Series (Special thread)

Ewaaaaa upo sahihi kabisa sequel ambayo ingemake sense ni ya Agron na Nasir wake,
Kuanzia uandishi hadi budget vyote hovyo tu,
Sasa mtu alishafyekwa kichwa mara karudi anafanya ujinga ujinga tu,
Bora walivyoitupia kwenye dustbin
 
unajua ile namna unamaliza tu kutazama movie kisha unazima zako taa ukalale..!? mara usikie kishindo, mara uhisi mtu anakugusa, hivi mateso huwa ni ya nini.!??
Yani juzi nimeota ndoto nakimbizwa na kuku wengi sina hamu! Kwanza vile vishindo vya kwneye movie vinavyoshtua🙆🏽‍♀️ Kwahiyo sitaki kabisa hizo habari!
 
Duh, unajua kwenye movie kila mtu kuna kitu anapenda. Ila hi movie ilikuwa ni stori ya kibabe sana hasa kuhusu loyalty, ile scene ya mwisho jamaa aliiwangalia ahmed na mke na mtoto akaona amewaingiza mkenge. Kama unamoyo mdogo unaeza huzunika sana.
kuna watu wanataka ngumi mkononi, siyo wapenzi wa kufuatilia story kama story..! Mimi huwa natazama movie kwa umakini balaa kiasi kwamba ningekuwa serious shule hivyo sahii ningekuwa mbali..!😒
 
Wewe calreen nilikimbizwa na kikundi kikubwa cha kuku mtaa kwa mtaa🤣
We isikie tu na wana mbio jamani🙌🏾
nakuelewa mamaqe..!
Mimi on real life niliwahi teswa na jogoo tena mmoja tu, nadhani alijua mimi ni mnyonge wake, kila nikipita hiyo njia ananikimbiza, nilikuwa nikipita hiyo njia nakimbizwa huku nalia,

na ndiyo ilikuwa njia ya kwenda dukani, kuna siku nilikimbizwaa, nikaanguka, nikamwaga masukari na majani ya chai niliyoagizwa, kipindi kile wanafunga vitu kwenye magazeti,

nikaacha hapo hapo hata vilivyobaki sikuokota, akaenda Mama kuvifata mwenyewe, wakaacha kuniagiza dukani kwa muda..!

hakuna siku nilifurahi kama kujua yule jogoo amechinjwa, yaani nilifurahi kama vile adui yangu kajikwaa kwenye kidole kidogo cha mguu..!😁😁
 
Khee🤣🤣🤣

Kuku akijua udhaifu wako atakutesa sana🤦🏽‍♀️
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…