Nakumbuka miaka mitano iliyopita aliyekuwa
nguli wa filamu Nchini Tanzania marehemu
""Steven Kanumba"" alienda kwenye jumba la
Big Brother....
amini usiamini bila sababu yyte ya maana
watanzania ndo walikuwa wa kwanza kuanza
kumsema kuwa hajui kuvaa, nani alimchagua ,
hajui kiingereza mpaka kufikia kumuigiza!!!
Walisahau hata watu maruufu kama Messi na
wengine wengi hawajui kuongea kabisa lugha
hiyo..
Baada ya kifo chake watanzania hawahawa
wakaanza kusema alikuwa nguli
aliyetuwakilisha vizuri nje ya nchi na kulia
sana!!!kumbe wakati akiwa hai tulikuwa
tunamshusha chini..
Miaka mitano baadae Tanzania imempata mtu
anayeiwakilisha vizuri nje ya mipaka na
kuitangaza vizuri nchi yake..
Pasipokuwa na sababu za msingi (chuki binafsi
tu)anapangiwa njama za kuzomewa na
kuabishwa katika ardhi ya nchi yake ambayo
kwa namna moja au nyingine kuna watu
wameifahamu sababu yake!! Ukiuliza sababu za
wengi wao kumchukia ni mafanikio yake lakini
hata kama humpendi mtu hivi ndo hadi
umzomee kwa kiasi kile !!!
leo na kesho naye huyu akitoka utaskia
hawahawa waliokuwa wanamzomea wanaanza
kusema jamaa alikuwa anatuwakilisha vizuri
sana , ametutangaza sana kimataifa!! lakini
Watanzania wenzake ndio vinara wa
kumuangusha..
Si lazima kila mtu ampende Diamond ila
kutumia nguvu kubwa sana kumuangusha mtu
ni ishara ya uwoga na Roho ya kimaskini...
Nimeamini ""maisha bila unafki hayaendi""