Sera Mpya ya ardhi, Kaburi jipya la CHADEMA

Sera Mpya ya ardhi, Kaburi jipya la CHADEMA

Tungepewa hiyo sera ya Ardhi ilivyo kwenye sera ya CDM na ufafanuzi wake alafu ndo tuanze kuijadili lakini kwasasa nifujo tu wala haijaeleweka
 
Mbona inaeleweka..maana yake rasilimali kama madini zitamilikiwa na wachache..ingekuwa hivyo leo tanzanite isingekuwa ya tanzania..ingekuwa ya mzee Ngoma na familia yake..nilichogundua hapa ni rahisi ukiwa nje kuona makosa ndani ya uwanja..chadema hawajachukua hata nchi wameanza kuleta ubinafsi
Hiyo tanzanite ni mali ya serikali au serikali inachukua kodi tu?
 
Mwenye jukumu la kuelimisha jamii ni Chadema wenyewe ambao ndio watunga sera.....kitu gani hujakielewa hapo kuhusu hiyo....

Au jiwe tuseme mkate ndio utafurahi
Ndio yale yale ya CCM mtu akihoji.

kuhusu maswala ya kitaifa inaonekana anapinga juhudi za raisi

Kwa nini watanzania hatupendi utamaduni wa kukosoana.
.
Mkuu huyu hajaandika kuelimisha jamii juu ya hii sera bali kupambana na chadema.Amefeli.
 
Tungepewa hiyo sera ya Ardhi ilivyo kwenye sera ya CDM na ufafanuzi wake alafu ndo tuanze kuijadili lakini kwasasa nifujo tu wala haijaeleweka
Naona bado hawajaiweka mtandaoni, ni vyema waiweke hadharani tuisome.
 
Mwenye jukumu la kuelimisha jamii ni Chadema wenyewe ambao ndio watunga sera.....kitu gani hujakielewa hapo kuhusu hiyo....

Au jiwe tuseme mkate ndio utafurahi.
Kilichokuleta wewe humu na huna ufafanuzi ni nini km ufafanuzi ni jukumu la chadema? .Basi kwa mtu mwenye ufahamu na muungwana mwenye nia njema ungeleta bandiko lako km mwanachi kuomba CHADEMA WATOE UFAFANUZI kwa manufaa ya wengi.wakati mwingine utoto unazidi. Kwa mambo mazito na ya msingi km haya tafuta hata uelewa kwa wanye upeo ndio uje humu.
 
Naona bado hawajaiweka mtandaoni, ni vyema waiweke hadharani tuisome.
Wewe umetoa wapi au ni miongoni mwa walioketi kutunga hiyo sera,na je wakiiweka hadharani na ikwa hicho kifungu hakisomeki hivyo tukueleweje .kwa majibu haya tuna vichaa nchi hii kuliko tunavyodhani. Unajibu upuuzi upuuzi tu. Km mwehu.
 
Kama mwisho wa kufikiria wa 'think tanks' wa Chadema umekomea hapa, bora CCM iendelee tu kushika hatamu na turudi kwenye chama kimoja!
 
Wewe umetoa wapi au ni miongoni mwa walioketi kutunga hiyo sera,na je wakiiweka hadharani na ikwa hicho kifungu hakisomeki hivyo tukueleweje .kwa majibu haya tuna vichaa nchi hii kuliko tunavyodhani. Unajibu upuuzi upuuzi tu. Km mwehu.
Kijana punguza povu, hiyo twitter ni ya Halima Mdee akiwa ameinukuu toka kwenye sera mpya ya chadema..
 
Wakati mwingine mtu anaweza kuchokoza mada ili tuichimbe kiundani. Maelezo yake yanatosha kutufikirisha kama sera hii ndio tiba bora against sera iliyopo? Au sera iliyopo inahitaji marekebisho kidogo tu hasa kwenye kumfaidisha mmiliki wa ardhi pale panapokuwa na ugunduzi?

Naam ww hasa ndio umefahamu nini tunakipata kwenye hii mada. Kwa sasa sehemu pekee kwenye mijadala huru na inayoweza kupata uchangiaji mujarabu ni huku kwenye social media hususani JF, hasa inayohusu wapinzani kuwasiliana na watanzania wote. Mjadala wa hivi huwezi kuupata kwenye redio au television. Hapa hao viongozi wa cdm wanaweza kuona ubora/mapungufu ya sera yao na pia wananchi wanaweza kuiboresha au kuiponda sera hiyo kwa uwazi. Hongera mtazamo kwa kuona hili kwa jicho la 3D.
 
