Sera Mpya ya ardhi, Kaburi jipya la CHADEMA

Sera Mpya ya ardhi, Kaburi jipya la CHADEMA

Hapana mkuu tatizo ni premise uliyoitumia ku set premise yako. Hiyo ni sera jaribu kufanya deep analysis katika kuchambua athali zake badala ya ulivyofanya.
Wakati mwingine mtu anaweza kuchokoza mada ili tuichimbe kiundani. Maelezo yake yanatosha kutufikirisha kama sera hii ndio tiba bora against sera iliyopo? Au sera iliyopo inahitaji marekebisho kidogo tu hasa kwenye kumfaidisha mmiliki wa ardhi pale panapokuwa na ugunduzi?
 
Mkuu kumbuka sera ya Taifa inasema ardhi ni mali ya serikali msimamizi mkuu akiwa Raisi...... hivyo hiyo sera mpya ya Chadema wanamaanisha ardhi itakuwa mikononi mwa wananchi wenyewe yaani ni juhudi zako kununua ardhi na kujimilikisha....bila kujali athari kwa kizazi kijacho.
Kununua kutoka kwa nani na kujimilikisha kivipi.

Nini maana ya kujimilikisha?
Tulia upate uelewa kabla ya kutafuta kutwa.
 
Bonta kwenye wimbo wake mmoja aliwahi kuuliza "mbezi kuna nini lami hadi ndani, shinyanga kuna dhahabu vumbi hadi ndani"... Huu ndo ukweli kwamba viongozi wamekua wanahamisha utajiri wa maeneo yenye madini nakuwaachia wazawa mashimo na vyumbi, kibaya zaidi utajiri unaelekea ulaya kama gesi yetu ilivyonyang'anywa na mabepari(JPM)...ndg yng ukweli ni kwamba Tanzania hajavamiwa tena na wazungu baada ya uhuru,iko wazi viongozi kupitia ccm waliwapa mabepari rasilimali zetu kwa mgongo wa " wawekezaji". CDM imepigana kadiri walivyoweza kutuamsha ili kuona kuanzia operesheni sangara hadi kudai sera ya gesi kabla yakugawa vitalu, yaani ni ww mleta mada na viongozi wachache mlingia mtaani na vifaru kule Mtwara kuwatawanya wananchi wanaotaka gesi yao isitoroshwe, Miaka michache imepita tokea muwakebehi wanamtwara leo mnaungana tena na JPM kulalamika gesi yetu inaibiwa...kwa kifupi idara yetu nyetu T..I..S ukiongezea na Jioni Wali(JW) mnatumika km kondomu mmewasaliti umma na mmegeuzwa kondoo wa wanasiasa mnageuzwa geuzwa kama samaki anayeliwa

Nadhani ile kauli ya gesi tumenyang'anywa ingetosha kuanzisha vita ya ukombozi mpya. CCM wametuuza utumwani. Tujikomboe kutoka kwenye makucha ya hawa walaghai
 
Tueleweshe mkuu kwa faida ya wengi.
Kununua kutoka kwa nani na kujimilikisha kivipi.

Nini maana ya kujimilikisha?
Tulia upate uelewa kabla ya kutafuta kutwa.
 
pint ya halima mdee hapo ni kuwa serikali inatumia kigezo cha ardhi kuwa chini yake kuwadhulumu wananchi hasa pale paapotokea maliasili chini ya ardhi hiyo.mwananchi anayeishi hapo wengi wao huwa wanadhulumiwa hapa fidia hawapewi
Mimi ninaamini ndani ya ccm siyohatuko salama kabisa imagine tuko maskini kuliko nchi zote duniani na bado wanasema kuunga mkono juhudi za ........
 
Hivi Chadema walipopitisha kuwa mtu amiliki chote kilicho chini ya ardhi hivi kulikuwa Na mtu yeyote aliyesoma jiografia? Wataalamu wa jiografia walihusishwa? Dunia wote tunavyojua ni duara .Tunafahamu lile tufe la dunia.Ujue hata choo ukichimba moja kwa moja unajua shimo lake laweza tokezea chumba kwa Trump? Angalia piga picha ukitoboa hapo ulipo mpaka mwisho wa tufe la Dunia utatokezea wapi.Kila upande wa tufe ukiamua mfano uchimbe choo hadi mwisho wa tufe la Dunia Kila binadamu Duniani lazima akutane Na mtu wa kupigana naye Kila mmoja akidai hilo ni eneo ni lake liko chini ya ardhi yake.Itakuwa Vita si ya Dunia tu lakini kwenye uchimbaji huo utauchimba muhimbili wa Dunia ule ambao husingizia Na ukikatika utabwa binadamu wote hewani kwa kukosa balance
 
Kama medi
Nadhani ile kauli ya gesi tumenyang'anywa ingetosha kuanzisha vita ya ukombozi mpya. CCM wametuuza utumwani. Tujikomboe kutoka kwenye makucha ya hawa walaghai
kama media ingekuwa huru wahuni wnaohama tungeruhusu wafanye mdahalo wa wazi uwanja wa Taifa watueleze wanaunga makono katika eneo gani na hasa pale tynaambiwa Madini na Gesi wamechukuwa wakoloni .
 
