapo. Naye hakuishi tena.

Kwa sasa kuna ndugu yangu anatibiwa hapo. Amefanyiwa upasuaji mara 3, hakuna mabadiliko makubwa. Siamini kuwa inatokana na ukubwa wa tatizo, uwezekano mkubwa ni huduma ya kiwango cha chini.

Majengo tulijengewa na Wakorea Kusini, ni mazuri, yanapendeza. Vifaa tiba navyo ni msaada, na vimejaa sana.

Baada ya kufuatilia kwa wataalam wa pale Muhimbili, taarifa nilizopewa na maprof. watatu tofaiti, ni kuwa hatuna wataalam wenye uwezo wa kuvitumia vifaa tiba vya kisasa vilivyopo pale.

Hata huyu prof. aliyeitoa hii taarifa, kama utakutana naye kama mtu binafsi, hatakosa kukuambia ukweli wa tatizo la Hospitali ya Mloganzila.

Bahati mbaya serikali yetu inaamini tuna uwezo wa kila kitu. Hatuna mipango ya kuwapeleka watu kwenda kujifunza nje ya nchi.

Jitihada kubwa zilizofanywa na Rais Kikwete mpaka kupata msaada huu mkubwa toka South Korea, zimeshindwa kufikia matarajio yake.

Ukweli ni kuwa:

HOSPITALI YA MLOGANZILA INA VIFAA TIBA VINGI VYA KISASA AMBAVYO MADAKTARI WETU HAWANA UWEZO WA KUVITUMIA.

Kama serikali itaendelea na huu utaratibu wa kuzuia watu kwenda kusoma nje, yaliyopo Mloganzila, msitarajie yatabadilika.
Hizi takuwimu wamezipika, simshauri mtu yoyote kupeleka mgonjwa wake muhimbili unless imeshindikana kabisa kupata huduma sehemu nyengine, chance ya ku-survive nasubutu kusema ni less than 1%, si hospital ni execution chamber.

Yamenitokea kwa wagojwa wangu 3, mmoja ameenda kwa maradhi mengine amekufa kwa maradhi mengine yaliosababishwa na either wauguzi au madoctor, mwengine alifariki emergency department after awaiting more than 30 hours bila kupata huduma, mwengine alifariki njiani kuelekea nyumbani after just one hour after being discharged from the hospital eti amepona, hao wote are closed related to me.

nukija kwa marafiki na majirani case ni nyingi JF hapatoshi.

Never ever again, pale nitawachia viongozi waende kupiga picha tu.
MAONI YA WADAU NJE YA JF (Social Media):.


9D0CA4AA-EFD2-46E0-8B75-6E30FADE88E0.jpeg

A094EA67-A257-4AF4-94E3-1DB6E5F5142A.jpeg

28604F45-8AB3-44B1-9245-E292CB484CCF.jpeg

6CAD1054-C53C-4F2A-A63A-A939D3719746.jpeg

87676098-EEAB-4FD3-B555-F39AC0149354.jpeg

DCA8AAC1-7D4E-4BED-8E50-63629FE82E1A.jpeg

DCA8AAC1-7D4E-4BED-8E50-63629FE82E1A.jpeg
 

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Messages
21,121
Points
2,000

Retired

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2016
21,121 2,000
Prof, definitely huwezi kukubali, admission of guilt is very rare in human nature! na data hizo authenticity yake unaijua wewe mwenyewe! We need independent verification of those data.

Two, you might have those numbers of highly qualified personnel, but the question is: Do they attend patients or they leave the duty to the interns? Laxity in our institutions is not a new phenomenon!

All in all jitahidini zaidi for better results. Tunawaamini sana tena sana.
 

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Messages
21,121
Points
2,000

Pakawa

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Messages
5,704
Points
2,000

Pakawa

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2009
5,704 2,000
Muhimbili Mloganzila ni death penalty. Hawa madaktari waliojifunzia udaktari bongo na kupata degree za kuungaunga ni wauaji.

Wanajivalisha hizo white coats lakini kichwani hamna kitu. Serikali/Wizara ya Afya na Mkurugenzi msije na haya majibu ya ovyo ovyo mnacheza na maisha ya watu.

Hakuna hospitali hapo ni uchafu mtupu. Pelekeni madaktari nje wakajifunze zaidi
Wengi ni failure ndio shida Proffesor.

