Serikali haina budi kupitia upya sera ya elimu bure

Mr Pixel3a

JF-Expert Member
Sep 15, 2021
5,054
7,263
Elimu ya sasa imewaacha vijana wengi kutojituma kimasomo, hawana uchungu kabisa kupambania viwango vyao darasani na hili ni tokeo la Elimu bure, Na ndio Maana shule binafsi bado zinaongoza kufaulisha wanafunzi kila iitwapo leo.

Hoja muhimu Hawa wanafunzi hawaoni uchungu kabisa Ela inayotolewa na serikali kuwasomesha, kama mdau nashauri kuwepo na kiwango kutoka kwa Wazazi kuchangia gharama za Elimu na hii itampa hali ya kupambania jasho la mzazi kwa kusoma kwa Bidii.

Nakaribisha maoni, mitazamo, ushauri, sera
 
Kwa hiyo gharama ambazo kijana anamsababishia mzazi ni ada pekee, vipi msosi anaokula daily wenyewe hauwezi kufanya asome kwa machungu ili aje amsaidie mzazi. Kuna nchi mfano Norway elimu ni bure hadi chuo kikuu wewe unaona wenge serikali kuwekeza pesa kwa ajili ya elimu ya vijana wake. Kwa maneno mengine unaishawishi serikali isitekeleze wajibu wake kwa wananchi.
 
Tatizo sio free education. Vijana hawajui wanasoma iweje... Kama ajira hamna na hakuna wa kuwapa hamasa na maarifa ya Maisha.... Motisha ya kusoma itoke wapi?
 
Ccm haiko tayari kubadilisha elimu ,katiba ,time huru kufanya hvyo Ni anguko la ccm ,ccm inapenda watu kuwa wajingaa tu
 
Back
Top Bottom