Kilichokuleta wewe humu na huna ufafanuzi ni nini km ufafanuzi ni jukumu la chadema? .Basi kwa mtu mwenye ufahamu na muungwana mwenye nia njema ungeleta bandiko lako km mwanachi kuomba CHADEMA WATOE UFAFANUZI kwa manufaa ya wengi.wakati mwingine utoto unazidi. Kwa mambo mazito na ya msingi km haya tafuta hata uelewa kwa wanye upeo ndio uje humu.
Tusaidiane tu ataelewa umuhimu wa kuweka thread inayojitosheleza.
 
Kijana punguchallenge huu, hiyo twitter ni ya Halima Mdee akiwa ameinukuu toka kwenye sera mpya ya chadema..
Mm nakuhoji ww uliyeleta humu na kuiponda hoja na ukipata challenge huna pa kushika. Narudia tena na nakushauri busara na uungwana ungeweka ushabiki pembeni ukawa na fahamu zako zote ukaomba ufafanuzi kwa wahusika. Ungeyachallenge majibu au ufafanuzi wao.
 
nimeamini chadema ni chama cha mabwanyenye....hii sera ni kinyume na katiba
 
idawa nadhani utakua haujamuelewa vizuri Halima Mdee, sheria ya Ardhi nchini inampa mamlaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumpa/kumnyang'anya/kumuongezea hati ya umiliki/kubatili haki ya umiliki kwa mtu yoyote anaemiliki ardhi kwa ridhaa/bila ridhaa yake, na kwa kumlipa fidia au bila kumlipa fidia.

Mara nyingi Ardhi inapogundulika kua ina madini au rasilimali nyingine chini, wananchi hua wanahamishwa kwa kulipwa fidia ya ARDHI tu (na si fidia za rasilimali iliopo katika ardhi yake au thamani ya kiwanja baada ya kugundulika kwa hizo rasilimali).

Mfano,

Una kiwanja, umekinunua Sh Milioni 1, kikagundulika kina madini ya dhahabu chini, utapewa hela ulionunulia hicho kiwanja na maendeleo uliofanya katika hicho kiwanja tu (kama vile kujenga nyumba, kupanda miti n.k) ila hautapewa fidia ya thamani ya hicho kiwanja baada ya ugunduzi wa hayo madini. Kawaida kiwanja hupanda thamani baada ya kugundulika kua kina rasilimali.
Unaifahamu sheria ya rasilimali za nchi?
 
Unaifahamu sheria ya rasilimali za nchi?
Vizuri sana, pengine kuliko unavyofikiria.

Tanzania Mineral Act, Chapter 123 of The Laws Of Tanzania. (Act No.14 ya 2010)

Imefanyiwa mabadiliko mara ya kwanza baadhi ya vifungu na sheria ya Finance Act of 2017, halafu ikaja kufanyiwa mabadiliko tena na sheria nyingine ya Miscl. Amendment Act of 2017, iliokua published tarehe 07.07.2017 katika gazeti la serekali toleo namba 27, volume 98).

NB pia sheria ya rasilimali ina uiano na sheria nyingine nyingi tu, kama vile Finance Act, Land Act, Companies Act, Tanzanian Tax Laws n.k
 
Isome basi
 
"2. USIMAMIZI WA ARDHI: Chadema itaanzisha mfumo wa umiliki wa ARDHI ambapo kila MWANANCHI atamiliki ardhi na rasilimali zake JUU na CHINI ya ARDHI hiyo. TOFAUTI na CCM, Chadema HAKIAMINI katika KUFUKUZA watanzania kwenye ARDHI YAO kufuatia UGUNDUZI wa MADINI."
===========================

Chadema hili swala la ardhi litawamaliza, Kama Baba wa Taifa angefuata hii sera yenu leo kungekuwa na mtu mmoja mwenye uwezo wa kumiliki mkoa mzima na kila kitu kilichomo ndani yake.
View attachment 880155
umetafsiri kichwa chini miguu juu ! shukrani pekee ninayokupa ni kuendelea kusambaza sera ya chadema ya 2018 kwa wananchi , nadhani sasa utakubaliana nami kwamba CHADEMA NDIO INAYOTOA DIRA NA MWONGOZO WA NCHI .
 
Mkuu binafsi nimeipongeza Chadema kwa kuja na kitu ambacho kitatusaidia kujua wao wanasimamia nini. Sasa inabidi wote waelewe sera yao ili wajue wapi waunge mkono serikali na wapi wapinge badala ya hii pingapinga isiyo na macho.

idawa amegusa sehemu tu ya sera ambayo naamini imeamua tu kuwa kinzani na sera ya CCM lakini haina mantiki. Labda tulete sera ya sasa ya ardhi vs hii ya chadema ili tuelewe nini anachogusia idawa.
Ni kweli ndio maana hata Halima Mdee amerusha kipande tu cha hiyo Sera, ni vyema angeiweka sera nzima kuhusu Ardhi tungeelewa zaidi... Hata hivyo hicho kipande kidogo kinaonyesha taswira nzima ya sera ya Chadema kuhusu ardhi...
 
Back
Top Bottom