Professor anza upya maelezo yako hayaridhishi
 

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Messages
1,631
Points
2,000

USSR

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2015
1,631 2,000
Hivi kwanini isitajwe hospital ingine iwe ni hapo tuu?

Hata mwana CCM USSR kaliona hilo. mana huwa wao swala linaloenda tofauti mkisema waonekana sijui huna uzalendo
Hivi nikitoa uthibitisho wa marehemu ,tena ameacha watoto na mke (mama wa nyumbani) kwa uzembe ule

Je wako tayari kufanya uchunguzi kama nitatoka hadharani na ushahidi watamlipa fidia mjane


USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 

FOCAL

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2019
Messages
437
Points
500

FOCAL

JF-Expert Member
Joined Jun 25, 2019
437 500
Yaani kwa MNH-Mloganzila wameweka asilimia za mortarity rate (14.9 to 10.5) bila ya idadi halisi, halafu kwa MNH-Upanga wameweka both asilimia za mortarity rate na idadi kamili ya waliofariki. Ukitumia asilimia peke yake bila kuweka figure halisi unaweza kuwa unataka kuficha kitu fulani, kwani waweza kuona asilimia ni ndogo lakini inawakilisha maelfu ya watu waliofariki.
 

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Messages
7,260
Points
2,000

Titicomb

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2012
7,260 2,000
Julai-September wagonjwa 12,375 vifo 1000. Tafsiri rahisi zaidi kwa kila wagonjwa 120 kuna vifo 10

Tuombe afya njema

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee!
Hivi vifo ni vingi sana kiuwiano.
Sema hii inatokana na wanaopelekwa pale ni kwamba wameshindikana huko hospital za chini na kati.
Kifupi wengi wanapelekwa tayari wanatarajiwa kutopona kirahisi shida zao, they are most likely to die than get cured.
Ukizingatia watanzania wengi hawapimi afya au hawaendi hospital hadi hali iwe mbaya wanakuwa washa chelewa sana.

Hii ni kama kesi za wengi wanaoenda kupima DNA kuhusu paternity test wanakutwa watoto sio wa wanaume wanao hisi wamebambikiwa watoto, sababu hadi wanaenda kufanya vipimo ujue hali mbaya kwenye uaminifu ktk mahusiano yao.
 

Kilatha

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2018
Messages
1,652
Points
2,000

Kilatha

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2018
1,652 2,000
Watoe data rasmi za sababu ya vifo hoja ya mleta mada ilikuwa tatizo la marehemu lilikuwa ni mguu tu ndio lililompeleka na wengine wakidai wagonjwa wao walienda na vidonda (propably vya kisukari) lakini walipoingia humo hawakutoka.

Kama kati ya watu 1000 waliofariki iwapo 200 tu ni kwa matibabu ambayo yalihitaji medical procedures za kawaida watakataa vipi uzembe.

Watoe stats za sababu ya vifo kama wanataka kujibu malalamiko yanayotolewa dhidi yao.
 

FOCAL

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2019
Messages
437
Points
500

FOCAL

JF-Expert Member
Joined Jun 25, 2019
437 500
Ukiwa wafikiria kama great thinker watakiwa uanze kwa kufikiria aina ya wagonjwa wanaoenda Mloganzila. Watanzania wengi wakienda hospitali ujue wako terminally ill, na hospitali huwa kama sehemu ya wao kufia.
Na hili huchangiwa na huduma duni za vipimo kwa maeneo mengi ya nchi, suala ambalo lilizaa utamaduni wa kutofanya hivyo vipimo. Kiufupi huduma za vipimo ni duni sana sana hata kwa bahadhi ya maeneo ya mijini, mtu akiugua ananunua dawa za malaria kumbe ana typhoid, amoeba au UTI.
 

Kilatha

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2018
Messages
1,652
Points
2,000

Kilatha

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2018
1,652 2,000
Hivi nikitoa uthibitisho wa marehemu ,tena ameacha watoto na mke (mama wa nyumbani) kwa uzembe ule

Je wako tayari kufanya uchunguzi kama nitatoka hadharani na ushahidi watamlipa fidia mjane


USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwe na utaratibu sasa wakufunguliana kesi za ‘medical negligence’ vifo ambavyo chanzo chake ni uzembe walipe fidia. Ndio njia pekee yakulazimishana ku maintain professionalism and quality standards kwenye kutoa huduma.
 

Forum statistics

Threads 1,390,620
Members 528,218
Posts 34,056,622
Top