Chukulia chini ya ardhi ya halima Mdee kumegunduliwa chanzo cha maji cha kunywesha Jimbo lake lote la uchaguzi.Kwa hiyo hayo maji yawe Mali ya Halima Mdee watu wa Jimbo la kawe wafe kwa ukosefu wa maji ?
 
Hivi Chadema walipopitisha kuwa mtu amiliki chote kilicho chini ya ardhi hivi kulikuwa Na mtu yeyote aliyesoma jiografia? Wataalamu wa jiografia walihusishwa? Dunia wote tunavyojua ni duara .Tunafahamu lile tufe la dunia.Ujue hata choo ukichimba moja kwa moja unajua shimo lake laweza tokezea chumba kwa Trump? Angalia piga picha ukitoboa hapo ulipo mpaka mwisho wa tufe la Dunia utatokezea wapi.Kila upande wa tufe ukiamua mfano uchimbe choo hadi mwisho wa tufe la Dunia Kila binadamu Duniani lazima akutane Na mtu wa kupigana naye Kila mmoja akidai hilo ni eneo ni lake liko chini ya ardhi yake.Itakuwa Vita si ya Dunia tu lakini kwenye uchimbaji huo utauchimba muhimbili wa Dunia ule ambao husingizia Na ukikatika utabwa binadamu wote hewani kwa kukosa balance
Duh!
 
Kwa hakika hauijui Kenya na Migogoro ya Ardhi jinsi inavyowatafuna.
Naijua kwa sababu nimesoma huko. Aidha, ndugu zangu wanaishi huko. Kama unavyofahamu makabila ya mipakani yana ndugu pande zote.
 
Naijua kwa sababu nimesoma huko. Aidha, ndugu zangu wanaishi huko. Kama unavyofahamu makabila ya mipakani yana ndugu pande zote.
Sidhani kama unaijua just for a simple fact ya kwamba umesoma Kenya! Let's be rational & reasonable katika masuala ya msingi tafadhali!
 
"2. USIMAMIZI WA ARDHI: Chadema itaanzisha mfumo wa umiliki wa ARDHI ambapo kila MWANANCHI atamiliki ardhi na rasilimali zake JUU na CHINI ya ARDHI hiyo. TOFAUTI na CCM, Chadema HAKIAMINI katika KUFUKUZA watanzania kwenye ARDHI YAO kufuatia UGUNDUZI wa MADINI."
=========================Hoja hapa ilitakiwa ufafanue kwa kina juu ya hiyo sera lkn umejitumbukuza ktk tatizo la ushabiki wa vyama.
 
Mkuu unaamini hiyo sera ya Chadema ndio matakwa ya watanzania walio wengi hadi usemame ni sera ya kuombea kura.?

Ikitokea Chadema wakashika madaraka na hiyo sera ikawafanyiwa kazi unaamini itamuondoa mtanzania kwenye lindi la umaskini.?

Ukweli uko hivi, kwa sasa cdm ina mashabiki wengi kinachofanya ukweli huo usitamalaki ni hii dhuluma ya wazi inayoendeshwa na ccm kupitia yenyewe kuwa chama dola. Hivyo wanachofanya cdm ni kucheza na akili za hao mashabiki wake. Ni kama matangazo ya hizi biashara za vodocom, cocacola nk. Ukitaka ukubalike inabidi uwe mbunifu. Wananchi wa nchi hii hata kama wanamatakwa yao hawana uwezo wa kulazimisha kinyume na wanachotaka walioko madarakani au kile kinachopendekezwa na wale wanaowasupport. Mfano mrahisi, kuna mwanacdm alikuwa anamkubali Lowassa kabla ya Mbowe kubadilisha gia angani? Na cdm walipata kura 6m+ za kutangazwa na tume achia za nyuma ya pazia. Itakuwa kuunga mkono hiyo sera ya ardhi?

Mwananchi wa Tanzania hawezi kuondoka kwenye lindi la umasikini kwa kumiliki ardhi tu, bali kwa ardhi anayoimiliki anaitumiaje kumletea maendeleo. Inabidi serekali iwe na mkakati unaotekelezeka ili kujiletea maendeleo kupitia hiyo ardhi. Ili ardhi iweze kumuendeleza mwananchi ni mjadala mwingine. Ukileta uzi huo tunaweza kutoa mawazo yetu.
 
Sidhani kama unaijua just for. a simple fact ya kwamba umesoma Kenya! Let's be rational & reasonable katika masuala ya msingi tafadhali!
Mkuu huyu hajaandika kuelimisha jamii juu ya hii sera bali kupambana na chadema.Amefeli.
 
Back
Top Bottom