Hii tume ya marekebisho ya mitaala ya elimu ukitazama mapendekezo yao ni wazi hawana uwezo wa kukwamua elimu ya Tanzania. ukitazama mapendekezo unaona kabisa ni watu ambao kwanza hawana taarifa kama elimu yetu ni mbovu, yawezekana ni watu walewale waliokuwa wakifundisha wakati hawajui kama wanayofundisha hayaleti tija.
Chimbuko la maboresho ni kelele za wananchi, jambo la kwanza ilitakiwa tufanye utafiti kujua changamoto zetu na pili kutizama mpango wa maendeleo wa Taifa. Huwezi kuandaa mitaala ya elimu bila kuwa na mpango wa maendeleo wa taifa lakini.
Ukitazama mapendekezo yao ni kwamba wanatatua kitu wasichokijua na pili wamemaliza kuandaa mitaala mipya wakati serikali inazindua kuandaa mpango wa maendeleo.
Niishauri wizara isikimbilie kuleta mabadiriko haya ambayo hayana tija.
Toeni mda wa watanzania kutafakari na kujiridhisha.
Chimbuko moja wapo la ubovu wa elimu ni mitaala kuandaliwa bila kufuata mipango ya maendeleo, kwamba huko nyuma tulifundishwa mambo ambayo hayaendani na maisha ya leo wakati changamoto tunazokutana nazo leo hatukuandaliwa. sasa unapoona tuko kwenye changamoto kama hiyo alafu mtu anayekwenda kurekebisha bado anafanya makosa yaleyale unajua huyu hajui anachokifanya na hawezi kutatua. ndiyo maana nikasema wangeanza kufanya utafiti kujua changamoto za elimu yetu ni zipi?
Mimi nilitamani sana kutoa kitabu cha "MABARIDIRIKO YA SERA NA MITAALA KUELEKEA TANZANIA YA 2050", lakini naona mda umebana sana tangu hawa jamaa wametoa rasimu mpaka mwisho wa kutoa maoni.
Upo umuhimu mkubwa sana wa kuhusisha mipango ya maendeleo katika kutunga sera na mitaala ya elimu.
Mfano serikali ikishatoa Dira kwamba tunataka kwenda wapi kufikia 2050, ni lazima kila wizara ichore ramani za kufikia malengo yao.
Tuchukulie mfano wizara ya kilimo inaweza kusema tunataka kufikia uzalishaji huu ifikapo 2050, na ili tufike huko tunahitaji wananchi washiriki hivi, wataalamu washiriki hivi na kila mmoja akitumia njia hizi stepu kwa stepu.
Huwezi kuwachukua wananchi wote ukawape kozi ndiyo walime, maana yake ni lazima elimu hii inayotolewa mashuleni impe basic knowledge.
siyo swala la kumfundisha somo la kilimo ila mkishajua mpango ni kutumia wataalamu kuwaongoza wakulima ila lazima huyu mkulima awe na uelewa fulani. Elimu ya sayansi inaweza kujikita katika elimu ya mimea badala ya kufundisha mambo ya kipuuzi kama formula za photosynthesis kwa watoto wadogo ambayo hayana maana wala tija kwa wanaobaki elimu za chini, elimu hiyo ijikite kumfahamisha mtoto mambo muhimu yanayohitajika kwa mmea ili kuwa na afya, mtoto anaweza kujua namna kubaini kwa kuangalia majani ya mimea kwa waliokwisha kupanda au kupima udongo kwa wanaojiandaa.
Mwananchi ajue huduma hizi atazipata kwa msaada wa wataalamu wala hahitaji kukalilishwa mambo haya.
Kilimo ni biashara ni lazima somo la biashara limueleze namna na umihimu wa kulinda ubora, kutafuta mitaji, kutafuta wateja n.k.
sasa elimu yetu ya sasa imejikita kufundisha vitu watu wanavyoamini ni sayansi lakini useless maarifa na ukienda njiani mtu akikuuzia ndoo ya nyanya unaweza kufika nyumbani ukakuta nusu ndoo, au chini zote mbovu. Juzi nilimuona balozi wa tanzania china akilalamika watu kuweka mawe kwenye njegere, hawa huwezi kuwalaumu hawana elimu. lakini unapoona msomi anaandaa vitu kuwakalilisha watoto visivyotoa elimu za kukabiliana na changamoto zilizopo. wanafundisha mambo genera hata yasiyokuwa na maana. tatizo hili la kuweka uchafu kwenye mazao ya kilimo lilikuwepo tangu miaka ya 90 wakati niko sekondari, leo hii miaka 30 baadae bado lipo na watunga sera hawatazami kwenye jamii kuna shida gani?
Ubovu wa elimu yetu una sababu nyingi na haya mambo mengine ni athari zilizotokana na mizizi ya tatizo.
Kitu cha kwanza ni lazima tufanye utafiti, kama watanzania wanasemekana ni wavivu lazima tutizame our parenting style kujua ni wapi tulipokosea katika malezi na tuweke mwongozo unaolenga kutatua.
Hapa tulipo tunatakiwa kutumia maarifa ya kisayansi kuboresha elimu yetu lakini nahisi waliotumika kuandaa sera na mitaala mipya wao wenyewe ni wahanga wa mitaala mibovu.
Elimu yetu kwa sasa ni sawa na kilimo cha jadi, mama yangu alikuwa analima shamba ekari mbili, lakini akisikia wanasema mti fulani ni dawa anachukua na kuleta kupanda shambani, akisikia hiki ni chakula analeta na kupanda. mwisho wa siku shamba lina mazao mengi lakini mavuno kidogo, bado hajitoshelezi anaishi kwa umasikini. kila anachosikia kina faida analeta na kupanda shambani. hana malengo bali anapanda chochote anachosikia kina faida.
Wataalamu wetu wamefanya elimu yetu kutokuwa na malengo, wakisikia jambo fulani wanaingiza tu. elimu imejaa mambo kibao anayojifunza mtoto lakini akimaliza maarifa ya kumsaidia sifuri. ni lazima elimu iwe na malengo na hakuna mtoto afundishwe upuuzi usiokuwa na tija