Series (Special thread)

Kuna series moja kali sana kwa wale wapenzi wa series za school life. Inaitwa RIVERDALE.

Humo ndani kuna Drama & Romance.
Kama tunavyojua wenzetu uzunguni huko huwa wanaanza kula life wakiwa sekondari tofauti na huku kwetu mpaka uingie chuo. Kwahiyo ma-party, mapenzi nini japo kwichi kwichi sio sana..

Nilichopendea mule wamepangilia visa vizuri sana na huwezi choka kuangalia.
Nakumbuka niliimaliza Season ya 1( Each episode takes 40 minutes) ndani ya siku moja yani sikutoka nje, ilikuwa ni mwendo wa Series/Toilet/Series/Msosi/Series/...


Chengine cha kuongezea, hawa jamaa wanaotengeneza hizi series huwa wanatupatia sana! Yani wanachagua mademu wakaliii ilimradi tu watupate wakina sisi.
Humo ndani kuna mademu warembo kichizi. Kuna demu humo namkubali sana, ni blonde hivi anaitwa Betty Copper.. Hhm nyie! Kweli wazungu wazuri wapo.

Kuna mdau anaitwa Archie, jamaa anapendwa sana na mademu. Aliwahi kutoka mpaka na mwalimu wake anaefundisha Music
.
Hizi bahati tungepata wakina sie sijui ingekuwaje.

Kama unapenda series za namna hii basi hii si ya kukosa, japo mzigo una Season 4 complete.
 
Daaah nimeingizwa chaka nikajikuta nashusha Ozark mzigo mzima! Meh nimejuta na nimefuta bila kumaliza! Kuna wana JF wana roho kama wajumbe!
Sijui aliekwambia alikuaminishaje.ila kama ni mtu wakupenda visa vya taratibu iko poa tu hasa season 3 naona imekaa poa zaidi.
 
Daaah nimeingizwa chaka nikajikuta nashusha Ozark mzigo mzima! Meh nimejuta na nimefuta bila kumaliza! Kuna wana JF wana roho kama wajumbe!
Utakuwa unapenda series za action na za vurugu kama Banshee.. Ukikaa ukatulia Ozark ni mzigo mkali sana

Nasubiri final season yake ya 4
 
Ahahaaaaaah!
Reddington AKA Maneno Kumi au Mr Mboyoyo!
Anasoma sana vitabu huyo muhuni.
 
Nilikuwa sijaichek condor season 2 weekend nikapakua mzigo nikakaa na savanna pemben kuchek season 2 kutokana na mishe mishe za season 1 nikawa na hamu kinouma kuchek unyama wa yule demu CIA black ops wazee wa clean up mission mama mamaaa jamaa wemetoa UTOPOLO haijawahi tokea sijui walikurupuka washenzi hawa season 1 bonge LA series ila season 2 wamezingua kinouma
 
Sana mzee, ilikuwa ni bora u mess up na Franklin ila sio huyo dogo mwenyewe afro


Umeicheki Animal Kingdom?
Yeah! Mzee nimeicheck mwanzo mpaka season ya mwisho kuitoa si mchezo humo bibi anaijenga empire yake ya wizi mwisho wa siku wanaanza kusalitiana
 
Ni mawazo yako na sikupingi Ila Hanna Ni nzuri na inaendelea na into the Badlands imesitishwa kwa kua na story ya kitoto na ndo maana China imebadilika asa hivi haitoi muvi za mapigano ovyo ovyo kama zamani.
Kaitafute strikeback ndo itakufaa au treadstone Ila kwa vile unapenda TV shows hata kama wakiwa mabubu basi angalia strikeback
 
Ukiachana na watoto wazuri aisee hii series ina story moja unique Sana yaani iyo iyo Riverdale ni kama kusema mbwinde ya marekani Kuna drama balaa yaani Kuna mda unabaki mdomo wazi kutokana na mwanzo unaona series imekaa kitoto Sana lkni unabaki unaumiza kichwa mzee kujua mwisho wake upoje, mim nimeangalia hadi season ya 3 Ila ya 4 nimeishusha bado sijaiona nimeweka pending
 

Attachments

  • IMG_20200804_163547_596.jpg
    25.8 KB · Views: 17

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…