idawa nadhani utakua haujamuelewa vizuri Halima Mdee, sheria ya Ardhi nchini inampa mamlaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumpa/kumnyang'anya/kumuongezea hati ya umiliki/kubatili haki ya umiliki kwa mtu yoyote anaemiliki ardhi kwa ridhaa/bila ridhaa yake, na kwa kumlipa fidia au bila kumlipa fidia.
Mara nyingi Ardhi inapogundulika kua ina madini au rasilimali nyingine chini, wananchi hua wanahamishwa kwa kulipwa fidia ya ARDHI tu (na si fidia za rasilimali iliopo katika ardhi yake au thamani ya kiwanja baada ya kugundulika kwa hizo rasilimali).
Mfano,
Una kiwanja, umekinunua Sh Milioni 1, kikagundulika kina madini ya dhahabu chini, utapewa hela ulionunulia hicho kiwanja na maendeleo uliofanya katika hicho kiwanja tu (kama vile kujenga nyumba, kupanda miti n.k) ila hautapewa fidia ya thamani ya hicho kiwanja baada ya ugunduzi wa hayo madini. Kawaida kiwanja hupanda thamani baada ya kugundulika kua kina rasilimali.