Series (Special thread)

valhalla nasikia wamei cancel
Umenifanya nikaangalie ni kweli japo wanasema hawajaicancel bali imeisha, walipanga seasons ziwe 3 tu, sasa mbona bado imeacha shauku ya kuendelea? Wengine wanasema ni personal interest kati ya makampuni mawili Netflix na Amazon kitu ambacho naona ndio jibu kuliko kusema imeisha, wamenikera sana
 
Wanakera mno, sasa hatutajua vita ya uongozi ilikuaje baada ya king Canute kufa, Harlad hajakutana na mwanaye
 
Valhala ukiangalia ilikua bado na story ila wameirush iishe wengine wanasema sababu ni views kidogo
 

Kama unapenda movie za mystery itafute hii ni nzuri, inahusu jamaa mmoja anashukiwa kumuua mke wake, akiwa anawakimbia polisi akaingia kwenye nyumba moja na kulikuwa na msichana ndani, na huko kukatokea mauaji mengine ya mume wa yule msichana, wote wakapelekwa polisi ila kila mmoja akawa anatoa maelezo tofauti ya tukio lilivyo tokea, na connection ya mauaji yote mawili.

‎Haina ngumi wala nyimbo zao ni story tu, hata kama hupendi movie za kihindi jaribu kuangalia hii, imeandikwa na ku directiwa vizuri
 
wanajitahidi hawa watu siku hizi, japo niliwahi kufanya nao kazi pahala nikawakinai balaa, nilitazama movie yao flani majuzi inafundisha mno pia, inaitwa CRAZXY, ukipata muda unaweza itafuta..!!
 
Sijui kwanini tu nilishapoteza imani na wahindi kwenye movies zao japokua siku hizi naona ona wanatoa actions movies zinazosemwa kua ni kali ila kwangu moyo unakuaga mzito ku download au kustream movies zao. Najitahidi nianze kuwazingatia ila nashindwa several times.
 
Hii haina ngumi zao za uongo hii ni pure story tu 😃😃
 
Hawa mabwana wamezidi uwongo

Ndio maana muvi zao nyingi tunakuwa na mashaka nazo 😃😃
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…